previous next

LK. 20

Swali kuhusu Mamlaka ya Yesu

1  tIkawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula; 2 wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka hii? 3 Akajibu akawaambia, Nami nitawauliza ninyi neno moja; niambieni, 4 Ubatizo wa Yohana, je! Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? 5 Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini? 6 Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii. 7 Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka.

8 Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.

Mfano wa Wakodishaji Shamba Waovu


9  t tAkaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu. 10 tNa wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu. 11 Akatuma na mtumwa mwingine. Wakampiga huyu naye, wakamwaibisha wakamfukuza mikono mitupu. 12 Akamtuma na wa tatu; huyu naye wakamtia jeraha, wakamtupa nje. 13 Basi, bwana wa shamba la mizabibu alisema, Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu, mpendwa wangu; yamkini watamheshimu yeye. 14 Lakini, wale wakulima walipomwona, walishauriana wao kwa wao, wakisema, Huyu ndiye mrithi; haya, na tumwue, ili urithi uwe wetu. 15 Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi, bwana wa shamba la mizabibu atawatendeje? 16 Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Waliposikia hayo walisema, Hasha! Yasitukie haya!

17 tAkawakazia macho akasema, Maana yake nini basi neno hili lililoandikwa,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni?
18  tKila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; na ye yote ambaye litamwangukia litamsaga kabisa.

19 tNao waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta kumkamata saa iyo hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao.

Swali Kuhusu Kulipa Kodi


20  t tWakamvizia-vizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali. 21 Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. 22 Je! Ni halali tumpe Kaisari kodi, au sivyo? 23 Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia, 24 Nionyesheni dinari. Ina sura na anwani ya nani? Wakamjibu, Ya Kaisari. 25 Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu.

26 Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa.

Swali Kuhusu Ufunuo


27  t tKisha baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale wasemao ya kwamba hakuna ufufuo, wakamwuliza, 28 twakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao. 29 Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, akafa hana mtoto; 30 na wa pili [akamtwaa yule mke, akafa hana mtoto;] 31 hata wa tatu akamwoa, na kadhalika wote saba, wakafa, wasiache watoto. 32 Mwisho akafa yule mke naye. 33 Basi, katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba. 34 Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; 35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; 36 twala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo. 37 tLakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. 38 tNaye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake. 39 Waandishi wengine wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema;

40 wala hawakuthubutu kumwuliza neno baada ya hayo.

Swali kuhusu Wana wa Daudi


41  tAkawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi?

42 tMaana, Daudi mwenyewe asema katika chuo cha Zaburi,
Bwana alimwambia Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,

43 Hata niwaweke adui zako
Kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.

44 Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake?

Yesu Awakana Waandishi


45  t tNa watu wote walipokuwa wakimsikiliza, aliwaambia wanafunzi wake, 46 Jilindeni na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni. 47 Wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu.

LUKE 20

A Question //about Jesus' Authority

(Matthew 21.23-27; Mark 11.27-33)

1 One day, Jesus was teaching in the temple and telling the good news. So the chief priests, the teachers, and the nation's leaders

2 asked him, “What right do you have to do these things? Who gave you this authority?”
3 Jesus replied, “I want to ask you a question.

4 Who gave John the right to baptize? Was it God in heaven or merely some human being?”
5 They talked this over and said to each other, “We can't say God gave John this right. Jesus will ask us why we didn't believe John.

6 And we can't say it was merely some human who gave John the right to baptize. The crowd will stone us to death, because they think John was a prophet.”

7 So they told Jesus, “We don't know who gave John the right to baptize.”

8 Jesus replied, “Then I won't tell you who gave me the right to do what I do.”

Renters of a Vineyard

(Matthew 21.33-46; Mark 12.1-12)


9  t Jesus told the people this story:
A man once planted a vineyard and rented it out. Then he left the country for a long time.
10 When it was time to harvest the crop, he sent a servant to ask the renters for his share of the grapes. But they beat up the servant and sent him away without anything. 11 So the owner sent another servant. The renters also beat him up. They insulted him terribly and sent him away without a thing.

12 The owner sent a third servant. He was also beaten terribly and thrown out of the vineyard.

13 The owner then said to himself, “What am I going to do? I know what. I'll send my son, the one I love so much. They will surely respect him!”
14 When the renters saw the owner's son, they said to one another, “Someday he will own the vineyard. Let's kill him! Then we can have it all for ourselves.”

15 So they threw him out of the vineyard and killed him.
Jesus asked, “What do you think the owner of the vineyard will do?

16 I'll tell you what. He will come and kill those renters and let someone else have his vineyard.”
When the people heard this, they said, “This must never happen!”
17  t But Jesus looked straight at them and said, “Then what do the Scriptures mean when they say, ‘The stone the builders tossed aside is now the most important stone of all’?

18 Anyone who stumbles over this stone will get hurt, and anyone it falls on will be smashed to pieces.”

19 The chief priests and the teachers of the Law of Moses knew that Jesus was talking about them when he was telling this story. They wanted to arrest him right then, but they were afraid of the people.

Paying Taxes

(Matthew 22.15-22; Mark 12.13-17)


20 Jesus' enemies kept watching him closely, because they wanted to hand him over to the Roman governor. So they sent some men who pretended to be good. But they were really spies trying to catch Jesus saying something wrong. 21 The spies said to him, “Teacher, we know you teach the truth about what God wants people to do. And you treat everyone with the same respect, no matter who they are.

22 Tell us, should we pay taxes to the Emperor or not?”
23 Jesus knew they were trying to trick him. So he told them,

24 “Show me a coin.” Then he asked, “Whose picture and name are on it?”
“The Emperor's,” they answered.
25 Then he told them, “Give the Emperor what belongs to him and give God what belongs to God.”

26 Jesus' enemies could not catch him saying anything wrong there in front of the people. They were amazed at his answer and kept quiet.

Life in the Future World

(Matthew 22.23-33; Mark 12.18-27)


27  t The Sadducees did not believe that people would rise to life after death. So some of them came to Jesus

28 t and said:
Teacher, Moses wrote that if a married man dies and has no children, his brother should marry the widow. Their first son would then be thought of as the son of the dead brother.
29 There were once seven brothers. The first one married, but died without having any children. 30 The second one married his brother's widow, and he also died without having any children. 31 The same thing happened to the third one. Finally, all seven brothers married this woman and died without having any children. 32 At last the woman died.

33 When God raises people from death, whose wife will this woman be? All seven brothers had married her.

34 Jesus answered:
The people in this world get married.
35 But in the future world no one who is worthy to rise from death will either marry

36 or die. They will be like the angels and will be God's children, because they have been raised to life.
37  t In the story about the burning bush, Moses clearly shows that people will live again. He said, “The Lord is the God worshiped by Abraham, Isaac, and Jacob.”t

38 So the Lord isn't the God of the dead, but of the living. This means that everyone is alive as far as God is concerned.
39 Some of the teachers of the Law of Moses said, “Teacher, you have given a good answer!”

40 From then on, no one dared to ask Jesus any questions.

About David's Son

(Matthew 22.41-46; Mark 12.35-37)


41 Jesus asked, “Why do people say that the Messiah will be the son of King David?t

42 t In the book of Psalms, David himself says,
‘The Lord said to my Lord,
Sit at my right sidet

43 until I make your enemies
into a footstool for you.’

44 David spoke of the Messiah as his Lord, so how can the Messiah be his son?”

Jesus and the Teachers //of the Law of Moses

(Matthew 23.1-36; Mark 12.38-40; Luke 11.37-54)


45 While everyone was listening to Jesus, he said to his disciples:
46 Guard against the teachers of the Law of Moses! They love to walk around in long robes, and they like to be greeted in the market. They want the front seats in the synagogues and the best seats at banquets. 47 But they cheat widows out of their homes and then pray long prayers just to show off. These teachers will be punished most of all.