previous next

YN. 17

Yesu Awaombea Wanafunzi wake

1  tManeno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2 tkama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 3 tNa uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 tMimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. 5 tNa sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 6 tJina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 8 tKwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 9 tMimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

10 tna wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.
11  tWala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 12 tNilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 13 tNa sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14 tMimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 tMimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17 tUwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18 tKama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.

19 tNa kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20  tWala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 tWote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 tNami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 tMimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24 tBaba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

JOHN 17

Jesus Prays

1 After Jesus had finished speaking to his disciples, he looked up toward heaven and prayed:
Father, the time has come for you to bring glory to your Son, in order that he may bring glory to you.
2 And you gave him power over all people, so he would give eternal life to everyone you give him. 3 t Eternal life is to know you, the only true God, and to know Jesus Christ, the one you sent. 4 I have brought glory to you here on earth by doing everything you gave me to do.

5 Now, Father, give me back the glory I had with you before the world was created.
6 You have given me some followers from this world, and I have shown them what you are like. They were yours, but you gave them to me, and they have obeyed you. 7 They know that you gave me everything I have. 8 I told my followers what you told me, and they accepted it. They know I came from you, and they believe you are the one who sent me. 9 I am praying for them, but not for those who belong to this world.t My followers belong to you, and I am praying for them.

10 All I have is yours, and all you have is mine, and they will bring glory to me.
11 Holy Father, I am no longer in the world. I am coming to you, but my followers are still in the world. So keep them safe by the power of the name you have given me. Then they will be one with each other, just as you and I are one.

12 t While I was with them, I kept them safe by the power you have given me. I guarded them, and not one of them was lost, except the one who had to be lost. This happened so that what the Scriptures say would come true.
13 I am on my way to you. But I say these things while I am still in the world, so my followers will have the same complete joy that I do.

14 I have told them your message. But the people of this world hate them, because they don't belong to this world, just as I don't.
15 Father, I don't ask you to take my followers out of the world, but keep them safe from the evil one. 16 They don't belong to this world, and neither do I. 17 Your word is the truth. So let this truth make them completely yours. 18 I am sending them into the world, just as you sent me.

19 I have given myself completely for their sake, so they may belong completely to the truth.
20 I am not praying just for these followers. I am also praying for everyone else who will have faith because of what my followers will say about me.

21 I want all of them to be one with each other, just as I am one with you and you are one with me. I also want them to be one with us. Then the people of this world will believe that you sent me.
22 I have honored my followers in the same way you honored me, in order that they may be one with each other, just as we are one.

23 I am one with them, and you are one with me, so they may become completely one. Then this world's people will know that you sent me. They will know that you love my followers as much as you love me.
24 Father, I want everyone you have given me to be with me, wherever I am. Then they will see the glory you have given me, because you loved me before the world was created. 25 Good Father, the people of this world don't know you. But I know you, and my followers know that you sent me. 26 I told them what you are like, and I will tell them even more. Then the love you have for me will become part of them, and I will be one with them.