1 KOR. 15
Kufufuka kwa Kristo
1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, 2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. 3 tKwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 tna ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 5 tna ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 7 tbaadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 8 tna mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. 9 tMaana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. 10 tLakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.Kufufuliwa kwa Mwili
12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 tNaam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 16 tMaana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.
19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
20 tLakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 21 tMaana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 23 tLakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 24 tHapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 tMaana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 tAdui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 27 tKwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
29 Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao? 30 tNa sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa? 31 tNaam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku. 32 tIkiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa. 33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
34 tTumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.Mwili wa Ufufuo
35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani? 36 tEwe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa; 37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo; 38 tlakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake. 39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki. 40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. 41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. 42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 thupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 45 tNdivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 tMtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
49 tNa kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.
50 tNdugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 51 tAngalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 tkwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 tMaana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 tBasi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. 55 tKu wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? 56 tUchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 58 tBasi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
1 CORINTHIANS 15
Christ Was Raised to Life
1 My friends, I want you to remember the message I preached and that you believed and trusted.
2 You will be saved by this message, if you hold firmly to it. But if you don't, your faith was all for nothing.
3 t I told you the most important part of the message exactly as it was told to me. This part is:
Christ died for our sins,
as the Scriptures say.
4 t He was buried,
and three days later
he was raised to life,
as the Scriptures say.
5 t Christ appeared to Peter, t
then to the twelve.
6 After this, he appeared
to more than five hundred
other followers.
Most of them are still alive,
but some have died.
7 He also appeared to James,
then to all of the apostles.
8 t Finally, he appeared to me, even though I am like someone who was born at the wrong time.t
9 t I am the least important of all the apostles. In fact, I caused so much trouble for God's church that I don't even deserve to be called an apostle. 10 But God treated me with undeserved grace! He made me what I am, and his grace wasn't wasted. I worked much harder than any of the other apostles, although it was really God's grace at work and not me.
11 But it doesn't matter if I preached or if they preached. All of you believed the message just the same.God's People //Will Be Raised to Life
12 If we preach that Christ was raised from death, how can some of you say the dead will not be raised to life? 13 If they won't be raised to life, Christ himself wasn't raised to life. 14 And if Christ wasn't raised to life, our message is worthless, and so is your faith.
15 If the dead won't be raised to life, we have told lies about God by saying he raised Christ to life, when he really did not.
16 So if the dead won't be raised to life, Christ wasn't raised to life. 17 Unless Christ was raised to life, your faith is useless, and you are still living in your sins. 18 And those people who died after putting their faith in him are completely lost.
19 If our hope in Christ is good only for this life, we are worse off than anyone else.
20 But Christ has been raised to life! And he makes us certain that others will also be raised to life. 21 Just as we will die because of Adam, we will be raised to life because of Christ. 22 Adam brought death to all of us, and Christ will bring life to all of us. 23 But we must each wait our turn. Christ was the first to be raised to life, and his people will be raised to life when he returns.
24 Then after Christ has destroyed all powers and forces, the end will come, and he will give the kingdom to God the Father.
25 t Christ will rule until he puts all his enemies under his power, 26 and the last enemy he destroys will be death. 27 t When the Scriptures say he will put everything under his power, they don't include God. It was God who put everything under the power of Christ.
28 After everything is under the power of God's Son, he will put himself under the power of God, who put everything under his Son's power. Then God will mean everything to everyone.
29 t If the dead are not going to be raised to life, what will people do who are being baptized for them? Why are they being baptized for those dead people? 30 And why do we always risk our lives 31 and face death every day? The pride that I have in you because of Christ Jesus our Lord is what makes me say this.
32 t What do you think I gained by fighting wild animals in Ephesus? If the dead are not raised to life,
“Let's eat and drink.
Tomorrow we die.”
33 Don't fool yourselves. Bad friends will destroy you.
34 Be sensible and stop sinning. You should be embarrassed that some people still don't know about God.What Our Bodies Will Be Like
35 Some of you have asked, “How will the dead be raised to life? What kind of bodies will they have?” 36 Don't be foolish. A seed must die before it can sprout from the ground. 37 Wheat seeds and all other seeds look different from the sprouts that come up. 38 This is because God gives everything the kind of body he wants it to have. 39 People, animals, birds, and fish are each made of flesh, but none of them are alike. 40 Everything in the heavens has a body, and so does everything on earth. But each one is very different from all the others.
41 The sun isn't like the moon, the moon isn't like the stars, and each star is different.
42 That's how it will be when our bodies are raised to life. These bodies will die, but the bodies that are raised will live forever. 43 These ugly and weak bodies will become beautiful and strong.
44 As surely as there are physical bodies, there are spiritual bodies. And our physical bodies will be changed into spiritual bodies.
45 t The first man was named Adam, and the Scriptures tell us that he was a living person. But Jesus, who may be called the last Adam, is a life-giving spirit. 46 We see that the one with a spiritual body did not come first. He came after the one who had a physical body. 47 The first man was made from the dust of the earth, but the second man came from heaven. 48 Everyone on earth has a body like the body of the one who was made from the dust of the earth. And everyone in heaven has a body like the body of the one who came from heaven.
49 Just as we are like the one who was made out of earth, we will be like the one who came from heaven.
50 My friends, I want you to know that our bodies of flesh and blood will decay. This means they cannot share in God's kingdom, which lasts forever. 51 t I will explain a mystery to you. Not every one of us will die, but we will all be changed. 52 It will happen suddenly, quicker than the blink of an eye. At the sound of the last trumpet the dead will be raised. We will all be changed, so we will never die again. 53 Our dead and decaying bodies will be changed into bodies that won't die or decay.
54 t The bodies we now have are weak and can die. But they will be changed into bodies that are eternal. Then the Scriptures will come true,
“Death has lost the battle!
55 t Where is its victory?
Where is its sting?”
56 Sin is what gives death its sting, and the Law is the power behind sin.
57 But thank God for letting our Lord Jesus Christ give us the victory!
58 My dear friends, stand firm and don't be shaken. Always keep busy working for the Lord. You know that everything you do for him is worthwhile.