previous next

1 Petro 5

Kundi la Mungu

1 Mimi mzee miongoni mwenu wazee wenzangu, mimi ambaye nilishuhudia mateso ya Kristo na kushiriki ule utukufu utakaofunuliwa, nawasihini 2 mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa; mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote. 3 Msiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali muwe mfano kwa hilo kundi. 4 Na wakati Mchungaji Mkuu atakapotokea, nyinyi mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.

5 Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Nyinyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema wanyenyekevu.” 6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao. 7 Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo. 9 Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo. 10 Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara. 11 Kwake yawe mamlaka milele! Amina.

Salamu za mwisho

12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.

13 Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni. 14 Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo. Nawatakieni amani nyinyi mlio wake Kristo.

1 Peter 5

1 The elders among you I exhort, who am a fellow-elder, and a witness of the sufferings of Christ, who am also a partaker of the glory that shall be revealed:2 Tend the flock of God which is among you, exercising the oversight, not of constraint, but willingly, according to the will of God; nor yet for filthy lucre, but of a ready mind;3 neither as lording it over the charge allotted to you, but making yourselves ensamples to the flock.4 And when the chief Shepherd shall be manifested, ye shall receive the crown of glory that fadeth not away.5 Likewise, ye younger, be subject unto the elder. Yea, all of you gird yourselves with humility, to serve one another: for God resisteth the proud, but giveth grace to the humble.6 Humble yourselves therefore under the mighty hand of God, that he may exalt you in due time;7 casting all your anxiety upon him, because he careth for you.8 Be sober, be watchful: your adversary the devil, as a roaring lion, walketh about, seeking whom he may devour,9 whom withstand stedfast in your faith, knowing that the same sufferings are accomplished in your brethren who are in the world.10 And the God of all grace, who called you unto his eternal glory in Christ, after that ye have suffered a little while, shall himself perfect, establish, strengthen you.11 To him be the dominion for ever and ever. Amen.12 By Silvanus, our faithful brother, as I account him, I have written unto you briefly, exhorting, and testifying that this is the true grace of God. Stand ye fast therein.13 She that is in Babylon, elect together with you, saluteth you; and so doth Mark my son.14 Salute one another with a kiss of love. Peace be unto you all that are in Christ.