1 Wakorintho 10
Onyo dhidi ya sanamu
1 Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari. 2 Wote walibatizwa katika umoja na Mose katika lile wingu na katika ile bahari. 3 Wote walikula chakula kilekile cha kiroho, 4 wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe. 5 Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
6 Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani. 7 Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.” 8 Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000. 9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka. 10 Wala msinungunike kama baadhi yao walivyonungunika, wakaangamizwa na Mwangamizi!
11 Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi ambao mwisho wa nyakati unatukabili. 12 Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke. 13 Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu. 15 Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo. 16 Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo. 18 Angalieni kwa mfano Wayahudi wenyewe: Wale wanaokula tambiko wanaungana na hiyo madhabahu. 19 Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu? 20 Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe nyinyi muwe na ushirika na pepo. 21 Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika Karamu ya Bwana na katika meza ya pepo. 22 Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?
Kila kitu kwa ajili ya utukufu wa Mungu
23 Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga. 24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.
25 Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu; 26 t maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.” 27 Kama mtu ambaye si mwaamini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu. 28 Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile. 29 Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?
30 Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?”
31 Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu. 33 Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.
1 Corinthians 10
1 For I would not, brethren, have you ignorant, that our fathers were all under the cloud, and all passed through the sea;2 and were all baptized unto Moses in the cloud and in the sea;3 and did all eat the same spiritual food;4 and did all drink the same spiritual drink: for they drank of a spiritual rock that followed them: and the rock was Christ.5 Howbeit with most of them God was not well pleased: for they were overthrown in the wilderness.6 Now these things were our examples, to the intent we should not lust after evil things, as they also lusted.7 Neither be ye idolaters, as were some of them; as it is written, The people sat down to eat and drink, and rose up to play.8 Neither let us commit fornication, as some of them committed, and fell in one day three and twenty thousand.9 Neither let us make trial of the Lord, as some of them made trial, and perished by the serpents.10 Neither murmur ye, as some of them murmured, and perished by the destroyer.11 Now these things happened unto them by way of example; and they were written for our admonition, upon whom the ends of the ages are come.12 Wherefore let him that thinketh he standeth take heed lest he fall.13 There hath no temptation taken you but such as man can bear: but God is faithful, who will not suffer you to be tempted above that ye are able; but will with the temptation make also the way of escape, that ye may be able to endure it.14 Wherefore, my beloved, flee from idolatry.15 I speak as to wise men; judge ye what I say.16 The cup of blessing which we bless, is it not a communion of the blood of Christ? The bread which we break, is it not a communion of the body of Christ?17 seeing that we, who are many, are one bread, one body: for we are all partake of the one bread.18 Behold Israel after the flesh: have not they that eat the sacrifices communion with the altar?19 What say I then? that a thing sacrificed to idols is anything, or that an idol is anything?20 But I say, that the things which the Gentiles sacrifice, they sacrifice to demons, and not to God: and I would not that ye should have communion with demons.21 Ye cannot drink the cup of the Lord, and the cup of demons: ye cannot partake of the table of the Lord, and of the table of demons.22 Or do we provoke the Lord to jealousy? are we stronger than he?23 All things are lawful; but not all things are expedient. All things are lawful; but not all things edify.24 Let no man seek his own, but each his neighbor’s good.25 Whatsoever is sold in the shambles, eat, asking no question for conscience’ sake,26 for the earth is the Lord’s, and the fulness thereof.27 If one of them that believe not biddeth you to a feast, and ye are disposed to go; whatsoever is set before you, eat, asking no question for conscience’ sake.28 But if any man say unto you, This hath been offered in sacrifice, eat not, for his sake that showed it, and for conscience sake:29 conscience, I say, not thine own, but the other’s; for why is my liberty judged by another conscience?30 If I partake with thankfulness, why am I evil spoken of for that for which I give thanks?31 Whether therefore ye eat, or drink, or whatsoever ye do, do all to the glory of God.32 Give no occasions of stumbling, either to Jews, or to Greeks, or to the church of God:33 even as I also please all men in all things, not seeking mine own profit, but the profit of the many, that they may be saved.