previous next

2 KOR. 10

Paulo Atetea Huduma yake

1  tBasi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu; 2 tnaam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili. 3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4 t(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 6 ttena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia. 7 Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi. 8 tMaana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika; 9 nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. 10 Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu.

11 tMtu kama huyo na afikiri hivi, ya kwamba jinsi tulivyo kwa maneno katika nyaraka tusipokuwapo, ndivyo tulivyo kwa matendo tukiwapo.
12  tKwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili. 13 tLakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu. 14 Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo; 15 twala hatujisifu zaidi ya kadiri yetu, yaani, katika taabu za watu wengine; bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri ya kipimo chetu, na kupata ziada; 16 thata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu; tusijisifu katika kipimo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa. 17 tLakini, Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana. 18 tMaana mtu mwenye kukubaliwa si yeye ajisifuye, bali yeye asifiwaye na Bwana.

2 CORINTHIANS 10

Paul Defends His Work //for Christ

1 Do you think I am a coward when I am with you and brave when I am far away? Well, I ask you to listen, because Christ himself was humble and gentle. 2 Some people have said we act like the people of this world. So when I arrive, I expect I will have to be firm and forceful in what I say to them. Please don't make me treat you that way. 3 We live in this world, but we don't act like its people 4 or fight our battles with the weapons of this world. Instead, we use God's power that can destroy fortresses. We destroy arguments 5 and every bit of pride that keeps anyone from knowing God. We capture people's thoughts and make them obey Christ.

6 And when you completely obey him, we will punish anyone who refuses to obey.
7 You judge by appearances.t If any of you think you are the only ones who belong to Christ, then think again. We belong to Christ as much as you do. 8 Maybe I brag a little too much about the authority that the Lord gave me to help you and not to hurt you. Yet I am not embarrassed to brag. 9 And I am not trying to scare you with my letters. 10 Some of you are saying, “Paul's letters are harsh and powerful. But in person, he is a weakling and has nothing worth saying.”

11 Those people had better understand that when I am with you, I will do exactly what I say in my letters.
12 We won't dare compare ourselves with those who think so much of themselves. But they are foolish to compare themselves with themselves. 13 We won't brag about something we don't have a right to brag about. We will only brag about the work God has sent us to do, and you are part of that work.

14 We are not bragging more than we should. After all, we did bring the message about Christ to you.
15 We don't brag about what others have done, as if we had done those things ourselves. But I hope as you become stronger in your faith, we will be able to reach many more of the people around you.t That has always been our goal. 16 Then we will be able to preach the good news in other lands where we cannot take credit for work someone else has already done. 17 t The Scriptures say, “If you want to brag, then brag about the Lord.” 18 You may brag about yourself, but the only approval that counts is the Lord's approval.