previous next

YN. 4

Yesu na Mwanamke Msamaria

1  tKwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, 2 t(lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,) 3 aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya. 4 tNaye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. 5 tBasi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. 6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. 7 Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. 8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9 tBasi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) 10 tYesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12 tJe! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 tYesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 twalakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. 19 tYule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! 20 tBaba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21 tYesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 tNinyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 tMungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 25 tYule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.

26 tYesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
27 Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye? 28 Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, 29 Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? 30 Basi wakatoka mjini, wakamwendea. 31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule. 32 tAkawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34 tYesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. 35 tHamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. 36 Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. 37 tKwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine.

38 Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
39 Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. 40 Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake.

42 tWakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.

Yesu Arudi Galilaya


43  tNa baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya. 44 tKwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.

45 tBasi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.

Yesu Amponya Mwana wa Ofisa


46  tBasi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. 47 tHuyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. 48 tBasi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? 49 Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. 50 Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia. 51 tHata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. 52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha. 53 tBasi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake. 54 tHiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.

JOHN 4

1 Jesus knew that the Pharisees had heard that he was winning and baptizing more followers than John was.

2 But Jesus' disciples were really the ones doing the baptizing, and not Jesus himself.

Jesus //and the Samaritan Woman


3 Jesus left Judea and started for Galilee again. 4 This time he had to go through Samaria, 5 t and on his way he came to the town of Sychar. It was near the field that Jacob had long ago given to his son Joseph.

6-8 The well that Jacob had dug was still there, and Jesus sat down beside it because he was tired from traveling. It was noon, and after Jesus' disciples had gone into town to buy some food, a Samaritan woman came to draw water from the well.
Jesus asked her, “Would you please give me a drink of water?”

9  t “You are a Jew,” she replied, “and I am a Samaritan woman. How can you ask me for a drink of water when Jews and Samaritans won't have anything to do with each other?”t

10 Jesus answered, “You don't know what God wants to give you, and you don't know who is asking you for a drink. If you did, you would ask me for the water that gives life.”
11 “Sir,” the woman said, “you don't even have a bucket, and the well is deep. Where are you going to get this life-giving water?

12 Our ancestor Jacob dug this well for us, and his family and animals got water from it. Are you greater than Jacob?”
13 Jesus answered, “Everyone who drinks this water will get thirsty again.

14 But no one who drinks the water I give will ever be thirsty again. The water I give will become in that person a flowing fountain that gives eternal life.”

15 The woman replied, “Sir, please give me a drink of that water! Then I won't get thirsty and have to come to this well again.”

16 Jesus told her, “Go and bring your husband.”

17-18 The woman answered, “I don't have a husband.”
“That's right,” Jesus replied, “you're telling the truth. You don't have a husband. You have already been married five times, and the man you are now living with isn't your husband.”
19 The woman said, “Sir, I can see that you are a prophet.

20 My ancestors worshiped on this mountain, t but you Jews say Jerusalem is the only place to worship.”

21 Jesus said to her:
Believe me, the time is coming when you won't worship the Father either on this mountain or in Jerusalem.
22 You Samaritans don't really know the one you worship. But we Jews do know the God we worship, and by using us, God will save the world. 23 But a time is coming, and it is already here! Even now the true worshipers are being led by the Spirit to worship the Father according to the truth. These are the ones the Father is seeking to worship him.

24 God is Spirit, and those who worship God must be led by the Spirit to worship him according to the truth.

25 The woman said, “I know that the Messiah will come. He is the one we call Christ. When he comes, he will explain everything to us.”

26 “I am that one,” Jesus told her, “and I am speaking to you now.”

27 The disciples returned about this time and were surprised to find Jesus talking with a woman. But none of them asked him what he wanted or why he was talking with her.
28 The woman left her water jar and ran back into town, where she said to the people, 29 “Come and see a man who told me everything I have ever done! Could he be the Messiah?”

30 Everyone in town went out to see Jesus.

31 While this was happening, Jesus' disciples were saying to him, “Teacher, please eat something.”

32 But Jesus told them, “I have food you don't know anything about.”

33 His disciples started asking each other, “Has someone brought him something to eat?”

34 Jesus said:
My food is to do what God wants! He is the one who sent me, and I must finish the work that he gave me to do.

35 You may say there are still four months until harvest time. But I tell you to look, and you will see that the fields are ripe and ready to harvest.
36 Even now the harvest workers are receiving their reward by gathering a harvest that brings eternal life. Then everyone who planted the seed and everyone who harvests the crop will celebrate together. 37 So the saying proves true, “Some plant the seed, and others harvest the crop.”

38 I am sending you to harvest crops in fields where others have done all the hard work.
39 A lot of Samaritans in that town put their faith in Jesus because the woman had said, “This man told me everything I have ever done.”

40 They came and asked him to stay in their town, and he stayed on for two days.
41 Many more Samaritans put their faith in Jesus because of what they heard him say.

42 They told the woman, “We no longer have faith in Jesus just because of what you told us. We have heard him ourselves, and we are certain that he is the Savior of the world!”

Jesus Heals an Official's Son

(Matthew 8.5-13; Luke 7.1-10)


43-44  t Jesus had said, “Prophets are honored everywhere, except in their own country.” Then two days later he left

45 t and went to Galilee. The people there welcomed him, because they had gone to the festival in Jerusalem and had seen everything he had done.
46  t While Jesus was in Galilee, he returned to the village of Cana, where he had turned the water into wine. There was an official in Capernaum whose son was sick.

47 And when the man heard that Jesus had come from Judea, he went and begged him to keep his son from dying.

48 Jesus told the official, “You won't have faith unless you see miracles and wonders!”

49 The man replied, “Lord, please come before my son dies!”

50 Jesus then said, “Your son will live. Go on home to him.” The man believed Jesus and started back home.
51 Some of the official's servants met him along the road and told him, “Your son is better!”

52 He asked them when the boy got better, and they answered, “The fever left him yesterday at one o'clock.”

53 The boy's father realized that at one o'clock the day before, Jesus had told him, “Your son will live!” So the man and everyone in his family put their faith in Jesus.
54 This was the second miraclet that Jesus worked after he left Judea and went to Galilee.