previous next

LK. 19

Yesu na Zakayo

1 Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. 2 Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. 3 Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. 4 Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. 5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. 7 tHata watu walipoona, walinung’unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. 8 tZakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang’anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. 9 tYesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.

10 tKwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Mfano wa Mafungu Kumi ya Fedha


11  t tWaliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara. 12 tBasi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. 13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. 14 tLakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. 15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17 tAkamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. 21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. 26 tNawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.

27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.

Yesu Aingia Yerusalemu kwa Shangwe


28 Na alipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
29  tIkawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi, 30 akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa. 31 Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji. 32 Na wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia. 33 Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda? 34 Wakasema, Bwana ana haja naye. 35 Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda, wakampandisha Yesu. 36 tNa alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani. 37 Hata alipokuwa amekaribia matelemko ya mlima wa Mizeituni, kundi zima la wanafunzi wake walianza kufurahi na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya matendo yote ya uwezo waliyoyaona, 38 twakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na utukufu huko juu. 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, uwakanye wanafunzi wako.

40 Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.

Yesu Aulilia Yerusalemu


41  tAlipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 takisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

44 twatakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.

Yesu Atakasa Hekalu


45  tAkaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,

46 takiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
47  tNaye akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza; 48 wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.

LUKE 19

Zacchaeus

1 Jesus was going through Jericho, 2 where a man named Zacchaeus lived. He was in charge of collecting taxest and was very rich.

3-4 Jesus was heading his way, and Zacchaeus wanted to see what he was like. But Zacchaeus was a short man and could not see over the crowd. So he ran ahead and climbed up into a sycamore tree.
5 When Jesus got there, he looked up and said, “Zacchaeus, hurry down! I want to stay with you today.”

6 Zacchaeus hurried down and gladly welcomed Jesus.

7 Everyone who saw this started grumbling, “This man Zacchaeus is a sinner! And Jesus is going home to eat with him.”

8 Later that day Zacchaeus stood up and said to the Lord, “I will give half of my property to the poor. And I will now pay back four times as mucht to everyone I have ever cheated.”
9 Jesus said to Zacchaeus, “Today you and your family have been saved, t because you are a true son of Abraham.t

10 t The Son of Man came to look for and to save people who are lost.”

A Story about Ten Servants

(Matthew 25.14-30)


11  t The crowd was still listening to Jesus as he was getting close to Jerusalem. Many of them thought that God's kingdom would soon appear,

12 and Jesus told them this story:
A prince once went to a foreign country to be crowned king and then to return.

13 But before leaving, he called in ten servants and gave each of them some money. He told them, “Use this to earn more money until I get back.”

14 But the people of his country hated him, and they sent messengers to the foreign country to say, “We don't want this man to be our king.”

15 After the prince had been made king, he returned and called in his servants. He asked them how much they had earned with the money they had been given.

16 The first servant came and said, “Sir, with the money you gave me I have earned ten times as much.”

17 “That's fine, my good servant!” the king said. “Since you have shown that you can be trusted with a small amount, you will be given ten cities to rule.”

18 The second one came and said, “Sir, with the money you gave me, I have earned five times as much.”

19 The king said, “You will be given five cities.”
20 Another servant came and said, “Sir, here is your money. I kept it safe in a handkerchief.

21 You are a hard man, and I was afraid of you. You take what isn't yours, and you harvest crops you didn't plant.”
22 “You worthless servant!” the king told him. “You have condemned yourself by what you have just said. You knew I am a hard man, taking what isn't mine and harvesting what I've not planted.

23 Why didn't you put my money in the bank? On my return, I could have had the money together with interest.”

24 Then he said to some other servants standing there, “Take the money away from him and give it to the servant who earned ten times as much.”

25 But they said, “Sir, he already has ten times as much!”
26  t The king replied, “Those who have something will be given more. But everything will be taken away from those who don't have anything.

27 Now bring me the enemies who didn't want me to be their king. Kill them while I watch!”

Jesus Enters Jerusalem

(Matthew 21.1-11; Mark 11.1-11; John 12.12-19)


28 When Jesus had finished saying all this, he went on toward Jerusalem. 29 As he was getting near Bethphage and Bethany on the Mount of Olives, he sent two of his disciples on ahead. 30 He told them, “Go into the next village, where you will find a young donkey that has never been ridden. Untie the donkey and bring it here.

31 If anyone asks why you are doing this, just say, ‘The Lordt needs it.’ ”
32 They went off and found everything just as Jesus had said.

33 While they were untying the donkey, its owners asked, “Why are you doing that?”

34 They answered, “The Lordt needs it.”
35 Then they led the donkey to Jesus. They put some of their clothes on its back and helped Jesus get on. 36 And as he rode along, the people spread clothes on the roadt in front of him. 37 When Jesus started down the Mount of Olives, his large crowd of disciples were happy and praised God because of all the miracles they had seen.

38 t They shouted,
“Blessed is the king who comes
in the name of the Lord!
Peace in heaven
and glory to God.”

39 Some Pharisees in the crowd said to Jesus, “Teacher, make your disciples stop shouting!”

40 But Jesus answered, “If they keep quiet, these stones will start shouting.”
41 When Jesus came closer and could see Jerusalem, he cried

42 and said:
It is too bad that today your people don't know what will bring them peace! Now it is hidden from them.
43 Jerusalem, the time will come when your enemies will build walls around you to attack you. Armies will surround you and close in on you from every side.

44 They will level you to the ground and kill your people. Not one stone in your buildings will be left on top of another. This will happen because you did not see that God had come to save you.t

Jesus in the Temple

(Matthew 21.12-17; Mark 11.15-19; John 2.13-22)


45 When Jesus entered the temple, he started chasing out the people who were selling things.

46 t He told them, “The Scriptures say, ‘My house should be a place of worship.’ But you have made it a place where robbers hide!”
47  t Each day, Jesus kept on teaching in the temple. So the chief priests, the teachers of the Law of Moses, and some other important people tried to have him killed. 48 But they could not find a way to do it, because everyone else was eager to listen to him.