1 Wathesalonike 5
Muwe tayari kwa siku ya Bwana
1 Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira ya mambo haya yatakapotukia. 2 Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. 3 Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. 4 Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. 5 Nyinyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza. 6 Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi. 7 Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku. 8 Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. 9 Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo 10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. 11 Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa.
Maagizo ya mwisho na salamu
12 Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo. 13 Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu.
14 Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote. 15 Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
16 Furahini daima, 17 salini kila wakati 18 na kuwa na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
19 Msimpinge Roho Mtakatifu; 20 msidharau unabii. 21 Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema, 22 na kuepuka kila aina ya uovu.
23 Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu – roho, mioyo na miili yenu – mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye anayewaita nyinyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.
25 Ndugu, tuombeeni na sisi pia.
26 Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.
27 Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua hii.
28 Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Thessalonians 5
1 But concerning the times and the seasons, brethren, ye have no need that aught be written unto you.2 For yourselves know perfectly that the day of the Lord so cometh as a thief in the night.3 When they are saying, Peace and safety, then sudden destruction cometh upon them, as travail upon a woman with child; and they shall in no wise escape.4 But ye, brethren, are not in darkness, that that day should overtake you as a thief:5 for ye are all sons of light, and sons of the day: we are not of the night, nor of darkness;6 so then let us not sleep, as do the rest, but let us watch and be sober.7 For they that sleep sleep in the night: and they that are drunken are drunken in the night.8 But let us, since we are of the day, be sober, putting on the breastplate of faith and love; and for a helmet, the hope of salvation.9 For God appointed us not into wrath, but unto the obtaining of salvation through our Lord Jesus Christ,10 who died for us, that, whether we wake or sleep, we should live together with him.11 Wherefore exhort one another, and build each other up, even as also ye do.12 But we beseech you, brethren, to know them that labor among you, and are over you in the Lord, and admonish you;13 and to esteem them exceeding highly in love for their work’s sake. Be at peace among yourselves.14 And we exhort you, brethren, admonish the disorderly, encourage the fainthearted, support the weak, be longsuffering toward all.15 See that none render unto any one evil for evil; but always follow after that which is good, one toward another, and toward all.16 Rejoice always;17 pray without ceasing;18 in everything give thanks: for this is the will of God in Christ Jesus to you-ward.19 Quench not the Spirit;20 despise not prophesyings;21 prove all things; hold fast that which is good;22 abstain from every form of evil.23 And the God of peace himself sanctify you wholly; and may your spirit and soul and body be preserved entire, without blame at the coming of our Lord Jesus Christ.24 Faithful is he that calleth you, who will also do it.25 Brethren, pray for us.26 Salute all the brethren with a holy kiss.27 I adjure you by the Lord that this epistle be read unto all the brethren.28 The grace of our Lord Jesus Christ be with you.