previous next

Waebrania 5

1 Kila kuhani mkuu ambaye huchaguliwa miongoni mwa watu hupewa jukumu la kushughulikia mambo ya Mungu kwa niaba ya watu, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi. 2 Maadamu yeye mwenyewe ni dhaifu, anaweza kuwatendea kwa huruma wale wasiojua kitu na wanaofanya makosa. 3 Kwa sababu hiyo anapaswa kutoa tambiko si tu kwa ajili ya watu, bali pia kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe. 4 Hakuna mtu awezaye kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni.

5  t Hali kadhalika naye Kristo; yeye hakujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhani mkuu, bali Mungu alimteua na kumwambia: “Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa baba yako.”

6  t Alisema pia mahali pengine: “Wewe ni kuhani milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”

7 Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kifoni; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu. 8 Lakini, ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, alijifunza kutii kwa njia ya mateso. 9 Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii, 10 naye Mungu akamteua kuwa kuhani mkuu kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.

Onyo kuhusu uasi

11 Tunayo mengi ya kusema juu ya jambo hili, lakini ni vigumu kuwaelezeni, kwa sababu nyinyi si wepesi wa kuelewa. 12 Kwa wakati huu nyinyi mngalipaswa kuwa waalimu tayari, lakini mnahitaji bado mtu wa kuwafundisheni mafundisho ya mwanzo juu ya neno la Mungu. Mnahitaji maziwa badala ya chakula kigumu. 13 Kila anayepaswa kunywa maziwa ni mtoto bado, hajui uadilifu ni nini. 14 Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, waliofunzwa kwa vitendo kubainisha mema na mabaya.

Hebrews 5

1 For every high priest, being taken from among men, is appointed for men in things pertaining to God, that he may offer both gifts and sacrifices for sins:2 who can bear gently with the ignorant and erring, for that he himself also is compassed with infirmity;3 and by reason thereof is bound, as for the people, so also for himself, to offer for sins.4 And no man taketh the honor unto himself, but when he is called of God, even as was Aaron.5 So Christ also glorified not himself to be made a high priest, but he that spake unto him, Thou art my Son, This day have I begotten thee:

6 as he saith also in another place, Thou art a priest for ever After the order of Melchizedek.

7 Who in the days of his flesh, having offered up prayers and supplications with strong crying and tears unto him that was able to save him from death, and having been heard for his godly fear,8 though he was a Son, yet learned obedience by the things which he suffered;9 and having been made perfect, he became unto all them that obey him the author of eternal salvation;10 named of God a high priest after the order of Melchizedek.11 Of whom we have many things to say, and hard of interpretation, seeing ye are become dull of hearing.12 For when by reason of the time ye ought to be teachers, ye have need again that some one teach you the rudiments of the first principles of the oracles of God; and are become such as have need of milk, and not of solid food.13 For every one that partaketh of milk is without experience of the word of righteousness; for he is a babe.14 But solid food is for fullgrown men, even those who by reason of use have their senses exercised to discern good and evil.