LK. 21
Sadaka ya Mjane
1 tAkainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. 2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. 3 tAkasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;
4 maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.Kuangamizwa kwa Hekalu Kwatabiriwa
5 tNa watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema,
6 tHaya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.Ishara na Mateso
7 Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia? 8 tAkasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.
9 tNanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.
10 tKisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; 11 kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni. 12 tLakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu. 13 Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu. 14 ttBasi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu; 15 tkwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga. 16 Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu. 17 tNanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. 18 tWalakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.
19 tNanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.Unabii wa kuangamizwa kwa Yerusalemu
20 Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. 21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. 22 tKwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. 23 tOle wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 tWataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.Kuja kwa Mwana wa Mtu
25 t tTena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; 26 twatu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. 27 tHapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
28 tBasi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.Funzo la Mtini
29 tAkawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. 31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. 32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.
33 tMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.Himizo za kuwa Waangalifu
34 tBasi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 tkwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 tBasi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
37 tBasi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni. 38 Na watu wote walikuwa wakiamka mapema waende hekaluni ili kumsikiliza.
LUKE 21
A Widow's Offering
(Mark 12.41-44)
1 Jesus looked up and saw some rich people tossing their gifts into the offering box. 2 He also saw a poor widow putting in a few cents. 3 And he said, “I tell you that this poor woman has put in more than all the others.
4 Everyone else gave what they didn't need. But she is very poor and gave everything she had.”The Temple Will Be Destroyed
(Matthew 24.1,2; Mark 13.1,2)
5 Some people were talking about the beautiful stones used to build the temple and about the gifts that had been placed in it. Jesus said,
6 “Do you see these stones? The time is coming when not one of them will be left in place. They will all be knocked down.”Warning about Trouble
(Matthew 24.3-14; Mark 13.3-13)
7 t Some people asked, “Teacher, when will all this happen? How can we know when these things are about to take place?”
8 Jesus replied:
Don't be fooled by those who will come and claim to be me. They will say, “I am Christ!” and “Now is the time!” But don't follow them.
9 When you hear about wars and riots, don't be afraid. These things will have to happen first, but this isn't the end.
10 Nations will go to war against one another, and kingdoms will attack each other.
11 There will be great earthquakes, and in many places people will starve to death and suffer terrible diseases. All sorts of frightening things will be seen in the sky.
12 Before all this happens, you will be arrested and punished. You will be tried in your synagogues and put in jail. Because of me you will be placed on trial before kings and governors.
13 But this will be your chance to tell about your faith.
14 t Don't worry about what you will say to defend yourselves. 15 I will give you the wisdom to know what to say. None of your enemies will be able to oppose you or to say that you are wrong. 16 You will be betrayed by your own parents, brothers, family, and friends. Some of you will even be killed. 17 Because of me, you will be hated by everyone. 18 But don't worry!t
19 You will be saved by being faithful to me.Jerusalem Will Be Destroyed
(Matthew 24.15-21; Mark 13.14-19)
20 When you see Jerusalem surrounded by soldiers, you will know that it will soon be destroyed. 21 If you are living in Judea at this time, run to the mountains. If you are in the city, leave it. And if you are out in the country, don't go back into the city. 22 t This time of punishment is what is written about in the Scriptures. 23 It will be an awful time for women who are expecting babies or nursing young children! Everywhere in the land people will suffer horribly and be punished.
24 Some of them will be killed by swords. Others will be carried off to foreign countries. Jerusalem will be overrun by foreign nations until their time comes to an end.When the Son of Man Appears
(Matthew 24.29-31; Mark 13.24-27)
25 t Strange things will happen to the sun, moon, and stars. The nations on earth will be afraid of the roaring sea and tides, and they won't know what to do. 26 People will be so frightened that they will faint because of what is happening to the world. Every power in the sky will be shaken.t 27 t Then the Son of Man will be seen, coming in a cloud with power and great glory.
28 When all of this starts happening, stand up straight and be brave. You will soon be set free.A Lesson from a Fig Tree
(Matthew 24.32-35; Mark 13.28-31)
29 Then Jesus told them a story:
When you see a fig tree or any other tree 30 putting out leaves, you know that summer will soon come. 31 So, when you see these things happening, you know that God's kingdom will soon be here. 32 You can be sure that some of the people of this generation will still be alive when all of this takes place.
33 The sky and the earth won't last forever, but my words will.A Warning
34 Don't spend all of your time thinking about eating or drinking or worrying about life. If you do, the final day will suddenly catch you 35 like a trap. This day will surprise everyone on earth.
36 Watch out and keep praying that you can escape all that is going to happen and that the Son of Man will be pleased with you.
37 t Jesus taught in the temple each day, and he spent each night on the Mount of Olives. 38 Everyone got up early and came to the temple to hear him teach.