LK. 10
Huduma ya wale Sabini
1 t tBasi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. 2 tAkawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. 3 tEnendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. 4 ttMsichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. 5 Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; 6 na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. 7 tBasi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. 8 tNa mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; 9 waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia. 10 tNa mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, 11 tHata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.
12 tNawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.Huzuni kwa Miji Isiyotubu
13 tOle wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. 14 Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi. 15 tNawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
16 tAwasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.Kurudi kwa wale Sabini
17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 tAkawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19 tTazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
20 tLakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.Yesu Ashangilia
21 tSaa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. 22 tAkasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. 23 tAkawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.
24 tKwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.Mfano wa Msamaria Mwema
25 t tNa tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? 26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? 27 tAkajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. 28 tAkamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. 29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? 30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. 32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. 33 tLakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. 35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. 36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.Yesu Awatembelea Martha na Mariamu
38 tIkawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. 39 Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. 40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. 41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; 42 tlakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
LUKE 10
The Work //of the Seventy-Two Followers
1 Later the Lord chose 72 t other followers and sent them out two by two to every town and village where he was about to go.
2 t He said to them:
A large crop is in the fields, but there are only a few workers. Ask the Lord in charge of the harvest to send out workers to bring it in. 3 t Now go, but remember, I am sending you like lambs into a pack of wolves. 4 t Don't take along a moneybag or a traveling bag or sandals. And don't waste time greeting people on the road.t 5 As soon as you enter a home, say, “God bless this home with peace.” 6 If the people living there are peace-loving, your prayer for peace will bless them. But if they are not peace-loving, your prayer will return to you.
7 t Stay with the same family, eating and drinking whatever they give you, because workers are worth what they earn. Don't move around from house to house.
8 If the people of a town welcome you, eat whatever they offer.
9 Heal their sick and say, “God's kingdom will soon be here!”t
10 t But if the people of a town refuse to welcome you, go out into the street and say, 11 “We are shaking the dust from our feett as a warning to you. And you can be sure that God's kingdom will soon be here!”t
12 t I tell you that on the day of judgment the people of Sodom will get off easier than the people of that town!The Unbelieving Towns
(Matthew 11.20-24)
13 t You people of Chorazin are in for trouble! You people of Bethsaida are also in for trouble! If the miracles that took place in your towns had happened in Tyre and Sidon, the people there would have turned to God long ago. They would have dressed in sackcloth and put ashes on their heads.t 14 On the day of judgment the people of Tyre and Sidon will get off easier than you will.
15 t People of Capernaum, do you think you will be honored in heaven? Well, you will go down to hell!
16 t My followers, whoever listens to you is listening to me. Anyone who says “No” to you is saying “No” to me. And anyone who says “No” to me is really saying “No” to the one who sent me.The Return of the Seventy-Two
17 When the 72t followers returned, they were excited and said, “Lord, even the demons obeyed when we spoke in your name!”
18 Jesus told them:
I saw Satan fall from heaven like a flash of lightning. 19 t I have given you the power to trample on snakes and scorpions and to defeat the power of your enemy Satan. Nothing can harm you.
20 But don't be happy because evil spirits obey you. Be happy that your names are written in heaven!Jesus Thanks His Father
(Matthew 11.25-27; 13.16,17)
21 At that same time, Jesus felt the joy that comes from the Holy Spirit, t and he said:
My Father, Lord of heaven and earth, I am grateful that you hid all this from wise and educated people and showed it to ordinary people. Yes, Father, this is what pleased you.
22 t My Father has given me everything, and he is the only one who knows the Son. The only one who really knows the Father is the Son. But the Son wants to tell others about the Father, so they can know him too.
23 Jesus then turned to his disciples and said to them in private, “You are really blessed to see what you see!
24 Many prophets and kings were eager to see what you see and to hear what you hear. But I tell you they did not see or hear.”The Good Samaritan
25 t An expert in the Law of Moses stood up and asked Jesus a question to see what he would say. “Teacher,” he asked, “what must I do to have eternal life?”
26 Jesus answered, “What is written in the Scriptures? How do you understand them?”
27 t The man replied, “The Scriptures say, ‘Love the Lord your God with all your heart, soul, strength, and mind.’ They also say, ‘Love your neighbors as much as you love yourself.’ ”
28 t Jesus said, “You have given the right answer. If you do this, you will have eternal life.”
29 But the man wanted to show that he knew what he was talking about. So he asked Jesus, “Who are my neighbors?”
30 Jesus replied:
As a man was going down from Jerusalem to Jericho, robbers attacked him and grabbed everything he had. They beat him up and ran off, leaving him half dead.
31 A priest happened to be going down the same road. But when he saw the man, he walked by on the other side.
32 Later a temple helpert came to the same place. But when he saw the man who had been beaten up, he also went by on the other side.
33 t A man from Samaria then came traveling along that road. When he saw the man, he felt sorry for him 34 and went over to him. He treated his wounds with olive oil and winet and bandaged them. Then he put him on his own donkey and took him to an inn, where he took care of him.
35 The next morning he gave the innkeeper two silver coins and said, “Please take care of the man. If you spend more than this on him, I will pay you when I return.”
36 Then Jesus asked, “Which one of these three people was a real neighbor to the man who was beaten up by robbers?”
37 The expert in the Law of Moses answered, “The one who showed pity.”
Jesus said, “Go and do the same!”Martha and Mary
38 t The Lord and his disciples were traveling along and came to a village. When they got there, a woman named Martha welcomed him into her home. 39 She had a sister named Mary, who sat down in front of the Lord and was listening to what he said.
40 Martha was worried about all that had to be done. Finally, she went to Jesus and said, “Lord, doesn't it bother you that my sister has left me to do all the work by myself? Tell her to come and help me!”
41 The Lord answered, “Martha, Martha! You are worried and upset about so many things, 42 but only one thing is necessary. Mary has chosen what is best, and it will not be taken away from her.”