previous next

MDO 1

Ahadi ya Roho Mtakatifu

1  tKitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha, 2 thata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; 3 wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu. 4 tHata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;

5 tya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.

Kupaa kwa Yesu


6  tBasi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? 7 tAkawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 8 tLakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 9 tAkiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 tWalipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,

11 twakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Mathiya Ateuliwa Kuchukua mahali pa Yuda


12  tKisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato. 13 tHata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo.

14 tHawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
15 Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilipata mia na ishirini), akasema, 16 tNdugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu; 17 kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii. 18 t(Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka. 19 Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.)

20 tKwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi,
Kikao chake na kiwe ukiwa,
Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo;
tena,
Usimamizi wake autwae mwingine.
21  tBasi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, 22 tkuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi. 23 Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. 24 tKisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, 25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26 tWakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

ACTS 1

1  t Theophilus, I first wrote to yout about all that Jesus did and taught from the very first

2 until he was taken up to heaven. But before he was taken up, he gave orders to the apostles he had chosen with the help of the Holy Spirit.
3 For 40 days after Jesus had suffered and died, he proved in many ways that he had been raised from death. He appeared to his apostles and spoke to them about God's kingdom.

4 t While he was still with them, he said:
Don't leave Jerusalem yet. Wait here for the Father to give you the Holy Spirit, just as I told you he has promised to do.

5 t John baptized with water, but in a few days you will be baptized with the Holy Spirit.

Jesus Is Taken to Heaven


6 While the apostles were still with Jesus, they asked him, “Lord, are you now going to give Israel its own king again?”t
7 Jesus said to them, “You don't need to know the time of those events that only the Father controls. 8 t But the Holy Spirit will come upon you and give you power. Then you will tell everyone about me in Jerusalem, in all Judea, in Samaria, and everywhere in the world.” 9 t After Jesus had said this and while they were watching, he was taken up into a cloud. They could not see him,

10 but as he went up, they kept looking up into the sky.
Suddenly two men dressed in white clothes were standing there beside them.

11 They said, “Why are you men from Galilee standing here and looking up into the sky? Jesus has been taken to heaven. But he will come back in the same way you have seen him go.”

Someone To Take the Place //of Judas


12-13  t The Mount of Olives was about a kilometer from Jerusalem. The apostles who had gone there were Peter, John, James, Andrew, Philip, Thomas, Bartholomew, Matthew, James the son of Alphaeus, Simon, known as the Eager One, t and Judas the son of James.
After the apostles returned to the city, they went upstairs to the room where they had been staying.
14 The apostles often met together and prayed with a single purpose in mind.t The women and Mary the mother of Jesus would meet with them, and so would his brothers. 15 One day there were about 120 of the Lord's followers meeting together, and Peter stood up to speak to them.

16-17 He said:
My friends, long ago by the power of the Holy Spirit, David said something about Judas, and what he said has now happened. Judas was one of us and had worked with us, but he brought the mob to arrest Jesus.
18 t Then Judas bought some land with the money he was given for doing that evil thing. He fell headfirst into the field. His body burst open, and all his insides came out.

19 When the people of Jerusalem found out about this, they called the place Akeldama, which in the local language means “Field of Blood.”

20  t In the book of Psalms it says,
“Leave his house empty,
and don't let anyone
live there.”
It also says,
“Let someone else
have his job.”

21-22  t So we need someone else to help us tell others that Jesus has been raised from death. He must also be one of the men who was with us from the very beginning. He must have been with us from the time the Lord Jesus was baptized by John until the day he was taken to heaven.
23 Two men were suggested: One of them was Joseph Barsabbas, known as Justus, and the other was Matthias. 24 Then they all prayed, “Lord, you know what everyone is like! Show us the one you have chosen 25 to be an apostle and to serve in place of Judas, who got what he deserved.” 26 They drew names, and Matthias was chosen to join the group of the eleven apostles.