Yohane 16
1 “Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. 2 Watu watawafukuza nyinyi katika masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua nyinyi atadhani anamhudumia Mungu. 3 Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi. 4 Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni.
Kazi ya Roho Mtakatifu
“Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
5 Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: ‘Unakwenda wapi?’ 6 Kwa kuwa nimewaambieni mambo hayo mmejaa huzuni mioyoni mwenu. 7 Lakini, nawaambieni ukweli: Afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu. 8 Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu. 9 Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu uadilifu, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, nanyi hamtaniona tena; 11 kuhusu hukumu, kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa.
12 “Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili. 13 Lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. 14 Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atawajulisheni yale atakayopata kutoka kwangu. 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho atawajulisheni yale atakayopata kutoka kwangu.
Huzuni na furaha
16 “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!” 17 Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, “Ana maana gani anapotuambia: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’ Tena anasema: ‘Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!’” 18 Basi, wakawa wanaulizana, “Ana maana gani anaposema: ‘Bado kitambo kidogo?’ Hatuelewi anasema nini.” 19 Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, “Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona?’ 20 Nawaambieni kweli, nyinyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi; mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Wakati mama anapojifungua huona huzuni kwa sababu saa ya maumivu imefika; lakini akisha jifungua hayakumbuki tena maumivu hayo kwa sababu ya furaha kwamba mtu amezaliwa duniani. 22 Nyinyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu. 23 Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni. 24 Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.
Nimeushinda ulimwengu
25 “Nimewaambieni mambo hayo kwa mafumbo. Lakini wakati utakuja ambapo sitasema tena nanyi kwa mafumbo, bali nitawaambieni waziwazi juu ya Baba. 26 Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 maana yeye mwenyewe anawapenda nyinyi, kwa sababu nyinyi mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 28 Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni; na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba.”
29 Basi, wanafunzi wake wakamwambia, “Ahaa! Sasa unasema waziwazi kabisa bila kutumia mafumbo. 30 Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu.” 31 Yesu akawajibu, “Je, mnaamini sasa? 32 Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo nyinyi nyote mtatawanywa kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami. 33 Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!”
John 16
1 These things have I spoken unto you, that ye should not be caused to stumble.2 They shall put you out of the synagogues: yea, the hour cometh, that whosoever killeth you shall think that he offereth service unto God.3 And these things will they do, because they have not known the Father, nor me.4 But these things have I spoken unto you, that when their hour is come, ye may remember them, how that I told you. And these things I said not unto you from the beginning, because I was with you.5 But now I go unto him that sent me; and none of you asketh me, Whither goest thou?6 But because I have spoken these things unto you, sorrow hath filled your heart.7 Nevertheless I tell you the truth: It is expedient for you that I go away; for if I go not away, the Comforter will not come unto you; but if I go, I will send him unto you.8 And he, when he is come, will convict the world in respect of sin, and of righteousness, and of judgment:9 of sin, because they believe not on me;10 of righteousness, because I go to the Father, and ye behold me no more;11 of judgment, because the prince of this world hath been judged.12 I have yet many things to say unto you, but ye cannot bear them now.13 Howbeit when he, the Spirit of truth, is come, he shall guide you into all the truth: for he shall not speak from himself; but what things soever he shall hear, these shall he speak: and he shall declare unto you the things that are to come.14 He shall glorify me: for he shall take of mine, and shall declare it unto you.15 All things whatsoever the Father hath are mine: therefore said I, that he taketh of mine, and shall declare it unto you.16 A little while, and ye behold me no more; and again a little while, and ye shall see me.17 Some of his disciples therefore said one to another, What is this that he saith unto us, A little while, and ye behold me not; and again a little while, and ye shall see me: and, Because I go to the Father?18 They said therefore, What is this that he saith, A little while? We know not what he saith.19 Jesus perceived that they were desirous to ask him, and he said unto them, Do ye inquire among yourselves concerning this, that I said, A little while, and ye behold me not, and again a little while, and ye shall see me?20 Verily, verily, I say unto you, that ye shall weep and lament, but the world shall rejoice: ye shall be sorrowful, but your sorrow shall be turned into joy.21 A woman when she is in travail hath sorrow, because her hour is come: but when she is delivered of the child, she remembereth no more the anguish, for the joy that a man is born into the world.22 And ye therefore now have sorrow: but I will see you again, and your heart shall rejoice, and your joy no one taketh away from you.23 And in that day ye shall ask me no question. Verily, verily, I say unto you, if ye shall ask anything of the Father, he will give it you in my name.24 Hitherto have ye asked nothing in my name: ask, and ye shall receive, that your joy may be made full.25 These things have I spoken unto you in dark sayings: the hour cometh, when I shall no more speak unto you in dark sayings, but shall tell you plainly of the Father.26 In that day ye shall ask in my name: and I say not unto you, that I will pray the Father for you;27 for the Father himself loveth you, because ye have loved me, and have believed that I came forth from the Father.28 I came out from the Father, and am come into the world: again, I leave the world, and go unto the Father.29 His disciples say, Lo, now speakest thou plainly, and speakest no dark saying.30 Now know we that thou knowest all things, and needest not that any man should ask thee: by this we believe that thou camest forth from God.31 Jesus answered them, Do ye now believe?32 Behold, the hour cometh, yea, is come, that ye shall be scattered, every man to his own, and shall leave me alone: and yet I am not alone, because the Father is with me.33 These things have I spoken unto you, that in me ye may have peace. In the world ye have tribulation: but be of good cheer; I have overcome the world.