YAK. 3
Kuuchunga Ulimi
1 tNdugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi. 2 tMaana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. 3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote. 4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha. 5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana. 6 tNao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum. 7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu. 8 tBali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9 tKwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo. 11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.Aina Mbili za Hekima
13 tN’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. 14 tLakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. 15 tHekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. 16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. 17 tLakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. 18 tNa tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
JAMES 3
The Tongue
1 My friends, we should not all try to become teachers. In fact, teachers will be judged more strictly than others.
2 t All of us do many wrong things. But if you can control your tongue, you are mature and able to control your whole body.
3 By putting a bit into the mouth of a horse, we can turn the horse in different directions. 4 It takes strong winds to move a large sailing ship, but the captain uses only a small rudder to make it go in any direction.
5 Our tongues are small too, and yet they brag about big things.
It takes only a spark to start a forest fire! 6 t The tongue is like a spark. It is an evil power that dirties the rest of the body and sets a person's entire life on fire with flames that come from hell itself. 7 All kinds of animals, birds, reptiles, and sea creatures can be tamed and have been tamed.
8 But our tongues get out of control. They are restless and evil, and always spreading deadly poison.
9-10 t My dear friends, with our tongues we speak both praises and curses. We praise our Lord and Father, and we curse people who were created to be like God, and this isn't right. 11 Can clean water and dirty water both flow from the same spring?
12 Can a fig tree produce olives or a grapevine produce figs? Does fresh water come from a well full of salt water?Wisdom from Above
13 t Are any of you wise or sensible? Then show it by living right and by being humble and wise in everything you do. 14 But if your heart is full of bitter jealousy and selfishness, don't brag or lie to cover up the truth. 15 This kind of wisdom doesn't come from above. It is earthly and selfish and comes from the devil himself. 16 Whenever people are jealous or selfish, they cause trouble and do all sorts of cruel things. 17 But the wisdom that comes from above leads us to be pure, friendly, gentle, sensible, kind, helpful, genuine, and sincere. 18 When peacemakers plant seeds of peace, they will harvest justice.