MDO 18
Paulo katika Korintho
1 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. 2 tAkamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao; 3 tna kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.
4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.
5 tHata Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. 6 tWalipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa. 7 Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Tito Yusto, mcha Mungu, ambaye nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sinagogi. 8 tNa Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa. 9 tBwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, 10 tkwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.
11 Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu.
12 Hata Galio alipokuwa liwali wa Akaya, Wayahudi wakamwinukia Paulo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu, 13 wakisema Mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria. 14 tNa Paulo alipotaka kufunua kinywa chake, Galio akawaambia Wayahudi, Kama lingekuwa jambo la dhuluma au la hila mbaya, enyi Wayahudi, ingekuwa haki mimi kuchukuliana nanyi; 15 tbali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sheria yenu, liangalieni ninyi wenyewe, maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo. 16 Akawafukuza waondoke mbele ya kiti cha hukumu.
17 tNao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.Paulo Arudi Antiokia
18 tBaada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. 19 Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi. 20 Walipomtaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali; 21 tbali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso, 22 tna alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu kanisa, kisha akatelemkia Antiokia.
23 Hata akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwathibitisha wanafunzi.Huduma ya Apolo
24 tBasi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. 25 tMtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. 26 Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. 27 tNa alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. 28 tKwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.
ACTS 18
Paul in Corinth
1 Paul left Athens and went to Corinth, 2 where he met Aquila, a Jewish man from Pontus. Not long before this, Aquila had come from Italy with his wife Priscilla, because Emperor Claudius had ordered the Jewish people to leave Rome.t Paul went to see Aquila and Priscilla
3 and found out they were tent makers. Paul was also a tent maker, so he stayed with them, and they worked together.
4 Every Sabbath, Paul went to the synagogue. He spoke to Jews and Gentilest and tried to win them over. 5 But after Silas and Timothy came from Macedonia, he spent all his time preaching to the Jews about Jesus the Messiah.
6 Finally, they turned against him and insulted him. So he shook the dust from his clothest and told them, “Whatever happens to you will be your own fault! I am not to blame. From now on I am going to preach to the Gentiles.”
7 Paul then moved into the house of a man named Titius Justus, who worshiped God and lived next door to the synagogue.
8 Crispus was the leader of the synagogue. He and everyone in his family put their faith in the Lord. Many others in Corinth also heard the message, and all the people who had faith in the Lord were baptized.
9 One night, Paul had a vision, and in it the Lord said, “Don't be afraid to keep on preaching. Don't stop! 10 I am with you, and you won't be harmed. Many people in this city belong to me.”
11 Paul stayed on in Corinth for a year and a half, teaching God's message to the people.
12 While Gallio was governor of Achaia, some of the Jewish leaders got together and grabbed Paul. They brought him into court
13 and said, “This man is trying to make our people worship God in a way that is against our Law!”
14 Even before Paul could speak, Gallio said, “If you were charging this man with a crime or some other wrong, I would have to listen to you. 15 But since this concerns only words, names, and your own law, you will have to take care of it yourselves. I refuse to judge such matters.” 16 Then he sent them out of the court.
17 The crowd grabbed Sosthenes, the Jewish leader, and beat him up in front of the court. But none of this mattered to Gallio.Paul Returns to //Antioch in Syria
18 t After Paul had stayed for a while with the Lord's followers in Corinth, he told them goodbye and sailed on to Syria with Aquila and Priscilla. But before he left, he had his head shavedt at Cenchreae because he had made a promise to God.
19 The three of them arrived in Ephesus, where Paul left Priscilla and Aquila. He then went into the synagogue to talk with the people there. 20 They asked him to stay longer, but he refused.
21 He told them goodbye and said, “If God lets me, I will come back.”
22 Paul sailed to Caesarea, where he greeted the church. Then he went on to Antioch.
23 After staying there for a while, he left and visited several places in Galatia and Phrygia. He helped the followers there to become stronger in their faith.Apollos in Ephesus
24 A Jewish man named Apollos came to Ephesus. Apollos had been born in the city of Alexandria. He was a very good speaker and knew a lot about the Scriptures.
25 He also knew much about the Lord's Way, t and he spoke about it with great excitement. What he taught about Jesus was right, but all he knew was John's message about baptism.
26 Apollos started speaking bravely in the synagogue. But when Priscilla and Aquila heard him, they took him to their home and helped him understand God's Way even better.
27 Apollos decided to travel through Achaia. So the Lord's followers wrote letters, encouraging the followers there to welcome him. After Apollos arrived in Achaia, he was a great help to everyone who had put their faith in the Lord Jesus because of God's gift of undeserved grace. 28 He got into fierce arguments with the Jewish people, and in public he used the Scriptures to prove that Jesus is the Messiah.