1 KOR. 3
Kuhusu Migawanyiko katika Kanisa la Korintho
1 tLakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. 2 tNaliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, 3 tkwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? 4 tMaana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? 5 tBasi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. 6 tMimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. 7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. 8 Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.
9 tMaana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
10 tKwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. 11 tMaana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 13 tMaana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.
15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.
16 tHamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
18 tMtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. 19 tMaana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao. 20 tNa tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili. 21 Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; 22 kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; 23 nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
1 CORINTHIANS 3
Working Together for God
1 My friends, you are acting like the people of this world. That's why I could not speak to you as spiritual people. You are like babies as far as your faith in Christ is concerned. 2 t So I had to treat you like babies and feed you milk. You could not take solid food, and you still cannot,
3 because you are not yet spiritual. You are jealous and argue with each other. This proves you are not spiritual and you are acting like the people of this world.
4 t Some of you say you follow me, and others claim to follow Apollos. Isn't this how ordinary people behave? 5 Apollos and I are merely servants who helped you to have faith. It was the Lord who made it all happen. 6 t I planted the seeds, Apollos watered them, but God made them sprout and grow. 7 What matters isn't those who planted or watered, but God who made the plants grow. 8 The one who plants is just as important as the one who waters. And each one will be paid for what they do.
9 Apollos and I work together for God, and you are God's garden and God's building.Only One Foundation
10 God treated me with undeserved grace and let me become an expert builder. I laid a foundation on which others have built. But we must each be careful how we build, 11 because Christ is the only foundation. 12-13 Whatever we build on this foundation will be tested by fire on the day of judgment. Then everyone will find out if we have used gold, silver, and precious stones, or wood, hay, and straw. 14 We will be rewarded if our building is left standing.
15 But if it is destroyed by the fire, we will lose everything. Yet we ourselves will be saved, like someone escaping from flames.
16 t All of you surely know you are God's temple and his Spirit lives in you.
17 Together you are God's holy temple, and God will destroy anyone who destroys his temple.
18 Don't fool yourselves! If any of you think you are wise in the things of this world, you will have to become foolish before you can be truly wise. 19 t This is because God considers the wisdom of this world to be foolish. It is just as the Scriptures say, “God catches the wise when they try to outsmart him.” 20 t The Scriptures also say, “The Lord knows that the plans made by wise people are useless.” 21-22 So stop bragging about what anyone has done. Paul and Apollos and Petert all belong to you. In fact, everything is yours, including the world, life, death, the present, and the future. Everything belongs to you, 23 and you belong to Christ, and Christ belongs to God.