previous next

1 KOR. 6

Mashitaka miongoni mwa Waumini

1 Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? 2 tAu hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? 4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa? 5 Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake? 6 Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini. 7 tBasi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu? 8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu. 9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 twala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.

11 tNa baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

Mtukuze Mungu katika Mwili na Roho


12  tVitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. 13 tVyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. 14 tNaye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. 15 tJe! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! 16 tAu hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 tLakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 tAu hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 tmaana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yen

1 CORINTHIANS 6

Taking Each Other to Court

1 When one of you has a complaint against another, do you take your complaint to a court of sinners? Or do you take it to God's people? 2 Don't you know that God's people will judge the world? And if you are going to judge the world, can't you settle small problems? 3 Don't you know we will judge angels? And if this is so, we can surely judge everyday matters. 4 Why do you take everyday complaints to judges who are not respected by the church? 5 I say this to your shame. Aren't any of you wise enough to act as a judge between one follower and another?

6 Why should one of you take another to be tried by unbelievers?
7 When one of you takes another to court, all of you lose. It would be better to let yourselves be cheated and robbed.

8 But instead, you cheat and rob other followers.
9 Don't you know that evil people won't have a share in the blessings of God's kingdom? Don't fool yourselves! No one who is immoral or worships idols or is unfaithful in marriage or is a pervert or behaves like a homosexual 10 will share in God's kingdom. Neither will any thief or greedy person or drunkard or anyone who curses and cheats others.

11 Some of you used to be like that. But now the name of our Lord Jesus Christ and the power of God's Spirit have washed you and made you holy and acceptable to God.

Honor God with Your Body


12  t Some of you say, “We can do anything we want to.” But I tell you not everything is good for us. So I refuse to let anything have power over me. 13 You also say, “Food is meant for our bodies, and our bodies are meant for food.” But I tell you that God will destroy them both. We are not supposed to do indecent things with our bodies. We are to use them for the Lord who is in charge of our bodies.

14 God will raise us from death by the same power he used when he raised our Lord to life.
15 Don't you know that your bodies are part of the body of Christ? Is it right for me to join part of the body of Christ to a prostitute? No, it isn't! 16 t Don't you know that a man who does that becomes part of her body? The Scriptures say, “The two of them will be like one person.”

17 But anyone who is joined to the Lord is one in spirit with him.
18 Don't be immoral in matters of sex. That is a sin against your own body in a way no other sin is. 19 t You surely know that your body is a temple where the Holy Spirit lives. The Spirit is in you and is a gift from God. You are no longer your own. 20 God paid a great price for you. So use your body to honor God.