previous next

3 YOH. 1

Salamu

1  tMzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.

Gayo Apongezwa kwa Ukarimu wake


2  tMpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.

4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.
5 Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao, 6 twaliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu. 7 tKwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.

8 tBasi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.

Diotrefe na Demetrio


9 Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.

10 Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

Salamu za Mwisho


11  tMpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

12 tDemetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia twashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.
13  tNalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. 14 Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema uso kwa uso. 15 Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

3 JOHN 1

1  t From the church leader.t
To my dear friend Gaius.
I love you because we follow the truth,
2 dear friend, and I pray all goes well for you. I hope you are as strong in body, as I know you are in spirit. 3 It makes me very happy when the Lord's followers come by and speak openly of how you obey the truth.

4 Nothing brings me greater happiness than to hear that my childrent are obeying the truth.

Working Together


5 Dear friend, you have always been faithful in helping other followers of the Lord, even the ones you didn't know before. 6 They have told the church about your love. They say you were good enough to welcome them and to send them on their mission in a way God's servants deserve. 7 When they left to tell others about the Lord, they decided not to accept help from anyone who wasn't a follower.

8 We must support people like them, so we can take part in what they are doing to spread the truth.
9 I wrote to the church. But Diotrephes likes to be the number-one leader, and he won't pay any attention to us.

10 So if I come, I will remind him of how he has been attacking us with gossip. Not only has he been doing this, but he refuses to welcome any of the Lord's followers who come by. And when other church members want to welcome them, he puts them out of the church.

11 Dear friend, don't imitate the evil deeds of others, but follow the example of people who do kind deeds. They are God's children, but those who are always doing evil have never seen God.

12 Everyone speaks well of Demetrius, and so does the true message that he teaches. I also speak well of him, and you know what I say is true.

Final Greetings


13 I have much more to say to you, but I don't want to write it with pen and ink.

14 I hope to see you soon, and then we can talk in person.

15 I pray that God will bless you with peace!
Your friends send their greetings. Please give a personal greeting to each of our friends.