1 Wathesalonike 4
Maisha yampendezayo Mungu
1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi. 2 Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu. 3 Mungu anataka nyinyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa. 4 Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima, 5 na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu. 6 Basi, mtu yeyote asimkosee au kumpunja mwenzake kuhusu jambo hili. Tulikwisha waambieni hayo na kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibu wanaofanya mambo hayo. 7 Mungu hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika utakatifu. 8 Kwa hiyo basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali anamdharau Mungu mwenyewe anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
9 Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Nyinyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana. 10 Na mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi, ndugu, tunawaombeni mfanye hata zaidi. 11 Muwe na nia ya kuishi maisha ya utulivu, kila mmoja ashughulikie mambo yake mwenyewe na afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe kama tulivyowaagiza pale awali. 12 Kwa namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
Bwana anakuja
13 Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. 14 Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
15 Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia. 16 Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana. 18 Basi, farijianeni kwa maneno haya.
1 Thessalonians 4
1 Finally then, brethren, we beseech and exhort you in the Lord Jesus, that, as ye received of us how ye ought to walk and to please God, even as ye do walk, --that ye abound more and more.2 For ye know what charge we gave you through the Lord Jesus.3 For this is the will of God, even your sanctification, that ye abstain from fornication;4 that each one of you know how to possess himself of his own vessel in sanctification and honor,5 not in the passion of lust, even as the Gentiles who know not God;6 that no man transgress, and wrong his brother in the matter: because the Lord is an avenger in all these things, as also we forewarned you and testified.7 For God called us not for uncleanness, but in sanctification.8 Therefore he that rejecteth, rejecteth not man, but God, who giveth his Holy Spirit unto you.9 But concerning love of the brethren ye have no need that one write unto you: for ye yourselves are taught of God to love one another;10 for indeed ye do it toward all the brethren that are in all Macedonia. But we exhort you, brethren, that ye abound more and more;11 and that ye study to be quiet, and to do your own business, and to work with your hands, even as we charged you;12 that ye may walk becomingly toward them that are without, and may have need of nothing.13 But we would not have you ignorant, brethren, concerning them that fall asleep; that ye sorrow not, even as the rest, who have no hope.14 For if we believe that Jesus died and rose again, even so them also that are fallen asleep in Jesus will God bring with him.15 For this we say unto you by the word of the Lord, that we that are alive, that are left unto the coming of the Lord, shall in no wise precede them that are fallen asleep.16 For the Lord himself shall descend from heaven, with a shout, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first;17 then we that are alive, that are left, shall together with them be caught up in the clouds, to meet the Lord in the air: and so shall we ever be with the Lord.18 Wherefore comfort one another with these words.