previous next

YN. 8

Mwanamke Afumaniwa

1  t[Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni. 2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha. 3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 tBasi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 tNao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 9 tNao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 tAkamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]

Yesu Nuru ya Ulimwengu


12  tBasi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. 13 tBasi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli. 14 tYesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako. 15 tNinyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu. 16 tNami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka. 17 tTena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. 18 tMimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia. 19 tBasi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.

20 tManeno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.

Yesu Atabiri kuhusu Kifo chake


21  tBasi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja. 22 tBasi Wayahudi wakasema, Je! Atajiua! Kwa kuwa asema, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja? 23 tAkawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. 24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu. 25 tBasi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia. 26 tNinayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu. 27 Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba. 28 tBasi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo. 29 tNaye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.

30 tNaye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini.

Wanafunzi wa Kweli


31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 33 tWakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 34 tYesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 tWala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36 tBasi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. 37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.

38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.

Yesu na Abrahamu


39  tWakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu. 40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo. 41 tNinyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. 42 tYesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. 43 tMbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu. 44 tNinyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 45 tNami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. 46 tNi nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?

47 tYeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
48  tWayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo? 49 Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu. 50 tWala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. 51 tAmin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. 52 tBasi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. 53 tWewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? 54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. 55 tWala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. 56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. 57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? 58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. 59 tBasi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.

JOHN 8

1 but Jesus walked out to the Mount of Olives.

2 Then early the next morning he went to the temple. The people came to him, and he sat downt and started teaching them.
3 The Pharisees and the teachers of the Law of Moses brought in a woman who had been caught in bed with a man who wasn't her husband. They made her stand in the middle of the crowd. 4 Then they said, “Teacher, this woman was caught sleeping with a man who isn't her husband.

5 t The Law of Moses teaches that a woman like this should be stoned to death! What do you say?”

6 They asked Jesus this question, because they wanted to test him and bring some charge against him. But Jesus simply bent over and started writing on the ground with his finger.
7  t They kept on asking Jesus about the woman. Finally, he stood up and said, “If any of you have never sinned, then go ahead and throw the first stone at her!” 8 Once again he bent over and began writing on the ground.

9 The people left one by one, beginning with the oldest. Finally, Jesus and the woman were there alone.

10 Jesus stood up and asked her, “Where is everyone? Isn't there anyone left to accuse you?”

11 “No sir,” the woman answered.
Then Jesus told her, “I am not going to accuse you either. You may go now, but don't sin anymore.”t

Jesus Is //the Light for the World


12  t Once again Jesus spoke to the people. This time he said, “I am the light for the world! Follow me, and you won't be walking in the dark. You will have the light that gives life.”

13  t The Pharisees objected, “You are the only one speaking for yourself, and what you say isn't true!”

14 Jesus replied:
Even if I do speak for myself, what I say is true! I know where I came from and where I am going. But you don't know where I am from or where I am going.
15 You judge in the same way that everyone else does, but I don't judge anyone. 16 If I did judge, I would judge fairly, because I would not be doing it alone. The Father who sent me is here with me. 17 t Your Law requires two witnesses to prove that something is true.

18 I am one of my witnesses, and the Father who sent me is the other one.

19 “Where is your Father?” they asked.
“You don't know me or my Father!” Jesus answered. “If you knew me, you would know my Father.”

20 Jesus said this while he was still teaching in the place where the temple treasures were stored. But no one arrested him, because his time had not yet come.t

You Cannot Go Where //I Am Going


21 Jesus also told them, “I am going away, and you will look for me. But you cannot go where I am going, and you will die with your sins unforgiven.”

22 The people asked, “Does he intend to kill himself? Is that what he means by saying we cannot go where he is going?”
23 Jesus answered, “You are from below, but I am from above. You belong to this world, but I don't.

24 This is why I said you will die with your sins unforgiven. If you don't have faith in me for who I am, t you will die, and your sins will not be forgiven.”

25 “Who are you?” they asked Jesus.
Jesus answered, “I am exactly who I told you at the beginning.

26 There is a lot more I could say to condemn you. But the one who sent me is truthful, and I tell the people of this world only what I have heard from him.”

27 No one understood that Jesus was talking to them about the Father.
28 Jesus went on to say, “When you have lifted up the Son of Man, t you will know who I am. You will also know that I don't do anything on my own. I say only what my Father taught me.

29 The one who sent me is with me. I always do what pleases him, and he will never leave me.”

30 After Jesus said this, many of the people put their faith in him.

The Truth Will Set You Free


31 Jesus told the people who had faith in him, “If you keep on obeying what I have said, you truly are my disciples.

32 t You will know the truth, and the truth will set you free.”

33  t They answered, “We are Abraham's children! We have never been anyone's slaves. How can you say we will be set free?”

34 Jesus replied:
I tell you for certain that anyone who sins is a slave of sin!
35 And slaves don't stay in the family forever, though the Son will always remain in the family. 36 If the Son gives you freedom, you are free! 37 I know that you are from Abraham's family. Yet you want to kill me, because my message isn't really in your hearts.

38 I am telling you what my Father has shown me, just as you are doing what your father has taught you.

Your Father Is the Devil


39 The people said to Jesus, “Abraham is our father!”
Jesus replied, “If you were Abraham's children, you would do what Abraham did.
40 Instead, you want to kill me for telling you the truth that God gave me. Abraham never did anything like that.

41 But you are doing exactly what your father does.”
“Don't accuse us of having someone else as our father!” they said. “We just have one father, and he is God.”

42 Jesus answered:
If God were your Father, you would love me, because I came from God and now I am here. He sent me. I did not come on my own.
43 Why can't you understand what I am talking about? Can't you stand to hear what I am saying?

44 t Your father is the devil, and you do exactly what he wants. He has always been a murderer and a liar. There is nothing truthful about him. He speaks on his own, and everything he says is a lie. Not only is he a liar himself, but he is also the father of all lies.
45 Everything I have told you is true, and you still refuse to have faith in me. 46 Can any of you accuse me of sin? If you cannot, why won't you have faith in me? After all, I am telling you the truth.

47 Anyone who belongs to God will listen to his message. But you refuse to listen, because you don't belong to God.

Jesus and Abraham


48 The people told Jesus, “We were right to say that you are a Samaritant and that you have a demon in you!”
49 Jesus answered, “I don't have a demon in me. I honor my Father, and you refuse to honor me. 50 I don't want honor for myself. But there is one who wants me to be honored, and he is also the one who judges.

51 I tell you for certain that if you obey my words, you will never die.”
52 Then the people said, “Now we are sure that you have a demon. Abraham is dead, and so are the prophets. How can you say that no one who obeys your words will ever die?

53 Are you greater than our father Abraham? He died, and so did the prophets. Who do you think you are?”
54 Jesus replied, “If I honored myself, it would mean nothing. My Father is the one who honors me. You claim that he is your God, 55 even though you don't really know him. If I said I didn't know him, I would be a liar, just like all of you. But I know him, and I do what he says.

56 Your father Abraham was really glad to see me.”

57 “You are not even 50 years old!” they said. “How could you have seen Abraham?”
58 Jesus answered, “I tell you for certain that even before Abraham was, I was, and I am.”t 59 The people picked up stones to kill Jesus, but he hid and left the temple.