previous next

1 KOR. 2

Kumtangaza Kristo Aliyesulubiwa

1  tBasi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. 2 tMaana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. 3 tNami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. 4 Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,

5 tili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.

Hekima ya Kweli ya Mungu


6  tWalakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; 7 tbali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; 8 tambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;

9 tlakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)
Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
10  tLakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 12 tLakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 13 tNayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 14 tBasi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 15 tLakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 16 tMaana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

1 CORINTHIANS 2

Telling about Christ //and the Cross

1 Friends, when I came and told you the mysteryt that God had shared with us, I didn't use big words or try to sound wise.

2 In fact, while I was with you, I made up my mind to speak only about Jesus Christ, who had been nailed to a cross.
3  t At first, I was weak and trembling with fear. 4 When I talked with you or preached, I didn't try to prove anything by sounding wise. I simply let God's Spirit show his power.

5 That way you would have faith because of God's power and not because of human wisdom.
6 We do use wisdom when speaking to people who are mature in their faith. But it isn't the wisdom of this world or of its rulers, who will soon disappear. 7 We speak of God's hidden and mysterious wisdom that God decided to use for our glory long before the world began. 8 t The rulers of this world didn't know anything about this wisdom. If they had known about it, they would not have nailed the glorious Lord to a cross.

9 t But it is just as the Scriptures say,
“What God has planned
for people who love him
is more than eyes have seen
or ears have heard.
It has never even
entered our minds!”
10 God's Spirit has shown you everything. His Spirit finds out everything, even what is deep in the mind of God. 11 You are the only one who knows what is in your own mind, and God's Spirit is the only one who knows what is in God's mind.

12 But God has given us his Spirit. This is why we don't think the same way that the people of this world think. This is also why we can recognize the blessings God has given us.
13 Every word we speak was taught to us by God's Spirit, not by human wisdom. And this same Spirit helps us teach spiritual things to spiritual people.t 14 This is why only someone who has God's Spirit can understand spiritual blessings. Anyone who doesn't have God's Spirit thinks these blessings are foolish. 15 People who are guided by the Spirit can make all kinds of judgments, but they cannot be judged by others.

16 t The Scriptures ask,
“Has anyone ever known
the thoughts of the Lord
or given him advice?”
But we understand what Christ is thinking.t