LK. 18
Mfano wa Mjane na Hakimu
1 tAkawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. 2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. 3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. 4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, 5 tlakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?Mfano wa Farisayo na Mtoza Ushuru
9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. 10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. 11 tYule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. 12 tMimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. 13 tLakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 tNawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.Yesu Awabariki Watoto Wadogo
15 tWakamletea na watoto wachanga ili awaguse; lakini wanafunzi walipoona waliwakemea. 16 Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao.
17 tAmin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.Mtawala Tajiri
18 tTena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele? 19 Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu. 20 tWazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako. 21 Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu. 22 tYesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate. 23 Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi. 24 Yesu alipoona vile alisema, Kwa shida gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu! 25 Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 26 Nao waliosikia walisema, Ni nani basi awezaye kuokoka? 27 Akasema, Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu. 28 Petro akasema, Tazama, sisi tumeviacha vitu vyetu vyote na kukufuata. 29 Akawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu,
30 asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.Yesu Atabiri kuhusu Kufa na Kufufuka kwake kwa mara ya tatu
31 t tAkawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. 32 Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; 33 nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.
34 tWalakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.Yesu Amponya Mwombaji Kipofu
35 tIkawa alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka; 36 na alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, Kuna nini? 37 Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita. 38 Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu. 39 Basi wale waliotangulia wakamkemea ili anyamaze; lakini yeye alizidi sana kupaza sauti, Ee Mwana wa Daudi, unirehemu. 40 Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; na alipomkaribia, alimwuliza, 41 Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona. 42 tYesu akamwambia, Upewe kuona; imani yako imekuponya. 43 Mara hiyo akapata kuona, akamfuata, huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo walimsifu Mungu.
LUKE 18
A Widow and a Judge
1 Jesus told his disciples a story about how they should keep on praying and never give up:
2 In a town there was once a judge who didn't fear God or care about people.
3 In that same town there was a widow who kept going to the judge and saying, “Make sure that I get fair treatment in court.”
4 For a while the judge refused to do anything. Finally, he said to himself, “Even though I don't fear God or care about people,
5 I will help this widow because she keeps on bothering me. If I don't help her, she will wear me out.”
6 The Lord said:
Think about what that crooked judge said. 7 t Won't God protect his chosen ones who pray to him day and night? Won't he be concerned for them?
8 He will surely hurry and help them. But when the Son of Man comes, will he find on this earth anyone with faith?A Pharisee //and a Tax Collector
9 Jesus told a story to some people who thought they were better than others and who looked down on everyone else:
10 Two men went into the temple to pray.t One was a Pharisee and the other a tax collector.t 11 The Pharisee stood over by himself and prayed, t “God, I thank you that I am not greedy, dishonest, and unfaithful in marriage like other people. And I am really glad that I am not like that tax collector over there.
12 I go without eatingt for two days a week, and I give you one tenth of all I earn.”
13 t The tax collector stood off at a distance and did not think he was good enough even to look up toward heaven. He was so sorry for what he had done that he pounded his chest and prayed, “God, have pity on me! I am such a sinner.”
14 t Then Jesus said, “When the two men went home, it was the tax collector and not the Pharisee who was pleasing to God. If you put yourself above others, you will be put down. But if you humble yourself, you will be honored.”Jesus Blesses Little Children
(Matthew 19.13-15; Mark 10.13-16)
15 Some people brought their little children for Jesus to bless. But when his disciples saw them doing this, they told the people to stop bothering him. 16 So Jesus called the children over to him and said, “Let the children come to me! Don't try to stop them. People who are like these children belong to God's kingdom.t
17 You will never get into God's kingdom unless you enter it like a child!”A Rich and Important Man
(Matthew 19.16-30; Mark 10.17-31)
18 An important man asked Jesus, “Good Teacher, what must I do to have eternal life?”
19 Jesus said, “Why do you call me good? Only God is good.
20 t You know the commandments: ‘Be faithful in marriage. Do not murder. Do not steal. Do not tell lies about others. Respect your father and mother.’ ”
21 He told Jesus, “I have obeyed all these commandments since I was a young man.”
22 When Jesus heard this, he said, “There is one thing you still need to do. Go and sell everything you own! Give the money to the poor, and you will have riches in heaven. Then come and be my follower.”
23 When the man heard this, he was sad, because he was very rich.
24 Jesus saw how sad the man was. So he said, “It's terribly hard for rich people to get into God's kingdom!
25 In fact, it's easier for a camel to go through the eye of a needle than for a rich person to get into God's kingdom.”
26 When the crowd heard this, they asked, “How can anyone ever be saved?”
27 Jesus replied, “There are some things that people cannot do, but God can do anything.”
28 Peter said, “Remember, we left everything to be your followers!”
29 Jesus answered, “You can be sure that anyone who gives up home or wife or brothers or family or children because of God's kingdom
30 will be given much more in this life. And in the future world they will have eternal life.”Jesus Again Tells about //His Death
(Matthew 20.17-19; Mark 10.32-34)
31 Jesus took the twelve apostles aside and said:
We are now on our way to Jerusalem. Everything that the prophets wrote about the Son of Man will happen there. 32 He will be handed over to foreigners, t who will make fun of him, mistreat him, and spit on him.
33 They will beat him and kill him, but three days later he will rise to life.
34 The apostles did not understand what Jesus was talking about. They could not understand, because the meaning of what he said was hidden from them.Jesus Heals a Blind Beggar
(Matthew 20.29-34; Mark 10.46-52)
35 When Jesus was coming close to Jericho, a blind man sat begging beside the road. 36 The man heard the crowd walking by and asked what was happening. 37 Some people told him that Jesus from Nazareth was passing by. 38 So the blind man shouted, “Jesus, Son of David, t have pity on me!”
39 The people who were going along with Jesus told the man to be quiet. But he shouted even louder, “Son of David, have pity on me!”
40 Jesus stopped and told some people to bring the blind man over to him. When the blind man was getting near, Jesus asked,
41 “What do you want me to do for you?”
“Lord, I want to see!” he answered.
42 Jesus replied, “Look and you will see! Your eyes are healed because of your faith.” 43 At once the man could see, and he went with Jesus and started thanking God. When the crowds saw what happened, they praised God.