1 Yohane 5
Tumeushinda ulimwengu
1 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi. 2 Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: Kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake; 3 maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na, amri zake si ngumu, 4 maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu. 5 Nani, basi, awezaye kuushinda ulimwengu? Ni yule anayeamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
Ushahidi juu ya Kristo
6 Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu ya kifo chake. Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Naye Roho anashuhudia kwamba ni kweli, kwani Roho ni ukweli. 7 Basi, wako mashahidi watatu: 8 Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana. 9 Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae. 10 Anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoa Mungu juu ya Mwanae. 11 Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana. 12 Yeyote aliye na Mwana wa Mungu anao uhai huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uhai.
Uhai wa milele
13 Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnao uhai wa milele nyinyi mnaoamini kwa jina la Mwana wa Mungu. 14 Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza. 15 Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba hutupatia yote tunayomwomba.
16 Mtu akimwona ndugu yake ametenda dhambi isiyompeleka kwenye kifo, anapaswa kumwombea kwa Mungu, naye Mungu atampatia uhai. Nasema jambo hili kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi yenye kumpeleka mtu kwenye kifo, nami sisemi kwamba mnapaswa kumwomba Mungu kwa ajili ya hiyo.
17 Kila tendo lisilo adilifu ni dhambi, lakini kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.
18 Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda salama, na yule Mwovu hawezi kumdhuru.
19 Tunajua kwamba sisi ni wake Mungu ingawa ulimwengu wote unatawaliwa na yule Mwovu.
20 Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli – katika muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio uhai wa milele.
21 Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu!
1 John 5
1 Whosoever believeth that Jesus is the Christ is begotten of God: and whosoever loveth him that begat loveth him also that is begotten of him.2 Hereby we know that we love the children of God, when we love God and do his commandments.3 For this is the love of God, that we keep his commandments: and his commandments are not grievous.4 For whatsoever is begotten of God overcometh the world: and this is the victory that hath overcome the world, even our faith.5 And who is he that overcometh the world, but he that believeth that Jesus is the Son of God?6 This is he that came by water and blood, even Jesus Christ; not with the water only, but with the water and with the blood.7 And it is the Spirit that beareth witness, because the Spirit is the truth.8 For there are three who bear witness, the Spirit, and the water, and the blood: and the three agree in one.9 If we receive the witness of men, the witness of God is greater: for the witness of God is this, that he hath borne witness concerning his Son.10 He that believeth on the Son of God hath the witness in him: he that believeth not God hath made him a liar; because he hath not believed in the witness that God hath borne concerning his Son.11 And the witness is this, that God gave unto us eternal life, and this life is in his Son.12 He that hath the Son hath the life; he that hath not the Son of God hath not the life.13 These things have I written unto you, that ye may know that ye have eternal life, even unto you that believe on the name of the Son of God.14 And this is the boldness which we have toward him, that, if we ask anything according to his will, he heareth us:15 and if we know that he heareth us whatsoever we ask, we know that we have the petitions which we have asked of him.16 If any man see his brother sinning a sin not unto death, he shall ask, and God will give him life for them that sin not unto death. There is a sin unto death: not concerning this do I say that he should make request.17 All unrighteousness is sin: and there is a sin not unto death.18 We know that whosoever is begotten of God sinneth not; but he that was begotten of God keepeth himself, and the evil one toucheth him not.19 We know that we are of God, and the whole world lieth in the evil one.20 And we know that the Son of God is come, and hath given us an understanding, that we know him that is true, and we are in him that is true, even in his Son Jesus Christ. This is the true God, and eternal life.21 My little children, guard yourselves from idols.