Luka 21
Sadaka ya mama mjane
(Marko 12:41-44)
1 Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya hekalu, 2 akamwona pia mama mmoja mjane akitumbukiza humo sarafu mbili ndogo. 3 Basi, akasema, “Nawaambieni kweli, mama huyu mjane maskini ametia katika hazina kiasi kikubwa kuliko walichotia wote. 4 Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Yesu anatabiri kuharibiwa kwa hekalu
(Mat 24:1-2; Marko 13:1-2)
5 Baadhi ya wanafunzi walikuwa wanazungumza juu ya hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe ya thamani, pamoja na sadaka zilizotolewa kwa Mungu. Yesu akasema, 6 “Haya yote mnayoyaona – zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
Taabu na mateso
(Mat 24:3-14; Marko 13:3-13)
7 Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”
8 Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate! 9 Basi, mtakaposikia habari za vita na misukosuko, msitishike; maana ni lazima hayo yatokee kwanza, lakini mwisho wa yote, bado.”
10 Halafu akaendelea kusema: “Taifa moja litapigana na taifa lingine, na ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. 11 Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani. 12 Lakini kabla ya kutokea hayo yote, watawatieni nguvuni, watawatesa na kuwapelekeni katika masunagogi na kuwatia gerezani; mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu, 13 mpate kunishuhudia kwao. 14 Muwe na msimamo huu mioyoni mwenu: Hakuna kufikiria kabla ya wakati juu ya jinsi mtakavyojitetea, 15 kwa sababu mimi mwenyewe nitawapeni ufasaha wa maneno na hekima, hata maadui zenu hawataweza kustahimili wala kupinga. 16 Wazazi wenu, ndugu, jamaa na rafiki zenu watawasaliti nyinyi; na baadhi yenu mtauawa. 17 Watu wote watawachukieni nyinyi kwa sababu ya jina langu. 18 Lakini, hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea. 19 Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.
Yesu anatabiri kuharibiwa kwa mji wa Yerusalemu
(Mat 24:15-21; Marko 13:14-19)
20 “Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi jueni ya kwamba wakati umefika ambapo mji huo utaharibiwa. 21 Hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini. 22 Kwa maana siku hizo ni siku za adhabu, ili yote yaliyoandikwa yatimie. 23 Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa. 24 Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
Kuja kwake Mwana wa Mtu
(Mat 24:29-31; Marko 13:24-27)
25 “Kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota. Mataifa duniani yatakuwa na dhiki kwa sababu ya wasiwasi kutokana na mshindo wa mawimbi ya bahari. 26 Watu watazirai kwa sababu ya woga, wakitazamia mambo yatakayoupata ulimwengu; kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa. 27 Halafu, watamwona Mwana wa Mtu akija katika wingu, mwenye nguvu na utukufu mwingi. 28 Wakati mambo hayo yatakapoanza kutukia, simameni na kuinua vichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia.”
Mfano wa mtini
(Mat 24:32-35; Marko 13:28-31)
29 Kisha akawaambia mfano: “Angalieni mtini na miti mingine yote. 30 Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba majira ya mavuno yamekaribia. 31 Vivyo hivyo, mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba ufalme wa Mungu umekaribia. 32 Kweli nawaambieni, kizazi hiki cha sasa hakitapita kabla ya hayo yote kutendeka. 33 Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Lazima kuwa macho
34 “Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla. 35 Kwa maana itawajia kama mtego wote wanaoishi duniani pote. 36 Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu.”
37 Wakati wa mchana, siku hizo, Yesu alikuwa akifundisha watu hekaluni; lakini usiku alikuwa akienda katika mlima wa Mizeituni na kukaa huko. 38 Watu wote walikuwa wanakwenda hekaluni asubuhi na mapema, wapate kumsikiliza.
Luke 21
1 And he looked up, and saw the rich men that were casting their gifts into the treasury.2 And he saw a certain poor widow casting in thither two mites.3 And he said, Of a truth I say unto you, This poor widow cast in more than they all:4 for all these did of their superfluity cast in unto the gifts; but she of her want did cast in all the living that she had.5 And as some spake of the temple, how it was adorned with goodly stones and offerings, he said,6 As for these things which ye behold, the days will come, in which there shall not be left here one stone upon another, that shall not be thrown down.7 And they asked him, saying, Teacher, when therefore shall these things be? and what shall be the sign when these things are about to come to pass?8 And he said, Take heed that ye be not led astray: for many shall come in my name, saying, I am he; and, The time is at hand: go ye not after them.9 And when ye shall hear of wars and tumults, be not terrified: for these things must needs come to pass first; but the end is not immediately.10 Then said he unto them, Nation shall rise against nation, and kingdom against kingdom;11 and there shall be great earthquakes, and in divers places famines and pestilences; and there shall be terrors and great signs from heaven.12 But before all these things, they shall lay their hands on you, and shall persecute you, delivering you up to the synagogues and prisons, bringing you before kings and governors for my name’s sake.13 It shall turn out unto you for a testimony.14 Settle it therefore in your hearts, not to meditate beforehand how to answer:15 for I will give you a mouth and wisdom, which all your adversaries shall not be able to withstand or to gainsay.16 But ye shall be delivered up even by parents, and brethren, and kinsfolk, and friends; and some of you shall they cause to be put to death.17 And ye shall be hated of all men for my name’s sake.18 And not a hair of your head shall perish.19 In your patience ye shall win your souls.20 But when ye see Jerusalem compassed with armies, then know that her desolation is at hand.21 Then let them that are in Judaea flee unto the mountains; and let them that are in the midst of her depart out; and let not them that are in the country enter therein.22 For these are days of vengeance, that all things which are written may be fulfilled.23 Woe unto them that are with child and to them that give suck in those days! for there shall be great distress upon the land, and wrath unto this people.24 And they shall fall by the edge of the sword, and shall be led captive into all the nations: and Jerusalem shall be trodden down of the Gentiles, until the times of the Gentiles be fulfilled.25 And there shall be signs in sun and moon and stars; and upon the earth distress of nations, in perplexity for the roaring of the sea and the billows;26 men fainting for fear, and for expectation of the things which are coming on the world: for the powers of the heavens shall be shaken.27 And then shall they see the Son of man coming in a cloud with power and great glory.28 But when these things begin to come to pass, look up, and lift up your heads; because your redemption draweth nigh.29 And he spake to them a parable: Behold the fig tree, and all the trees:30 when they now shoot forth, ye see it and know of your own selves that the summer is now nigh.31 Even so ye also, when ye see these things coming to pass, know ye that the kingdom of God is nigh.32 Verily I say unto you, This generation shall not pass away, till all things be accomplished.33 Heaven and earth shall pass away: but my words shall not pass away.34 But take heed to yourselves, lest haply your hearts be overcharged with surfeiting, and drunkenness, and cares of this life, and that day come on you suddenly as a snare:35 for so shall it come upon all them that dwell on the face of all the earth.36 But watch ye at every season, making supplication, that ye may prevail to escape all these things that shall come to pass, and to stand before the Son of man.37 And every day he was teaching in the temple; and every night he went out, and lodged in the mount that is called Olivet.38 And all the people came early in the morning to him in the temple, to hear him.