YN. 2
Harusi ya Kana
1 tNa siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 tYesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5 Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. 6 tBasi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. 8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. 9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, 10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
11 tMwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
12 tBaada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.Yesu Atakasa Hekalu
13 tNa Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. 14 tAkaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. 15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16 takawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. 17 tWanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila. 18 tBasi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? 19 tYesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. 20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? 21 tLakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.
22 Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
23 Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya. 24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; 25 tna kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.
JOHN 2
Jesus at a Wedding in Cana
1 Three days later Mary, the mother of Jesus, was at a wedding feast in the village of Cana in Galilee.
2 Jesus and his disciples had also been invited and were there.
3 When the wine was all gone, Mary said to Jesus, “They don't have any more wine.”
4 Jesus replied, “Mother, my time hasn't yet come!t You must not tell me what to do.”
5 Mary then said to the servants, “Do whatever Jesus tells you to do.”
6 At the feast there were six stone water jars that were used by the people for washing themselves in the way that their religion said they must. Each jar held about 100 liters . 7 Jesus told the servants to fill them to the top with water. Then after the jars had been filled,
8 he said, “Now take some water and give it to the man in charge of the feast.”
The servants did as Jesus told them, 9 and the man in charge drank some of the water that had now turned into wine. He did not know where the wine had come from, but the servants did. He called the bridegroom over
10 and said, “The best wine is always served first. Then after the guests have had plenty, the other wine is served. But you have kept the best until last!”
11 This was Jesus' first miracle, t and he did it in the village of Cana in Galilee. There Jesus showed his glory, and his disciples put their faith in him.
12 t After this, he went with his mother, his brothers, and his disciples to the town of Capernaum, where they stayed for a few days.Jesus in the Temple
(Matthew 21.12,13; Mark 11.15-17; Luke 19.45,46)
13 t Not long before the Jewish festival of Passover, Jesus went to Jerusalem. 14 There he found people selling cattle, sheep, and doves in the temple. He also saw moneychangers sitting at their tables.
15 So he took some rope and made a whip. Then he chased everyone out of the temple, together with their sheep and cattle. He turned over the tables of the moneychangers and scattered their coins.
16 Jesus said to the people who had been selling doves, “Get those doves out of here! Don't make my Father's house a marketplace.”
17 t The disciples then remembered that the Scriptures say, “My love for your house burns in me like a fire.”
18 The Jewish leaders asked Jesus, “What miraclet will you work to show us why you have done this?”
19 t “Destroy this temple,” Jesus answered, “and in three days I will build it again!”
20 The leaders replied, “It took 46 years to build this temple. What makes you think you can rebuild it in three days?”
21 But Jesus was talking about his body as a temple.
22 And when he was raised from death, his disciples remembered what he had told them. Then they believed the Scriptures and the words of Jesus.Jesus Knows //What People Are Like
23 In Jerusalem during Passover many people put their faith in Jesus, because they saw him work miracles.t 24 But Jesus knew what was in their hearts, and he would not let them have power over him. 25 No one had to tell him what people were like. He already knew.