LK. 14
Yesu Amponya Mtu mwenye Ugonjwa wa Safura
1 tIkawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. 2 Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura. 3 Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo? 4 Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake. 5 tAkawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?
6 Nao hawakuweza kujibu maneno haya.Unyenyekevu na Ukarimu
7 tAkawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, 8 tUkialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, 9 akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. 10 Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.
11 tKwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. 13 tBali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,
14 tnawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.Mfano wa Karamu Kuu
15 tBasi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu. 16 tAkamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, 17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. 18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. 19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20 tMwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. 21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. 22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.
24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.Gharama ya Uanafunzi
25 Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, 26 ttKama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27 tMtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? 29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, 30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. 31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? 32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Kuhusu Chumvi
34 tChumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee? 35 Haiifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
LUKE 14
Jesus Heals a Sick Man
1 One Sabbath, Jesus was having dinner in the home of an important Pharisee, and everyone was carefully watching Jesus. 2 All of a sudden a man with swollen legs stood up in front of him. 3 Jesus turned and asked the Pharisees and the teachers of the Law of Moses, “Is it right to heal on the Sabbath?”
4 But they did not say a word.
Jesus took hold of the man. Then he healed him and sent him away. 5 t Afterwards, Jesus asked the people, “If your son or ox falls into a well, wouldn't you pull him out at once, even on the Sabbath?”
6 There was nothing they could say.How To Be a Guest
7 Jesus saw how the guests had tried to take the best seats. So he told them:
8 t When you are invited to a wedding feast, don't sit in the best place. Someone more important may have been invited.
9 Then the one who invited you will come and say, “Give your place to this other guest!” You will be embarrassed and will have to sit in the worst place.
10 When you are invited to be a guest, go and sit in the worst place. Then the one who invited you may come and say, “My friend, take a better seat!” You will then be honored in front of all the other guests.
11 t If you put yourself above others, you will be put down. But if you humble yourself, you will be honored.
12 Then Jesus said to the man who had invited him:
When you give a dinner or a banquet, don't invite your friends and family and relatives and rich neighbors. If you do, they will invite you in return, and you will be paid back. 13 When you give a feast, invite the poor, the paralyzed, the lame, and the blind.
14 They cannot pay you back. But God will bless you and reward you when his people rise from death.The Great Banquet
(Matthew 22.1-10)
15 After Jesus had finished speaking, one of the guests said, “The greatest blessing of all is to be at the banquet in God's kingdom!”
16 Jesus told him:
A man once gave a great banquet and invited a lot of guests.
17 When the banquet was ready, he sent a servant to tell the guests, “Everything is ready! Please come.”
18 One guest after another started making excuses. The first one said, “I bought some land, and I've got to look it over. Please excuse me.”
19 Another guest said, “I bought five teams of oxen, and I need to try them out. Please excuse me.”
20 Still another guest said, “I've just now married, and I can't be there.”
21 The servant told his master what happened, and the master became so angry he said, “Go as fast as you can to every street and alley in town! Bring in everyone who is poor or paralyzed or blind or lame.”
22 When the servant returned, he said, “Master, I've done what you told me, and there is still plenty of room for more people.”
23 His master then told him, “Go out along the back roads and make people come in, so my house will be full.
24 Not one of the guests I first invited will get even a bite of my food!”Being a Disciple
(Matthew 10.37,38)
25 Large crowds were walking along with Jesus, when he turned and said:
26 t You cannot be my disciple, unless you love me more than you love your father and mother, your wife and children, and your brothers and sisters. You cannot follow me unless you love me more than you love your own life.
27 t You cannot be my disciple unless you carry your own cross and follow me.
28 Suppose one of you wants to build a tower. What is the first thing you will do? Won't you sit down and figure out how much it will cost and if you have enough money to pay for it? 29 Otherwise, you will start building the tower, but not be able to finish. Then everyone who sees what is happening will laugh at you.
30 They will say, “You started building, but could not finish the job.”
31 What will a king do if he has only 10,000 soldiers to defend himself against a king who is about to attack him with 20,000 soldiers? Before he goes out to battle, won't he first sit down and decide if he can win? 32 If he thinks he won't be able to defend himself, he will send messengers and ask for peace while the other king is still a long way off.
33 So then, you cannot be my disciple unless you give away everything you own.Salt and Light
(Matthew 5.13; Mark 9.50)
34 Salt is good, but if it no longer tastes like salt, how can it be made to taste salty again? 35 It is no longer good for the soil or even for the manure pile. People simply throw it out. If you have ears, pay attention!