Yohane 6
Yesu anawapa chakula watu elfu tano
(Mat 14:13-21; Marko 6:30-44; Luka 9:10-17)
1 Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au ziwa Tiberia). 2 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa. 3 Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake. 4 Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia. 5 Basi, Yesu alipotazama na kuona umati wa watu ukija kwake, alimwambia Filipo, “Tununue wapi mikate ili watu hawa wapate kula?” 6 (Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.) 7 Filipo akamjibu, “Mikate ya fedha dinari 200 haiwatoshi watu hawa hata kama kila mmoja atapata kipande kidogo tu!” 8 Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, 9 “Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?” 10 Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume 5,000. 11 Yesu akaitwaa ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia watu waliokuwa wameketi; akafanya vivyo hivyo na wale samaki, kila mtu akapata kadiri alivyotaka. 12 Watu waliposhiba Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki visipotee.” 13 Basi, wakakusanya vipande vya mikate ya shayiri walivyobakiza wale watu waliokula, wakajaza vikapu kumi na viwili. 14 Watu walipoiona ishara hiyo aliyoifanya Yesu, wakasema, “Hakika huyu ndiye nabii anayekuja ulimwenguni.” 15 Yesu akajua kwamba watu walitaka kumchukua wamfanye mfalme, akaondoka tena, akaenda mlimani peke yake.
Yesu anatembea juu ya maji
(Mat 14:22-33; Marko 6:45-52)
16 Ilipokuwa jioni wanafunzi wake waliteremka hadi ziwani, 17 wakapanda mashua ili wavuke kwenda Kafarnaumu. Giza lilikuwa limeingia, na Yesu alikuwa hajawafikia bado. 18 Ziwa likaanza kuchafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 19 Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana. 20 Yesu akawaambia, “Ni mimi, msiogope!” 21 Basi wakataka kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walikokuwa wanakwenda.
Watu wanamtafuta Yesu
22 Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao. 23 Mashua nyingine kutoka Tiberia zilifika mahali hapo watu walipokula ile mikate, Bwana alipokwisha mshukuru Mungu. 24 Basi, hao watu walipogundua kwamba Yesu na wanafunzi wake hawakuwapo mahali hapo, walipanda mashua, wakaenda Kafarnaumu wakimtafuta.
Yesu mkate wa uhai
25 Wale watu walipomkuta Yesu ngambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu, ulifika lini hapa?” 26 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. 27 Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishughulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uhai wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.” 28 Wao wakamwuliza, “Tufanye nini ili tuweze kuzitenda kazi za Mungu?” 29 Yesu akawajibu, “Hii ndiyo kazi anayotaka Mungu mwifanye: Kumwamini yule aliyemtuma.”
30 Hapo wakamwambia, “Utafanya ishara gani ili tuione tupate kukuamini? Utafanya kitu gani? 31 t Wazee wetu walikula mana kule jangwani, kama yasemavyo Maandiko: ‘Aliwalisha mkate kutoka mbinguni.’”
32 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mose hakuwapeni mkate kutoka mbinguni; Baba yangu ndiye awapaye nyinyi mkate wa kweli kutoka mbinguni. 33 Maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na aupaye ulimwengu uhai.” 34 Basi, wakamwambia, “Bwana, tupe daima mkate huo.” 35 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uhai. Anayekuja kwangu hataona njaa; anayeniamini hataona kiu kamwe. 36 Lakini niliwaambieni kwamba ingawa mmeniona hamniamini. 37 Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami kamwe sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu, 38 kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwa ya yule aliyenituma. 39 Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: Nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote siku ya mwisho. 40 Maana anachotaka Baba yangu ndicho hiki: Kila amwonaye Mwana na kumwamini awe na uhai wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.”
41 Basi, Wayahudi wakaanza kunungunika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” 42 Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunamjua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?” 43 Yesu akawaambia, “Acheni kunungunika nyinyi kwa nyinyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta kwangu; nami nitamfufua mtu huyo siku ya mwisho. 45 Manabii wameandika: ‘Watu wote watafundishwa na Mungu.’ Kila mtu anayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake, huja kwangu. 46 Hii haina maana kwamba yupo mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yule aliyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. 47 Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uhai wa milele. 48 Mimi ni mkate wa uhai. 49 Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa. 50 Lakini huu ni mkate unaoshuka kutoka mbinguni ili yeyote atakayeula asife. 51 Mimi ni mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huu ataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili ya uhai wa ulimwengu.”
52 Ndipo Wayahudi wakaanza kubishana kati yao: “Anawezaje huyu kutupa mwili wake, tule?” 53 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, msipokula mwili wa Mwana wa Mtu na kunywa damu yake, hamtakuwa na uhai ndani yenu. 54 Anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anao uhai wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa ndani yake. 57 Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu. 58 Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zenu, wakafa. Aulaye mkate huu atakuwa hai milele.” 59 Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu.
Maneno yaletayo uhai wa milele
60 Basi, wengi wa wafuasi wake waliposikia hayo, wakasema, “Haya ni mambo magumu! Nani awezaye kuyasikiliza?” 61 Yesu alijua bila kuambiwa na mtu kwamba wanafunzi wake walikuwa wananungunika juu ya jambo hilo, akawauliza, “Je, jambo hili linawafanya muwe na mashaka? 62 Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza? 63 Roho ndiyo iletayo uhai; mwili hauwezi kitu. Maneno niliyowaambia ni roho na uhai. 64 Hata hivyo, wako baadhi yenu wasioamini.” (Yesu alisema hivyo kwani alijua tangu mwanzo ni kina nani wasioamini, na pia ni nani atakayemsaliti). 65 Kisha akasema, “Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakuna awezaye kuja kwangu asipowezeshwa na Baba yangu.”
66 Kutokana na hayo, wengi wa wafuasi wake walirudi nyuma, wasiandamane naye tena. 67 Basi, Yesu akawauliza wale kumi na wawili, “Je, nanyi pia mwataka kwenda zenu?” 68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno ya uhai wa milele. 69 Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu” 70 Yesu akawaambia, “Je, sikuwachagua nyinyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!” 71 Yesu alisema hayo juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyu alikuwa ndiye atakayemsaliti, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili.
John 6
1 After these things Jesus went away to the other side of the sea of Galilee, which is the sea of Tiberias.2 And a great multitude followed him, because they beheld the signs which he did on them that were sick.3 And Jesus went up into the mountain, and there he sat with his disciples.4 Now the passover, the feast of the Jews, was at hand.5 Jesus therefore lifting up his eyes, and seeing that a great multitude cometh unto him, saith unto Philip, Whence are we to buy bread, that these may eat?6 And this he said to prove him: for he himself knew what he would do.7 Philip answered him, Two hundred shillings’ worth of bread is not sufficient for them, that every one may take a little.8 One of his disciples, Andrew, Simon Peter’s brother, saith unto him,9 There is a lad here, who hath five barley loaves, and two fishes: but what are these among so many?10 Jesus said, Make the people sit down. Now there was much grass in the place. So the men sat down, in number about five thousand.11 Jesus therefore took the loaves; and having given thanks, he distributed to them that were set down; likewise also of the fishes as much as they would.12 And when they were filled, he saith unto his disciples, Gather up the broken pieces which remain over, that nothing be lost.13 So they gathered them up, and filled twelve baskets with broken pieces from the five barley loaves, which remained over unto them that had eaten.14 When therefore the people saw the sign which he did, they said, This is of a truth the prophet that cometh into the world.15 Jesus therefore perceiving that they were about to come and take him by force, to make him king, withdrew again into the mountain himself alone.16 And when evening came, his disciples went down unto the sea;17 and they entered into a boat, and were going over the sea unto Capernaum. And it was now dark, and Jesus had not yet come to them.18 And the sea was rising by reason of a great wind that blew.19 When therefore they had rowed about five and twenty or thirty furlongs, they behold Jesus walking on the sea, and drawing nigh unto the boat: and they were afraid.20 But he saith unto them, It is I; be not afraid.21 They were willing therefore to receive him into the boat: and straightway the boat was at the land whither they were going.22 On the morrow the multitude that stood on the other side of the sea saw that there was no other boat there, save one, and that Jesus entered not with his disciples into the boat, but that his disciples went away alone23 (howbeit there came boats from Tiberias nigh unto the place where they ate the bread after the Lord had given thanks):24 when the multitude therefore saw that Jesus was not there, neither his disciples, they themselves got into the boats, and came to Capernaum, seeking Jesus.25 And when they found him on the other side of the sea, they said unto him, Rabbi, when camest thou hither?26 Jesus answered them and said, Verily, verily, I say unto you, Ye seek me, not because ye saw signs, but because ye ate of the loaves, and were filled.27 Work not for the food which perisheth, but for the food which abideth unto eternal life, which the Son of man shall give unto you: for him the Father, even God, hath sealed.28 They said therefore unto him, What must we do, that we may work the works of God?29 Jesus answered and said unto them, This is the work of God, that ye believe on him whom he hath sent.30 They said therefore unto him, What then doest thou for a sign, that we may see, and believe thee? what workest thou?31 Our fathers ate the manna in the wilderness; as it is written, He gave them bread out of heaven to eat.32 Jesus therefore said unto them, Verily, verily, I say unto you, It was not Moses that gave you the bread out of heaven; but my Father giveth you the true bread out of heaven.33 For the bread of God is that which cometh down out of heaven, and giveth life unto the world.34 They said therefore unto him, Lord, evermore give us this bread.35 Jesus said unto them. I am the bread of life: he that cometh to me shall not hunger, and he that believeth on me shall never thirst.36 But I said unto you, that ye have seen me, and yet believe not.37 All that which the Father giveth me shall come unto me; and him that cometh to me I will in no wise cast out.38 For I am come down from heaven, not to do mine own will, but the will of him that sent me.39 And this is the will of him that sent me, that of all that which he hath given me I should lose nothing, but should raise it up at the last day.40 For this is the will of my Father, that every one that beholdeth the Son, and believeth on him, should have eternal life; and I will raise him up at the last day.41 The Jews therefore murmured concerning him, because he said, I am the bread which came down out of heaven.42 And they said, Is not this Jesus, the son of Joseph, whose father and mother we know? how doth he now say, I am come down out of heaven?43 Jesus answered and said unto them, Murmur not among yourselves.44 No man can come to me, except the Father that sent me draw him: and I will raise him up in the last day.45 It is written in the prophets, And they shall all be taught of God. Every one that hath heard from the Father, and hath learned, cometh unto me.46 Not that any man hath seen the Father, save he that is from God, he hath seen the Father.47 Verily, verily, I say unto you, He that believeth hath eternal life.48 I am the bread of life.49 Your fathers ate the manna in the wilderness, and they died.50 This is the bread which cometh down out of heaven, that a man may eat thereof, and not die.51 I am the living bread which came down out of heaven: if any man eat of this bread, he shall live for ever: yea and the bread which I will give is my flesh, for the life of the world.52 The Jews therefore strove one with another, saying, How can this man give us his flesh to eat?53 Jesus therefore said unto them, Verily, verily, I say unto you, Except ye eat the flesh of the Son of man and drink his blood, ye have not life in yourselves.54 He that eateth my flesh and drinketh my blood hath eternal life: and I will raise him up at the last day.55 For my flesh is meat indeed, and my blood is drink indeed.56 He that eateth my flesh and drinketh my blood abideth in me, and I in him.57 As the living Father sent me, and I live because of the Father; so he that eateth me, he also shall live because of me.58 This is the bread which came down out of heaven: not as the fathers ate, and died; he that eateth this bread shall live for ever.59 These things said he in the synagogue, as he taught in Capernaum.60 Many therefore of his disciples, when they heard this, said, This is a hard saying; who can hear it?61 But Jesus knowing in himself that his disciples murmured at this, said unto them, Doth this cause you to stumble?62 What then if ye should behold the Son of man ascending where he was before?63 It is the spirit that giveth life; the flesh profiteth nothing: the words that I have spoken unto you are spirit, and are life.64 But there are some of you that believe not. For Jesus knew from the beginning who they were that believed not, and who it was that should betray him.65 And he said, For this cause have I said unto you, that no man can come unto me, except it be given unto him of the Father.66 Upon this many of his disciples went back, and walked no more with him.67 Jesus said therefore unto the twelve, Would ye also go away?68 Simon Peter answered him, Lord, to whom shall we go? thou hast the words of eternal life.69 And we have believed and know that thou art the Holy One of God.70 Jesus answered them, Did not I choose you the twelve, and one of you is a devil?71 Now he spake of Judas the son of Simon Iscariot, for he it was that should betray him, being one of the twelve.