previous next

1 PET. 4

Mawakili Wema na Neema ya Mungu

1  tBasi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2 tTangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3 tMaana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 5 tNao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.

6 tMaana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
7  tLakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. 8 tZaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 9 tMkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika; 10 tkila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.

11 tMtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

Kuteseka kama Mkristo


12  tWapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13 tLakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14 tMkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 16 tLakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. 17 tKwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? 18 tNa mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? 19 tBasi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.

1 PETER 4

Being Faithful to God

1 Christ suffered here on earth. Now you must be ready to suffer as he did, because suffering shows that you have stopped sinning. 2 It means you have turned from your own desires and want to obey God for the rest of your life. 3 You have already lived long enough like people who don't know God. You were immoral and followed your evil desires. You went around drinking and partying and carrying on. In fact, you even worshiped disgusting idols. 4 Now your former friends wonder why you have stopped running around with them, and they curse you for it. 5 But they will have to answer to God, who judges the living and the dead.

6 The good news has even been preached to the dead, t so that after they have been judged for what they have done in this life, their spirits will live with God.

7 Everything will soon come to an end. So be serious and be sensible enough to pray.

8  t Most important of all, you must sincerely love each other, because love wipes away many sins.

9 Welcome people into your home and don't grumble about it.
10 Each of you has been blessed with one of God's many wonderful gifts to be used in the service of others. So use your gift well.

11 If you have the gift of speaking, preach God's message. If you have the gift of helping others, do it with the strength that God supplies. Everything should be done in a way that will bring honor to God because of Jesus Christ, who is glorious and powerful forever. Amen.

Suffering for Being //a Christian


12 Dear friends, don't be surprised or shocked that you are going through testing that is like walking through fire.

13 Be glad for the chance to suffer as Christ suffered. It will prepare you for even greater happiness when he makes his glorious return.
14 Count it a blessing when you suffer for being a Christian. This shows that God's glorious Spirit is with you. 15 But you deserve to suffer if you are a murderer, a thief, a crook, or a busybody. 16 Don't be ashamed to suffer for being a Christian. Praise God that you belong to him.

17 God has already begun judging his own people. And if his judgment begins with us, imagine how terrible it will be for those who refuse to obey his message. The Scriptures say,

18  t “If good people barely escape,
what will happen to sinners
and to others
who don't respect God?”
19 If you suffer for obeying God, you must have complete faith in your faithful Creator and keep on doing right.