MDO 21
Safari ya Paulo kwenda Yerusalemu
1 Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na kuabiri, tukafika Kosi kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara, 2 tukapata merikebu itakayovuka mpaka Foinike tukapanda tukatweka. 3 Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake. 4 tTukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paulo kwa uweza wa Roho asipande kwenda Yerusalemu. 5 tHata tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote, pamoja na wake zao na watoto wao, wakatusindikiza mpake nje ya mji, tukapiga magoti pwani tukaomba;
6 na baada ya kuagana tukapanda merikebuni, nao wakarudi kwao.
7 Hata tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai, tukawaamkua ndugu tukakaa kwao siku moja.
8 tAsubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.
9 tMtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri. 10 tBasi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. 11 tAlipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa. 12 tBasi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu. 13 tNdipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.
14 tAlipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke.
15 Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemu.
16 Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakamchukua na Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani ambaye ndiye tutakayekaa kwake.Paulo Amtembelea Yakobo Yerusalemu
17 Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha. 18 tHata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako. 19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake. 20 tNao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati. 21 tNao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi. 22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja. 23 tBasi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri. 24 tWachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati. 25 tLakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.
26 tNdipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao.Paulo Ashikwa akiwa Hekaluni
27 Basi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimia, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata, 28 twakapiga kelele, na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu. 29 tKwa maana walikuwa wamemwona Trofimo, Mwefeso, pamoja naye mjini, ambaye walidhania ya kuwa Paulo amemwingiza katika hekalu. 30 Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni; mara milango ikafungwa. 31 Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, habari zikamfikilia jemadari wa kikosi ya kwamba Yerusalemu imechafuka, mji mzima. 32 Mara akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo. 33 tKisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili; akauliza, Nani huyu? Tena, amefanya nini? 34 Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome. 35 Basi Paulo alipofika darajani ilikuwa kuchukuliwa na askari kwa sababu ya nguvu ya makutano.
36 tMaana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, na kusema, Mwondoe huyu.Paulo Ajitetea
37 Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kiyunani? 38 tWewe si yule Mmisri ambaye kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani? 39 tPaulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa. 40 Basi, alipompa ruhusa, Paulo akasimama madarajani, akawapungia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania, akisema,
ACTS 21
Paul Goes to Jerusalem
1 After saying goodbye, we sailed straight to Cos. The next day we reached Rhodes and from there sailed on to Patara.
2 We found a ship going to Phoenicia, so we got on board and sailed off.
3 We came within sight of Cyprus and then sailed south of it on to the port of Tyre in Syria, where the ship was going to unload its cargo. 4 We found the Lord's followers and stayed with them for a week. The Holy Spirit had told them to warn Paul not to go on to Jerusalem. 5 But when the week was over, we started on our way again. All the men, together with their wives and children, walked with us from the town to the seashore. We knelt on the beach and prayed.
6 Then after saying goodbye to each other, we got into the ship, and they went back home.
7 We sailed from Tyre to Ptolemais, where we greeted the followers and stayed with them for a day. 8 t The next day we went to Caesarea and stayed with Philip, the preacher. He was one of the seven men who helped the apostles,
9 and he had four unmarriedt daughters who prophesied.
10 t We had been in Caesarea for several days, when the prophet Agabus came to us from Judea. 11 He took Paul's belt, and with it he tied up his own hands and feet. Then he told us, “The Holy Spirit says that some of the Jewish leaders in Jerusalem will tie up the man who owns this belt. They will also hand him over to the Gentiles.”
12 After Agabus said this, we and the followers living there begged Paul not to go to Jerusalem.
13 But Paul answered, “Why are you crying and breaking my heart? I am not only willing to be put in jail for the Lord Jesus, but I am even willing to die for him in Jerusalem!”
14 Since we could not get Paul to change his mind, we gave up and prayed, “Lord, please make us willing to do what you want.”
15 Then we got ready to go to Jerusalem.
16 Some of the followers from Caesarea went with us and took us to stay in the home of Mnason. He was from Cyprus and had been a follower from the beginning.Paul Visits James
17 When we arrived in Jerusalem, the Lord's followers gladly welcomed us. 18 Paul went with us to see Jamest the next day, and all the church leaders were present. 19 Paul greeted them and told how God had used him to help the Gentiles.
20 Everyone who heard this praised God and said to Paul:
My friend, you can see how many tens of thousands of our people have become followers! And all of them are eager to obey the Law of Moses.
21 But they have been told that you are teaching those who live among the Gentiles to disobey this Law. They claim that you are telling them not to circumcise their sons or to follow our customs.
22 What should we do now that our people have heard you are here? 23 t Please do what we ask, because four of our men have made special promises to God.
24 Join with them and prepare yourself for the ceremony that goes with the promises. Pay the cost for their heads to be shaved. Then everyone will learn that the reports about you are not true. They will know you do obey the Law of Moses.
25 t Some while ago we told the Gentile followers what we think they should do. We instructed them not to eat anything offered to idols. They were told not to eat any meat with blood still in it or the meat of an animal that has been strangled. They were also told not to commit any terrible sexual sins.t
26 The next day Paul took the four men with him and got himself ready at the same time they did. Then he went into the temple and told when the final ceremony would take place and when an offering would be made for each of them.Paul Is Arrested
27 When the period of seven days for the ceremony was almost over, some of the Jewish people from Asia saw Paul in the temple. They got a large crowd together and started attacking him. 28 They were shouting, “Friends, help us! This man goes around everywhere, saying bad things about our nation and about the Law of Moses and about this temple. He has even brought shame to this holy temple by bringing in Gentiles.”
29 t Some of them thought that Paul had brought Trophimus from Ephesus into the temple, because they had seen them together in the city.
30 The whole city was in an uproar, and the people turned into a mob. They grabbed Paul and dragged him out of the temple. Then suddenly the doors were shut. 31 The people were about to kill Paul when the Roman army commander heard that all Jerusalem was starting to riot.
32 So he quickly took some soldiers and officers and ran to where the crowd had gathered.
As soon as the mob saw the commander and soldiers, they stopped beating Paul. 33 The army commander went over and arrested him and had him bound with two chains. Then he tried to find out who Paul was and what he had done. 34 Part of the crowd shouted one thing, and part of them shouted something else. But they were making so much noise that the commander could not find out a thing. Then he ordered Paul to be taken into the fortress. 35 As they reached the steps, the crowd became so wild that the soldiers had to lift Paul up and carry him.
36 The crowd followed and kept shouting, “Kill him! Kill him!”Paul Speaks to the Crowd
37 When Paul was about to be taken into the fortress, he asked the commander, “Can I say something to you?”
“How do you know Greek?” the commander asked.
38 “Aren't you that Egyptian who started a riot not long ago and led 4,000 terrorists into the desert?”
39 “No!” Paul replied. “I am a Jew from Tarsus, an important city in Cilicia. Please let me speak to the crowd.”
40 The commander told him he could speak, so Paul stood on the steps and motioned to the people. When they were quiet, he spoke to them in Aramaic:t