LK. 22
Mpango wa Kumwua Yesu
1 tIkakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka.
2 tNa wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu.
3 t tShetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. 5 Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha.
6 Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.Maandalizi ya Pasaka
7 t tIkafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka. 8 Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila. 9 Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? 10 Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. 11 Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? 12 Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo.
13 tWakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka.Kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana
14 Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 15 Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16 tkwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. 17 Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; 18 Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. 19 tAkatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20 tKikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.] 21 tWalakini, tazama, mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani, 22 Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye!
23 Wakaanza kuulizana wao kwa wao, ni yupi miongoni mwao atakayelitenda jambo hilo.Mashindano kuhusu Ukubwa
24 tYakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa. 25 tAkawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa Wenye fadhili; 26 tlakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. 27 tMaana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye. 28 Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. 29 tNami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi;
30 tmpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.Yesu Atabiri kuhusu Petro Kumkana
31 t tAkasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; 32 tlakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. 33 Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.
34 Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.Mfuko, Mkoba, na Upanga
35 tAkawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La! 36 Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho yake akanunue. 37 tKwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake.
38 Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi.Yesu Aomba katika Mlima wa Mizeituni
39 t tAkatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.
40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. 41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, 42 takisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [ 43 tMalaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. 44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.] 45 Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.
46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.Kusalitiwa na Kukamatwa kwa Yesu
47 tBasi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. 48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? 49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga? 50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. 51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya. 52 tYesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang’anyi?
53 tKila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.Petro Amkana Yesu
54 tWakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali. 55 Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye Petro akaketi kati yao. 56 Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye. 57 Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. 58 Baadaye kitambo mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi. 59 Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya. 60 Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika. 61 tBwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.
62 Akatoka nje akalia kwa majonzi.Kumdhihaki na Kumpiga Yesu
63 tNa wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. 64 Wakamfunika macho, kisha wakamwuliza-uliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga?
65 Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana.Yesu Mbele ya Baraza
66 tHata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema, 67 tKama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa. 68 Tena, nikiwauliza, hamtajibu. 69 tLakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi. 70 Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. 71 Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
LUKE 22
A Plot To Kill Jesus
(Matthew 26.1-5,14,16; Mark 14.1,2,10,11; John 11.45-53)
1 t The Festival of Thin Bread, also called Passover, was near. 2 The chief priests and the teachers of the Law of Moses were looking for a way to get rid of Jesus, because they were afraid of what the people might do.
3 Then Satan entered the heart of Judas Iscariot, t who was one of the twelve apostles.
4 Judas went to talk with the chief priests and the officers of the temple police about how he could help them arrest Jesus. 5 They were very pleased and offered to pay Judas some money.
6 He agreed and started looking for a good chance to betray Jesus when the crowds were not around.Jesus Eats with His Disciples
(Matthew 26.17-25; Mark 14.12-21; John 13.21-30)
7 The day had come for the Festival of Thin Bread, and it was time to kill the Passover lambs.
8 So Jesus said to Peter and John, “Go and prepare the Passover meal for us to eat.”
9 But they asked, “Where do you want us to prepare it?”
10 Jesus told them, “As you go into the city, you will meet a man carrying a jar of water.t Follow him into the house 11 and say to the owner, ‘Our teacher wants to know where he can eat the Passover meal with his disciples.’
12 The owner will take you upstairs and show you a large room ready for you to use. Prepare the meal there.”
13 Peter and John left. They found everything just as Jesus had told them, and they prepared the Passover meal.The Lord's Supper
(Matthew 26.26-30; Mark 14.22-26; 1 Corinthians 11.23-25)
14 When the time came for Jesus and the apostles to eat, 15 he said to them, “I have very much wanted to eat this Passover meal with you before I suffer.
16 I tell you I will not eat another Passover meal until it is finally eaten in God's kingdom.”
17 Jesus took a cup of wine in his hands and gave thanks to God. Then he told the apostles, “Take this wine and share it with each other.
18 I tell you that I will not drink any more wine until God's kingdom comes.”
19 Jesus took some bread in his hands and gave thanks for it. He broke the bread and handed it to his apostles. Then he said, “This is my body, which is given for you. Eat this as a way of remembering me!”
20 t After the meal he took another cup of wine in his hands. Then he said, “This is my blood. It is poured out for you, and with it God makes his new agreement. 21 t The one who will betray me is here at the table with me!
22 The Son of Man will die in the way that has been decided for him, but it will be terrible for the one who betrays him!”
23 Then the apostles started arguing about who would ever do such a thing.An Argument about Greatness
24 t The apostles got into an argument about which one of them was the greatest.
25 t So Jesus told them:
Foreign kings order their people around, and powerful rulers call themselves everyone's friends.t 26 t But don't be like them. The most important one of you should be like the least important, and your leader should be like a servant.
27 t Who do people think is the greatest, a person who is served or one who serves? Isn't it the one who is served? But I have been with you as a servant.
28 You have stayed with me in all my troubles. 29 So I will give you the right to rule as kings, just as my Father has given me the right to rule as a king.
30 t You will eat and drink with me in my kingdom, and you will each sit on a throne to judge the twelve tribes of Israel.Jesus' Disciples //Will Be Tested
(Matthew 26.31-35; Mark 14.27-31; John 13.36-38)
31 Jesus said, “Simon, listen to me! Satan has demanded the right to test each one of you, as a farmer does when he separates wheat from the husks.t
32 But Simon, I have prayed that your faith will be strong. And when you have come back to me, help the others.”
33 Peter said, “Lord, I am ready to go with you to jail and even to die with you.”
34 Jesus replied, “Peter, I tell you that before a rooster crows tomorrow morning, you will say three times that you don't know me.”Moneybags, Traveling Bags, //and Swords
35 t Jesus asked his disciples, “When I sent you out without a moneybag or a traveling bag or sandals, did you need anything?”
“No!” they answered.
36 Jesus told them, “But now, if you have a moneybag, take it with you. Also take a traveling bag, and if you don't have a sword, t sell some of your clothes and buy one.
37 t Do this because the Scriptures say, ‘He was considered a criminal.’ This was written about me, and it will soon come true.”
38 The disciples said, “Lord, here are two swords!”
“Enough of that!” Jesus replied.Jesus Prays
(Matthew 26.36-46; Mark 14.32-42)
39 Jesus went out to the Mount of Olives, as he often did, and his disciples went with him.
40 When they got there, he told them, “Pray that you won't be tested.”
41 Jesus walked on a little way before he knelt down and prayed,
42 “Father, if you will, please don't make me suffer by drinking from this cup.t But do what you want, and not what I want.”
43 Then an angel from heaven came to help him.
44 Jesus was in great pain and prayed so sincerely that his sweat fell to the ground like drops of blood.t
45 Jesus got up from praying and went over to his disciples. They were asleep and worn out from being so sad.
46 He said to them, “Why are you asleep? Wake up and pray that you won't be tested.”Jesus Is Arrested
(Matthew 26.47-56; Mark 14.43-50; John 18.3-11)
47 While Jesus was still speaking, a crowd came up. It was led by Judas, one of the twelve apostles. He went over to Jesus and greeted him with a kiss.t
48 Jesus asked Judas, “Are you betraying the Son of Man with a kiss?”
49 When Jesus' disciples saw what was about to happen, they asked, “Lord, should we attack them with a sword?”
50 One of the disciples even struck at the high priest's servant with his sword and cut off the servant's right ear.
51 “Enough of that!” Jesus said. Then he touched the servant's ear and healed it.
52 Jesus spoke to the chief priests, the temple police, and the leaders who had come to arrest him. He said, “Why do you come out with swords and clubs and treat me like a criminal?
53 t I was with you every day in the temple, and you didn't arrest me. But this is your time, and darknesst is in control.”Peter Says //He Doesn't Know Jesus
(Matthew 26.57,58,67-75; Mark 14.53,54,66-72; John 18.12-18,25-27)
54 Jesus was arrested and led away to the house of the high priest, while Peter followed at a distance. 55 Some people built a fire in the middle of the courtyard and were sitting around it. Peter sat there with them,
56 and a servant girl saw him. Then after she had looked at him carefully, she said, “This man was with Jesus!”
57 Peter said, “Woman, I don't even know that man!”
58 A little later someone else saw Peter and said, “You are one of them!”
“No, I'm not!” Peter replied.
59 About an hour later another man insisted, “This man must have been with Jesus. They both come from Galilee.”
60 Peter replied, “I don't know what you are talking about!” Right then, while Peter was still speaking, a rooster crowed.
61 The Lord turned and looked at Peter. And Peter remembered that the Lord had said, “Before a rooster crows tomorrow morning, you will say three times that you don't know me.”
62 Then Peter went out and cried bitterly.
63 The men who were guarding Jesus made fun of him and beat him. 64 They put a blindfold on him and said, “Tell us who struck you!”
65 They kept on insulting Jesus in many other ways.Jesus Is Questioned //by the Council
(Matthew 26.59-66; Mark 14.55-64; John 18.19-24)
66 At daybreak the nation's leaders, the chief priests, and the teachers of the Law of Moses got together and brought Jesus before their council.
67 They said, “Tell us! Are you the Messiah?”
Jesus replied, “If I said so, you wouldn't believe me. 68 And if I asked you a question, you wouldn't answer.
69 But from now on, the Son of Man will be seated at the right side of God All-Powerful.”
70 Then they asked, “Are you the Son of God?”t
Jesus answered, “You say I am!”t
71 They replied, “Why do we need more witnesses? He said it himself!”