GAL. 5
1 tKatika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.Asili ya Uhuru wa Mkristo
2 tTazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. 3 Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. 4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. 5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.
6 tMaana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
7 Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8 tKushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. 9 tChachu kidogo huchachua donge zima. 10 tNina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote. 11 tNami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!
12 tLaiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!
13 tMaana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. 14 tMaana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
15 Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.Kazi za Kimwili
16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 tKwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 tLakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. 19 tBasi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 thusuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.Tunda la Roho
22 tLakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 tupole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24 tNa hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 25 tTukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. 26 tTusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
GALATIANS 5
Christ Gives Freedom
1 Christ has set us free! This means we are really free. Now hold on to your freedom and don't ever become slaves of the Law again.
2 I, Paul, promise you that Christ won't do you any good if you get circumcised. 3 If you do, you must obey the whole Law. 4 And if you try to please God by obeying the Law, you have cut yourself off from Christ and his gift of undeserved grace. 5 But the Spirit makes us sure God will accept us because of our faith in Christ.
6 If you are a follower of Christ Jesus, it makes no difference whether you are circumcised or not. All that matters is your faith that makes you love others.
7 You were doing so well until someone made you turn from the truth. 8 And that person was certainly not sent by the one who chose you. 9 t A little yeast can change a whole batch of dough,
10 but you belong to the Lord. This makes me certain you will do what I say, instead of what someone else tells you to do. Whoever is causing trouble for you will be punished.
11 My friends, if I still preach that people need to be circumcised, why am I in so much trouble? The message about the cross would no longer be a problem, if I told people to be circumcised.
12 I wish everyone who is upsetting you would not only get circumcised, but would cut off much more!
13 My friends, you were chosen to be free. So don't use your freedom as an excuse to do anything you want. Use it as an opportunity to serve each other with love. 14 t All the Law says can be summed up in the command to love others as much as you love yourself.
15 But if you keep attacking each other like wild animals, you had better watch out or you will destroy yourselves.God's Spirit //and Our Own Desires
16 If you are guided by the Spirit, you won't obey your selfish desires. 17 t The Spirit and your desires are enemies of each other. They are always fighting each other and keeping you from doing what you feel you should.
18 But if you obey the Spirit, the Law of Moses has no control over you.
19 People's desires make them give in to immoral ways, filthy thoughts, and shameful deeds. 20 They worship idols, practice witchcraft, hate others, and are hard to get along with. People become jealous, angry, and selfish. They not only argue and cause trouble, but they are
21 envious. They get drunk, carry on at wild parties, and do other evil things as well. I told you before, and I am telling you again: No one who does these things will share in the blessings of God's kingdom.
22 God's Spirit makes us loving, happy, peaceful, patient, kind, good, faithful, 23 gentle, and self-controlled. There is no law against behaving in any of these ways. 24 And because we belong to Christ Jesus, we have killed our selfish feelings and desires. 25 God's Spirit has given us life, and so we should follow the Spirit. 26 But don't be conceited or make others jealous by claiming to be better than they are.