LK. 11
Sala ya Bwana
1 tIkawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake. 2 tAkawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.] 3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].Kuomba bila Kukoma
5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, 6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; 7 tna yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? 8 tNawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake. 9 tNami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. 10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? 12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?Yesu na Beelzebuli
14 tNaye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu. 15 tWengine wao wakasema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo. 16 tWengine walimjaribu, wakimtaka ishara itokayo mbinguni. 17 Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. 18 Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli. 19 Basi, kama mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu. 20 tLakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. 21 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; 22 tlakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
23 tMtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutawanya.Kurudi kwa Pepo Mchafu
24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, 25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
26 tHata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.Kubarikiwa kwa Kweli
27 tIkawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.
28 tLakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.Ishara ya Yona
29 t tNa makutano walipokuwa wakimkusanyikia, alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. 30 tMaana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki. 31 tMalkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani.
32 tWatu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.
33 tHakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.Taa ya Mwili
34 tTaa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza. 35 Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.
36 Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa mwanga wake.Yesu Awakana Mafarisayo na Wanasheria
37 tAlipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani. 38 tFarisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. 39 tBwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovu. 40 Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia?
41 Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.
42 tLakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili. 43 tOle wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni.
44 Ole wenu, kwa kuwa mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu wapitao juu yake hawana habari nayo.
45 Mtu mmoja katika wana-sheria akajibu, akamwambia, Mwalimu, kwa kusema hayo umetushutumu sisi nasi. 46 Akasema, Nanyi wana-sheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu. 47 Ole wenu, kwa kuwa mwajenga maziara ya manabii, na baba zenu ndio waliowaua. 48 Basi, mwashuhudia na kuziridhia kazi za baba zenu; kwa kuwa wao waliwaua nanyi mwawajengea maziara. 49 Na kwa sababu hiyo hekima ya Mungu ilisema, Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na kuwafukuza, 50 ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kupigwa msingi wa ulimwengu; 51 ttangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu. Naam, nawaambieni ya kwamba itatakwa kwa kizazi hiki.
52 Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
53 Alipotoka humo, waandishi na Mafarisayo walianza kumsonga vibaya, na kumchokoza kwa maswali mengi, 54 twakimvizia, ili wapate neno litokalo kinywani mwake.
LUKE 11
Prayer
(Matthew 6.9-13; 7.7-11)
1 When Jesus had finished praying, one of his disciples said to him, “Lord, teach us to pray, just as John taught his followers to pray.”
2 So Jesus told them, “Pray in this way:
‘Father, help us
to honor your name.
Come and set up
your kingdom.
3 Give us each day
the food we need.t
4 Forgive our sins,
as we forgive everyone
who has done wrong to us.
And keep us
from being tempted.’ ”
5 Then Jesus went on to say:
Suppose one of you goes to a friend in the middle of the night and says, “Let me borrow three loaves of bread. 6 A friend of mine has dropped in, and I don't have a thing for him to eat.”
7 And suppose your friend answers, “Don't bother me! The door is bolted, and my children and I are in bed. I cannot get up to give you something.”
8 He may not get up and give you the bread, just because you are his friend. But he will get up and give you as much as you need, simply because you are not ashamed to keep on asking.
9 So I tell you to ask and you will receive, search and you will find, knock and the door will be opened for you. 10 Everyone who asks will receive, everyone who searches will find, and the door will be opened for everyone who knocks. 11 Which one of you fathers would give your hungry child a snake if the child asked for a fish? 12 Which one of you would give your child a scorpion if the child asked for an egg?
13 As bad as you are, you still know how to give good gifts to your children. But your heavenly Father is even more ready to give the Holy Spirit to anyone who asks.Jesus and the Ruler //of Demons
(Matthew 12.22-30; Mark 3.20-27)
14 Jesus forced a demon out of a man who could not talk. And after the demon had gone out, the man started speaking, and the crowds were amazed.
15 t But some people said, “He forces out demons by the power of Beelzebul, the ruler of the demons!”
16 t Others wanted to put Jesus to the test. So they asked him to show them a sign from God.
17 Jesus knew what they were thinking, and he said:
A kingdom where people fight each other will end up in ruin. And a family that fights will break up. 18 If Satan fights against himself, how can his kingdom last? Yet you say that I force out demons by the power of Beelzebul. 19 If I use his power to force out demons, whose power do your own followers use to force them out? They are the ones who will judge you.
20 But if I use God's power to force out demons, it proves that God's kingdom has already come to you.
21 When a strong man arms himself and guards his home, everything he owns is safe. 22 But if a stronger man comes and defeats him, he will carry off the weapons in which the strong man trusted. Then he will divide with others what he has taken.
23 t If you are not on my side, you are against me. If you don't gather in the crop with me, you scatter it.Return of an Evil Spirit
(Matthew 12.43-45)
24 When an evil spirit leaves a person, it travels through the desert, looking for a place to rest. But when it doesn't find a place, it says, “I will go back to the home I left.” 25 When it gets there and finds the place clean and fixed up,
26 it goes off and finds seven other evil spirits even worse than itself. They all come and make their home there, and that person ends up in worse shape than before.Being Really Blessed
27 While Jesus was still talking, a woman in the crowd spoke up, “The woman who gave birth to you and nursed you is blessed!”
28 Jesus replied, “That's true, but the people who are really blessed are the ones who hear and obey God's message!”tA Sign from God
(Matthew 12.38-42; Mark 8.12)
29 t As crowds were gathering around Jesus, he said:
You people of today are evil! You keep looking for a sign from God. But what happened to Jonaht is the only sign you will be given. 30 t Just as Jonah was a sign to the people of Nineveh, the Son of Man will be a sign to the people of today. 31 t When the judgment comes, the Queen of the Southt will stand there with you and condemn you. She traveled a long way to hear Solomon's wisdom, and yet here is something far greater than Solomon.
32 t The people of Nineveh will also stand there with you and condemn you. They turned to God when Jonah preached, and yet here is something far greater than Jonah.Light
(Matthew 5.15; 6.22,23)
33 t No one lights a lamp and then hides it or puts it under a clay pot. A lamp is put on a lampstand, so everyone who comes into the house can see the light. 34 Your eyes are the lamp for your body. When your eyes are good, you have all the light you need. But when your eyes are bad, everything is dark. 35 So be sure your light isn't darkness.
36 If you have light, and nothing is dark, then light will be everywhere, as when a lamp shines brightly on you.Jesus Condemns the Pharisees //and Teachers of the Law of Moses
(Matthew 23.1-36; Mark 12.38-40; Luke 20.45-47)
37 When Jesus finished speaking, a Pharisee invited him home for a meal. Jesus went and sat down to eat.t 38 The Pharisee was surprised that he did not wash his handst before eating.
39 So the Lord said to him:
You Pharisees clean the outside of cups and dishes, but on the inside you are greedy and evil. 40 You fools! Didn't God make both the outside and the inside?t
41 If you would only give what you have to the poor, everything you do would please God.
42 t You Pharisees are in for trouble! You give God a tenth of the spices from your gardens, such as mint and rue. But you cheat people, and you don't love God. You should be fair and kind to others and still give a tenth to God.
43 You Pharisees are in for trouble! You love the front seats in the synagogues, and you like to be greeted with honor in the market.
44 But you are in for trouble! You are like unmarked gravest that people walk on without even knowing it.
45 A teacher of the Law of Moses spoke up, “Teacher, you said cruel things about us.”
46 Jesus replied:
You teachers are also in for trouble! You load people down with heavy burdens, but you won't lift a finger to help them carry the loads. 47 Yes, you are really in for trouble. You build monuments to honor the prophets your own people murdered long ago.
48 You must think that was the right thing for your people to do, or else you would not have built monuments for the prophets they murdered.
49 Because of your evil deeds, the Wisdom of God said, “I will send prophets and apostles to you. But you will murder some and mistreat others.” 50 You people living today will be punished for all the prophets who have been murdered since the beginning of the world.
51 t This includes every prophet from the time of Abel to the time of Zechariah, t who was murdered between the altar and the temple. You people will certainly be punished for all of this.
52 You teachers of the Law of Moses are really in for trouble! You carry the keys to the door of knowledge about God. But you never go in, and you keep others from going in.
53 Jesus was about to leave, but the teachers and the Pharisees wanted to get even with him. They tried to make him say what he thought about other things, 54 so they could catch him saying something wrong.