EFE. 1
Salamu
1 tPaulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.
2 tNeema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.Baraka za Kiroho katika Kristo
3 tAtukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 4 tkama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 tKwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 6 tNa usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. 7 tKatika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. 8 tNaye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi; 9 takiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. 10 tYaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo; 11 tna ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. 12 Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu. 13 tNanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
14 tNdiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.Sala ya Paulo
15 tKwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, 16 tsiachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, 17 tMungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; 18 tmacho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; 19 tna ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; 20 taliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 tjuu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 takavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 tndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
EPHESIANS 1
1 t From Paul, chosen by God to be an apostle of Christ Jesus.
To God's people who live in Ephesus andt are faithful followers of Christ Jesus.
2 I pray that God our Father and our Lord Jesus Christ will be kind to you and will bless you with peace!Christ Brings Spiritual //Blessings
3 Praise the God and Father of our Lord Jesus Christ for the spiritual blessings that Christ has brought us from heaven! 4 Before the world was created, God had Christ choose us to live with him and to be his holy and innocent and loving people. 5 God was kindt and decided that Christ would choose us to be God's own adopted children.
6 God treated us with undeserved grace because of the Son he dearly loves, and so we should praise God.
7-8 t Christ sacrificed his life's blood to set us free, which means our sins are now forgiven. Christ did this because of God's gift of undeserved grace to us. God has great wisdom and understanding, 9 and by what Christ has done, God has shown us his own mysterious ways.
10 Then when the time is right, God will do all he has planned, and Christ will bring together everything in heaven and on earth.
11 God always does what he plans, and this is why he appointed Christ to choose us. 12 He did this so we Jews would bring honor to him and be the first ones to have hope because of him. 13 Christ also brought you the truth, which is the good news about how you can be saved. You put your faith in Christ and were given the promised Holy Spirit to show you belong to God.
14 The Spirit also makes us sure we will be given what God has stored up for his people. Then we will be set free, and God will be honored and praised.Paul's Prayer
15 I have heard about your faith in the Lord Jesus and your love for all God's people. 16 So I never stop being grateful for you, as I mention you in my prayers. 17 I ask the glorious Father and God of our Lord Jesus Christ to give you his Spirit. The Spirit will make you wise and let you understand what it means to know God.
18 My prayer is that light will flood your hearts and you will understand the hope given to you when God chose you. Then you will discover the glorious blessings that will be yours together with all God's people.
19 I want you to know about the great and mighty power that God has for us followers. It is the same wonderful power he used 20 t when he raised Christ from death and let him sit at his right sidet in heaven. 21 There Christ rules over all forces, authorities, powers, and rulers. He rules over all beings in this world and will rule in the future world as well. 22 t t God has put all things under the power of Christ, and for the good of the church he has made him the head of everything. 23 The church is the body of Christ and is filled with Christ who completely fills everything.t