previous next

1 KOR. 10

Maonyo kutoka kwa Historia ya Israeli

1  tKwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 twote wakala chakula kile kile cha roho; 4 twote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 tLakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. 6 tBasi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. 7 tWala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 tWala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 tWala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka. 10 tWala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.

11 tBasi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.

13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
14  tKwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 16 tKikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 tKwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 tWaangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 tBasi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20 tSivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 tHamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

22 tAu twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

Fanyeni yote kwa Utukufu wa Mungu


23  tVitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. 24 tMtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. 25 tKila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; 26 tmaana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo. 27 tNa mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri. 28 tLakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri. 29 Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30 tIkiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho? 31 tBasi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 32 tMsiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu, 33 tvile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa. a.

1 CORINTHIANS 10

Don't Worship Idols

1  t Friends, I want to remind you that all our ancestors walked under the cloud and went through the sea. 2 This was like being baptized and becoming followers of Moses. 3 t All of them also ate the same spiritual food 4 t and drank the same spiritual drink, which flowed from the spiritual rock that followed them. That rock was Christ.

5 t But most of them did not please God. So they died, and their bodies were scattered all over the desert.
6 What happened to them is a warning to keep us from wanting to do the same evil things. 7 t They worshiped idols, just as the Scriptures say, “The people sat down to eat and drink. Then they got up to dance around.” So don't worship idols. 8 t Some of those people did shameful things, and in a single day about 23,000 died. Don't do shameful things as they did. 9 t And don't try to test Christ, t as some of them did and were later bitten by poisonous snakes. 10 t Don't even grumble, as some of them did and were killed by the destroying angel.

11 These things happened to them as a warning to us. All this was written in the Scriptures to teach us who live in these last days.
12 Even if you think you can stand up to temptation, be careful not to fall.

13 t You are tempted in the same way that everyone else is tempted. But God can be trusted not to let you be tempted too much, and he will show you how to escape from your temptations.
14 My friends, you must keep away from idols. 15 I am speaking to you as people who have enough sense to know what I am talking about. 16 t When we drink from the cup we ask God to bless, isn't that sharing in the blood of Christ? When we eat the bread we break, isn't that sharing in the body of Christ?

17 By sharing in the same loaf of bread, we become one body, even though there are many of us.
18  t t Aren't the people of Israel sharing in the worship when they gather around the altar and eat the sacrifices offered there? 19 Am I saying that either the idols or the food sacrificed to them is anything at all? 20 t No, I am not! This food is really sacrificed to demons and not to God. I don't want you to have anything to do with demons. 21 You cannot drink from the cup of demons and still drink from the Lord's cup. You cannot eat at the table of demons and still eat at the Lord's table.

22 t We would make the Lord jealous if we did this. And we are not stronger than the Lord.

Always Honor God


23  t Some of you say, “We can do whatever we want to!” But I tell you not everything may be good or helpful. 24 We should think about others and not about ourselves. 25 However, when you buy meat in the market, go ahead and eat it. Keep your conscience clear by not asking where the meat came from.

26 t The Scriptures say, “The earth and everything in it belong to the Lord.”
27 If an unbeliever invites you to dinner, and you want to go, then go. Eat whatever you are served. Don't cause a problem for someone's conscience by asking where the food came from. 28-29 But if you are told it has been sacrificed to idols, don't cause a problem by eating it. I don't mean a problem for yourself, but for the one who told you. Why should my freedom be limited by someone else's conscience?

30 If I give thanks for what I eat, why should anyone accuse me of doing wrong?
31 When you eat or drink or do anything else, always do it to honor God. 32 Don't cause problems for Jews or Greeks or anyone else who belongs to God's church. 33 I always try to please others instead of myself, in the hope that many of them will be saved.