previous next

Wakolosai 3

1  t Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu. 2 Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani. 3 Maana nyinyi mmekufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Uhai wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.

Maisha ya kale na maisha mapya

5 Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia: Uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu). 6 Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi. 7 Wakati mmoja nyinyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo, mlipotawaliwa nayo. 8 Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: Hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu. 9 Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, 10 mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu. 11 Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote.

12 Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi. 14 Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili. 15 Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani! 16 Ujumbe wa Kristo na ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani. 17 Na, kila mfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyote kwa jina la Bwana Yesu na kumshukuru Mungu Baba kwa njia yake.

Wajibu wa jamii katika maisha mapya

18 Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. 19 Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.

20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.

21 Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.

22 Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana. 23 Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. 24 Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana! 25 Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.

Colossians 3

1 If then ye were raised together with Christ, seek the things that are above, where Christ is, seated on the right hand of God.2 Set your mind on the things that are above, not on the things that are upon the earth.3 For ye died, and your life is hid with Christ in God.4 When Christ, who is our life, shall be manifested, then shall ye also with him be manifested in glory.5 Put to death therefore your members which are upon the earth: fornication, uncleanness, passion, evil desire, and covetousness, which is idolatry;6 for which things’ sake cometh the wrath of God upon the sons of disobedience:7 wherein ye also once walked, when ye lived in these things;8 but now do ye also put them all away: anger, wrath, malice, railing, shameful speaking out of your mouth:9 lie not one to another; seeing that ye have put off the old man with his doings,10 and have put on the new man, that is being renewed unto knowledge after the image of him that created him:11 where there cannot be Greek and Jew, circumcision and uncircumcision, barbarian, Scythian, bondman, freeman; but Christ is all, and in all.12 Put on therefore, as God’s elect, holy and beloved, a heart of compassion, kindness, lowliness, meekness, longsuffering;13 forbearing one another, and forgiving each other, if any man have a complaint against any; even as the Lord forgave you, so also do ye:14 and above all these things put on love, which is the bond of perfectness.15 And let the peace of Christ rule in your hearts, to the which also ye were called in one body; and be ye thankful.16 Let the word of Christ dwell in you richly; in all wisdom teaching and admonishing one another with psalms and hymns and spiritual songs, singing with grace in your hearts unto God.17 And whatsoever ye do, in word or in deed, do all in the name of the Lord Jesus, giving thanks to God the Father through him.18 Wives, be in subjection to your husbands, as is fitting in the Lord.19 Husbands, love your wives, and be not bitter against them.20 Children, obey your parents in all things, for this is well-pleasing in the Lord.21 Fathers, provoke not your children, that they be not discouraged.22 Servants, obey in all things them that are your masters according to the flesh; not with eye-service, as men-pleasers, but in singleness of heart, fearing the Lord:23 whatsoever ye do, work heartily, as unto the Lord, and not unto men;24 knowing that from the Lord ye shall receive the recompense of the inheritance: ye serve the Lord Christ.25 For he that doeth wrong shall receive again for the wrong that he hath done: and there is no respect of persons.