YN. 11
Kifo cha Lazaro
1 tBasi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. 2 tNdiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. 3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. 4 tNaye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. 5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. 6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. 7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. 8 tWale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? 9 tYesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10 tBali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. 11 tAliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. 15 tNami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake.
16 tBasi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye.Yesu aliye Ufufuo na Uzima
17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. 18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; 19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. 20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. 21 tBasi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. 23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. 24 tMartha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 tnaye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
27 tAkamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.Yesu Alia
28 Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. 29 Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea. 30 tNa Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. 31 Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko. 32 tBasi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 33 tBasi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, 34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. 35 tYesu akalia machozi. 36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.
37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?Yesu Amfufua Lazaro
38 tBasi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 tYesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 tYesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 tNami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.Njama za Kumwua Yesu
45 tBasi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini.
46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu.
47 Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. 48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 twala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. 51 tNa neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. 52 tWala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.
53 Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.
54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. 55 tNa Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase. 56 Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii? 57 Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata.
JOHN 11
The Death of Lazarus
1-2 t A man by the name of Lazarus was sick in the village of Bethany. He had two sisters, Mary and Martha. This was the same Mary who later poured perfume on the Lord's head and wiped his feet with her hair.
3 The sisters sent a message to the Lord and told him that his good friend Lazarus was sick.
4 When Jesus heard this, he said, “His sickness won't end in death. It will bring glory to God and his Son.”
5 Jesus loved Martha and her sister and brother. 6 But he stayed where he was for two more days.
7 Then he said to his disciples, “Now we will go back to Judea.”
8 “Teacher,” they said, “the people there want to stone you to death! Why do you want to go back?”
9 Jesus answered, “Aren't there twelve hours in each day? If you walk during the day, you will have light from the sun, and you won't stumble. 10 But if you walk during the night, you will stumble, because you don't have any light.”
11 Then he told them, “Our friend Lazarus is asleep, and I am going there to wake him up.”
12 They replied, “Lord, if he is asleep, he will get better.”
13 Jesus really meant that Lazarus was dead, but they thought he was talking only about sleep.
14 Then Jesus told them plainly, “Lazarus is dead!
15 I am glad I wasn't there, because now you will have a chance to put your faith in me. Let's go to him.”
16 Thomas, whose nickname was “Twin,” said to the other disciples, “Come on. Let's go, so we can die with him.”Jesus Brings Lazarus to Life
17 When Jesus got to Bethany, he found that Lazarus had already been in the tomb four days. 18 Bethany was less than three kilometers from Jerusalem,
19 and many people had come from the city to comfort Martha and Mary because their brother had died.
20 When Martha heard that Jesus had arrived, she went out to meet him, but Mary stayed in the house. 21 Martha said to Jesus, “Lord, if you had been here, my brother would not have died.
22 Yet even now I know that God will do anything you ask.”
23 Jesus told her, “Your brother will live again!”
24 t Martha answered, “I know he will be raised to life on the last day, t when all the dead are raised.”
25 Jesus then said, “I am the one who raises the dead to life! Everyone who has faith in me will live, even if they die.
26 And everyone who lives because of faith in me will never really die. Do you believe this?”
27 “Yes, Lord!” she replied. “I believe you are the Christ, the Son of God. You are the one we hoped would come into the world.”
28 After Martha said this, she went and privately said to her sister Mary, “The Teacher is here, and he wants to see you.” 29 As soon as Mary heard this, she got up and went out to Jesus. 30 He was still outside the village where Martha had gone to meet him.
31 Many people had come to comfort Mary, and when they saw her quickly leave the house, they thought she was going out to the tomb to cry. So they followed her.
32 Mary went to where Jesus was. Then as soon as she saw him, she knelt at his feet and said, “Lord, if you had been here, my brother would not have died.”
33 When Jesus saw that Mary and the people with her were crying, he was terribly upset
34 and asked, “Where have you put his body?”
They replied, “Lord, come and you will see.”
35 Jesus started crying,
36 and the people said, “See how much he loved Lazarus.”
37 Some of them said, “He gives sight to the blind. Why couldn't he have kept Lazarus from dying?”
38 Jesus was still terribly upset. So he went to the tomb, which was a cave with a stone rolled against the entrance.
39 Then he told the people to roll the stone away. But Martha said, “Lord, you know that Lazarus has been dead four days, and there will be a bad smell.”
40 Jesus replied, “Didn't I tell you that if you had faith, you would see the glory of God?”
41 After the stone had been rolled aside, Jesus looked up toward heaven and prayed, “Father, I thank you for answering my prayer.
42 I know that you always answer my prayers. But I said this, so the people here would believe you sent me.”
43 When Jesus had finished praying, he shouted, “Lazarus, come out!”
44 The man who had been dead came out. His hands and feet were wrapped with strips of burial cloth, and a cloth covered his face.
Jesus then told the people, “Untie him and let him go.”The Plot To Kill Jesus
(Matthew 26.1-5; Mark 14.1,2; Luke 22.1,2)
45 Many of the people who had come to visit Mary saw the things Jesus did, and they put their faith in him. 46 Others went to the Pharisees and told what Jesus had done. 47 Then the chief priests and the Pharisees called the council together and said, “What should we do? This man is working a lot of miracles.t
48 If we don't stop him now, everyone will put their faith in him. Then the Romans will come and destroy our temple and our nation.”t
49 One of the council members was Caiaphas, who was also high priest that year. He spoke up and said, “You people don't have any sense at all! 50 Don't you know it is better for one person to die for the people than for the whole nation to be destroyed?” 51 Caiaphas did not say this on his own. As high priest that year, he was prophesying that Jesus would die for the nation. 52 Yet Jesus would not die just for the Jewish nation. He would die to bring together all of God's scattered people.
53 From that day on, the council started making plans to put Jesus to death.
54 Because of this plot against him, Jesus stopped going around in public. He went to the town of Ephraim, which was near the desert, and he stayed there with his disciples.
55 It was almost time for Passover. Many of the Jewish people who lived out in the country had come to Jerusalem to get themselves readyt for the festival.
56 They looked around for Jesus. Then when they were in the temple, they asked each other, “You don't think he will come here for Passover, do you?”
57 The chief priests and the Pharisees told the people to let them know if any of them saw Jesus. This is how they hoped to arrest him.