previous next

LK. 2

Kuzaliwa kwa Yesu

1 Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. 2 Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. 3 Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. 4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; 5 tili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. 6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,

7 takamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Wachungaji na Malaika


8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. 9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. 10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; 11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. 12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.

13 tMara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,

14  tAtukuzwe Mungu juu mbinguni,
Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.
15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana. 16 Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini. 17 tWalipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. 18 Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. 19 tLakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.

20 Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.

Yesu Apewa Jina


21  tHata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.

Yesu Apelekwa Hekaluni


22  tKisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, 23 t(kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), 24 twakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili. 25 tNa tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29  tSasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako,
Kwa amani, kama ulivyosema;

30  tKwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32  tNuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa,
Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
33 Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. 34 tSimeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.

35 Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.
36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 tNaye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.

38 tHuyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.

Kurudi huko Nazareti


39  tBasi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

40 tYule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Kijana Yesu Hekaluni


41  tBasi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; 43 tna walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. 44 Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; 45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. 48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. 49 tAkawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? 50 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia.

51 tAkashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.
52  tNaye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

LUKE 2

The Birth of Jesus

(Matthew 1.18-25)

1 About that time Emperor Augustus gave orders for the names of all the people to be listed in record books.t

2 These first records were made when Quirinius was governor of Syria.t
3 Everyone had to go to their own hometown to be listed.

4 So Joseph had to leave Nazareth in Galilee and go to Bethlehem in Judea. Long ago Bethlehem had been King David's hometown, and Joseph went there because he was from David's family.
5 Mary was engaged to Joseph and traveled with him to Bethlehem. She was soon going to have a baby, 6 and while they were there,

7 she gave birth to her first-bornt son. She dressed him in baby clothest and laid him on a bed of hay, because there was no room for them in the inn.

The Shepherds


8 That night in the fields near Bethlehem some shepherds were guarding their sheep. 9 t All at once an angel came down to them from the Lord, and the brightness of the Lord's glory flashed around them. The shepherds were frightened. 10 But the angel said, “Don't be afraid! I have good news for you, which will make everyone happy. 11 This very day in King David's hometown a Savior was born for you. He is Christ the Lord.

12 You will know who he is, because you will find him dressed in baby clothes and lying on a bed of hay.”

13 Suddenly many other angels came down from heaven and joined in praising God. They said:

14 “Praise God in heaven!
Peace on earth to everyone
who pleases God.”
15 After the angels had left and gone back to heaven, the shepherds said to each other, “Let's go to Bethlehem and see what the Lord has told us about.”

16 They hurried off and found Mary and Joseph, and they saw the baby lying on a bed of hay.
17 When the shepherds saw Jesus, they told his parents what the angel had said about him. 18 Everyone listened and was surprised.

19 But Mary kept thinking about all this and wondering what it meant.

20 As the shepherds returned to their sheep, they were praising God and saying wonderful things about him. Everything they had seen and heard was just as the angel had said.

21  t Eight days later Jesus' parents did for him what the Law of Moses commands.t And they named him Jesus, just as the angel had told Mary when he promised she would have a baby.

Simeon Praises the Lord


22  t The time came for Mary and Joseph to do what the Law of Moses says a mother is supposed to do after her baby is born.t
They took Jesus to the temple in Jerusalem and presented him to the Lord,
23 t just as the Law of the Lord says, “Each first-bornt baby boy belongs to the Lord.”

24 The Law of the Lord also says parents have to offer a sacrifice, giving at least a pair of doves or two young pigeons. So that is what Mary and Joseph did.
25 At this time a man named Simeon was living in Jerusalem. Simeon was a good man. He loved God and was waiting for him to save the people of Israel. God's Spirit came to him

26 and told him that he would not die until he had seen Christ the Lord.
27 When Mary and Joseph brought Jesus to the temple to do what the Law of Moses says should be done for a new baby, the Spirit told Simeon to go into the temple.

28 Simeon took the baby Jesus in his arms and praised God,

29 “Lord, I am your servant,
and now I can die in peace,
because you have kept
your promise to me.

30 With my own eyes I have seen
what you have done
to save your people,

31 and foreign nations
will also see this.

32  t Your mighty power is a light
for all nations,
and it will bring honor
to your people Israel.”
33 Jesus' parents were surprised at what Simeon had said. 34 Then he blessed them and told Mary, “This child of yours will cause many people in Israel to fall and others to stand. The child will be like a warning sign. Many people will reject him,

35 and you, Mary, will suffer as though you had been stabbed by a dagger. But all this will show what people are really thinking.”

Anna Speaks about //the Child Jesus


36  t The prophet Anna was also there in the temple. She was the daughter of Phanuel from the tribe of Asher, and she was very old. In her youth she had been married for seven years, but her husband died.

37 And now she was 84 years old.t Night and day she served God in the temple by praying and often going without eating.t

38 At this time Anna came in and praised God. She spoke about the child Jesus to everyone who hoped for Jerusalem to be set free.

The Return to Nazareth


39  t After Joseph and Mary had done everything that the Law of the Lord commands, they returned home to Nazareth in Galilee.

40 The child Jesus grew. He became strong and wise, and God blessed him.

The Boy Jesus in the Temple


41  t Every year Jesus' parents went to Jerusalem for Passover. 42 And when Jesus was twelve years old, they all went there as usual for the celebration. 43 After Passover his parents left, but they did not know that Jesus had stayed on in the city. 44 They thought he was traveling with some other people, and they went a whole day before they started looking for him.

45 When they could not find him with their relatives and friends, they went back to Jerusalem and started looking for him there.
46 Three days later they found Jesus sitting in the temple, listening to the teachers and asking them questions.

47 Everyone who heard him was surprised at how much he knew and at the answers he gave.

48 When his parents found him, they were amazed. His mother said, “Son, why have you done this to us? Your father and I have been very worried, and we have been searching for you!”
49 Jesus answered, “Why did you have to look for me? Didn't you know that I would be in my Father's house?”t

50 But they did not understand what he meant.

51 Jesus went back to Nazareth with his parents and obeyed them. His mother kept on thinking about all that had happened.
52  t Jesus became wise, and he grew strong. God was pleased with him and so were the people.