2 Timotheo 3
Siku ya mwisho
1 Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. 2 Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu; 3 watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema; 4 watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. 5 Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo. 6 Baadhi yao huenda katika nyumba za watu na huwateka wanawake dhaifu waliolemewa mizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa na tamaa za kila aina; 7 wanawake ambao wanajaribu daima kujifunza lakini hawawezi kuufikia ujuzi wa huo ukweli. 8 Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose. Hao ni watu wa akili potovu na imani ya uongo. 9 Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
Maagizo ya Mwisho
10 Wewe, lakini, umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu, subira yangu, 11 udhalimu na mateso. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote. 12 Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kumcha Mungu katika kuungana na Kristo Yesu lazima adhulumiwe. 13 Watu waovu na wadanganyifu wataendelea kuwa wabaya, wakidanganya wengine, na wao wenyewe wakidanganywa. 14 Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa ukaukubali kabisa. Wawajua wale waliokuwa waalimu wako, 15 wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu. 16 Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili, 17 ili mtu wa Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila kazi njema.
2 Timothy 3
1 But know this, that in the last days grievous times shall come.2 For men shall be lovers of self, lovers of money, boastful, haughty, railers, disobedient to parents, unthankful, unholy,3 without natural affection, implacable, slanderers, without self-control, fierce, no lovers of good,4 traitors, headstrong, puffed up, lovers of pleasure rather than lovers of God;5 holding a form of godliness, but having denied the power therefore. From these also turn away.6 For of these are they that creep into houses, and take captive silly women laden with sins, led away by divers lusts,7 ever learning, and never able to come to the knowledge of the truth.8 And even as Jannes and Jambres withstood Moses, so do these also withstand the truth. Men corrupted in mind, reprobate concerning the faith.9 But they shall proceed no further. For their folly shall be evident unto all men, as theirs also came to be.10 But thou didst follow my teaching, conduct, purpose, faith, longsuffering, love, patience,11 persecutions, sufferings. What things befell me at Antioch, at Iconium, at Lystra; what persecutions I endured. And out of them all the Lord delivered me.12 Yea, and all that would live godly in Christ Jesus shall suffer persecution.13 But evil men and impostors shall wax worse and worse, deceiving and being deceived.14 But abide thou in the things which thou hast learned and hast been assured of, knowing of whom thou hast learned them.15 And that from a babe thou hast known the sacred writings which are able to make thee wise unto salvation through faith which is in Christ Jesus.16 Every scripture inspired of God is also profitable for teaching, for reproof, for correction, for instruction which is in righteousness.17 That the man of God may be complete, furnished completely unto every good work.