EBR. 5
1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; 2 tawezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu; 3 tna kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. 4 tNa hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.
5 tVivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa.
6 tkama asemavyo mahali pengine,
Ndiwe kuhani milele
Kwa mfano wa Melkizedeki.
7 tYeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 8 tna, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 9 tnaye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.Maonyo dhidi ya Uasi
11 Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12 tKwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13 tKwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14 tLakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.
HEBREWS 5
1 Every high priest is appointed to help others by offering gifts and sacrifices to God because of their sins. 2 A high priest has weaknesses of his own, and he feels sorry for foolish and sinful people. 3 t This is why he must offer sacrifices for his own sins and for the sins of others.
4 t But no one can have the honor of being a high priest simply by wanting to be one. Only God can choose a priest, and God is the one who chose Aaron.
5 t This is how it was with Christ. He became a high priest, but not just because he wanted the honor of being one. It was God who told him,
“You are my Son, because today
I have become your Father!”
6 t In another place, God says,
“You are a priest forever
just like Melchizedek.”t
7 t God had the power to save Jesus from death. And while Jesus was on earth, he begged God with loud crying and tears to save him. He truly worshiped God, and God listened to his prayers. 8 Jesus is God's own Son, but still he had to suffer before he could learn what it really means to obey God. 9 Suffering made Jesus perfect, and now he can save forever all who obey him.
10 This is because God chose him to be a high priest like Melchizedek.Warning against Turning Away
11 Much more could be said about this subject. But it is hard to explain, and all of you are slow to understand. 12 t By now you should have been teachers, but once again you need to be taught the simplest things about what God has said. You need milk instead of solid food. 13 People who live on milk are like babies who don't really know what is right. 14 Solid food is for mature people who have been trained to know right from wrong.