previous next

YN. 1

Neno akawa Mwili

1  tHapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 tHuyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 tVyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4 tNdani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

5 tNayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
6  tPalitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7 tHuyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. 8 tHuyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. 9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10 tAlikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12 tBali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 twaliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

14 tNaye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
15  tYohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16 tKwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. 17 tKwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

18 tHakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji


19  tNa huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20 tNaye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. 21 tWakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. 22 Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? 23 tAkasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. 24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. 25 tWakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? 26 tYohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27 tNdiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

28 tHayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.

Mwanakondoo wa Mungu


29  tSiku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 tHuyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31 Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. 32 tTena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33 tWala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.

34 tNami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

Wanafunzi wa kwanza wa Yesu


35 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36 tAkamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40 tAndrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41 tHuyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).

42 tAkampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

Yesu Awaita Filipo na Nathanaeli


43  tSiku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. 44 Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45 tFilipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 46 tNathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. 47 tBasi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. 48 Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 49 tNathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. 50 Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. 51 tAkamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

JOHN 1

The Word of Life

1 In the beginning was the one
who is called the Word.
The Word was with God
and was truly God.

2 From the very beginning
the Word was with God.

3 And with this Word,
God created all things.
Nothing was made
without the Word.
Everything that was created

4 received its life from him,
and his life gave light
to everyone.

5 The light keeps shining
in the dark,
and darkness has never
put it out.t

6  t God sent a man named John,

7 who came to tell
about the light
and to lead all people
to have faith.

8 John wasn't this light.
He came only to tell
about the light.

9 The true light that shines
on everyone
was coming into the world.

10 The Word was in the world,
but no one knew him,
though God had made the world
with his Word.

11 He came into his own world,
but his own nation
did not welcome him.

12 Yet some people accepted him
and put their faith in him.
So he gave them the right
to be the children of God.

13 They were not God's children
by nature or because
of any human desires.
God himself was the one
who made them his children.

14 The Word became
a human being
and lived here with us.
We saw his true glory,
the glory of the only Son
of the Father.
From him the complete gifts
of undeserved grace and truth
have come down to us.

15 John spoke about him and shouted, “This is the one I told you would come! He is greater than I am, because he was alive before I was born.”
16 Because of all that the Son is, we have been given one blessing after another.t 17 The Law was given by Moses, but Jesus Christ brought us undeserved kindness and truth.

18 No one has ever seen God. The only Son, who is truly God and is closest to the Father, has shown us what God is like.

John the Baptist Tells //about Jesus

(Matthew 3.1-12; Mark 1.1-8; Luke 3.15-17)


19-20 The religious authorities in Jerusalem sent priests and temple helpers to ask John who he was. He told them plainly, “I am not the Messiah.”

21 t Then when they asked him if he were Elijah, he said, “No, I am not!” And when they asked if he were the Prophet, t he also said “No!”

22 Finally, they said, “Who are you then? We have to give an answer to the ones who sent us. Tell us who you are!”

23  t John answered in the words of the prophet Isaiah, “I am only someone shouting in the desert, ‘Get the road ready for the Lord!’ ”
24 Some Pharisees had also been sent to John.

25 They asked him, “Why are you baptizing people, if you are not the Messiah or Elijah or the Prophet?”
26 John told them, “I use water to baptize people. But here with you is someone you don't know. 27 Even though I came first, I am not good enough to untie his sandals.”

28 John said this as he was baptizing east of the Jordan River in Bethany.t

The Lamb of God


29 The next day, John saw Jesus coming toward him and said:
Here is the Lamb of God who takes away the sin of the world!
30 He is the one I told you about when I said, “Someone else will come, who is greater than I am, because he was alive before I was born.”

31 I didn't know who he was. But I came to baptize you with water, so that everyone in Israel would see him.
32 I was there and saw the Spirit come down on him like a dove from heaven. And the Spirit stayed on him. 33 Before this I didn't know who he was. But the one who sent me to baptize with water had told me, “You will see the Spirit come down and stay on someone. Then you will know that he is the one who will baptize with the Holy Spirit.”

34 I saw this happen, and I tell you that he is the Son of God.

The First Disciples of Jesus


35 The next day, John was there again, and two of his followers were with him. 36 When he saw Jesus walking by, he said, “Here is the Lamb of God!”

37 John's two followers heard him, and they went with Jesus.

38 When Jesus turned and saw them, he asked, “What do you want?”
They answered, “Rabbi, where do you live?” The Hebrew word “Rabbi” means “Teacher.”

39 Jesus replied, “Come and see!” It was already about four o'clock in the afternoon when they went with him and saw where he lived. So they stayed on for the rest of the day.
40 One of the two men who had heard John and had gone with Jesus was Andrew, the brother of Simon Peter.

41 The first thing Andrew did was to find his brother and tell him, “We have found the Messiah!” The Hebrew word “Messiah” means the same as the Greek word “Christ.”

42 Andrew brought his brother to Jesus. And when Jesus saw him, he said, “Simon son of John, you will be called Cephas.” This name can be translated as “Peter.”t

Jesus Chooses Philip //and Nathanael


43-44 The next day Jesus decided to go to Galilee. There he met Philip, who was from Bethsaida, the hometown of Andrew and Peter. Jesus said to Philip, “Follow me.”

45 Philip then found Nathanael and said, “We have found the one that Moses and the Prophetst wrote about. He is Jesus, the son of Joseph from Nazareth.”

46 Nathanael asked, “Can anything good come from Nazareth?”
Philip answered, “Come and see.”

47 When Jesus saw Nathanael coming toward him, he said, “Here is a true descendant of our ancestor Israel. And he isn't deceitful.”t

48 “How do you know me?” Nathanael asked.
Jesus answered, “Before Philip called you, I saw you under the fig tree.”

49 Nathanael said, “Rabbi, you are the Son of God and the King of Israel!”
50 Jesus answered, “Did you believe me just because I said that I saw you under the fig tree? You will see something even greater. 51 t I tell you for certain you will see heaven open and God's angels going up and coming down on the Son of Man.”t