previous next

LK. 8

Baadhi ya Wanawake Waandamana na Yesu

1  tIkawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, 2 tna wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,

3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.

Mfano wa Mpanzi


4  tMkutano mkuu ulipokutanika, na wale waliotoka kila mji wakimjia, alisema kwa mfano; 5 Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. 6 Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. 7 Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga.

8 Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
9 Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo?

10 tAkasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.

Mfano wa Mpanzi


11  tNa huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. 12 tWale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka. 13 Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. 14 Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.

15 tNa zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.

Taa chini ya Mtungi


16  t tHakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake. 17 tKwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi.

18 tJiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.

Jamaa wa Kweli wa Yesu


19  tWakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. 20 Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.

21 Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.
22  tIkawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. 23 Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. 24 Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.

25 Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?

Yesu Amponya Mgerasi Mwenye pepo


26  tWakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. 27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. 28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. 29 Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. 30 Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. 31 Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. 32 Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa. 33 Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji. 34 Wachungaji walipoona lililotokea walikimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. 35 Watu wakatoka kwenda kuliona lililotokea, wakamwendea Yesu, wakamwona mtu yule aliyetokwa na pepo ameketi miguuni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake; wakaogopa. 36 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza jinsi alivyoponywa yule aliyepagawa na pepo. 37 Na jamii ya watu wa nchi ya Wagerasi iliyo kando kando walimwomba aondoke kwao, kwa kuwa walishikwa na hofu nyingi; basi akapanda chomboni, akarudi. 38 Na mtu yule aliyetokwa na pepo alimwomba ruhusa afuatane naye; lakini yeye alimwaga akisema,

39 Rudi nyumbani kwako, ukahubiri yalivyo makuu Mungu aliyokutendea. Akaenda zake, akihubiri katika mji wote, yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu.

Msichana Afufuliwa na Mwanamke Kuponywa


40  tBasi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote. 41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;

42 tkwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. 45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. 46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka. 47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.

48 tAkamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.
49 Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu. 50 Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa. 51 Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye. 52 tNa watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu. 53 Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa. 54 Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka. 55 Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula. 56 tWazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia.

LUKE 8

Women Who Helped Jesus

1 Soon after this, Jesus was going through towns and villages, telling the good news about God's kingdom. His twelve apostles were with him, 2 t and so were some women who had been healed of evil spirits and all sorts of diseases. One of the women was Mary Magdalene, t who once had seven demons in her.

3 Joanna, Susanna, and many others had also used what they owned to help Jesust and his disciples. Joanna's husband Chuza was one of Herod's officials.t

A Story about a Farmer

(Matthew 13.1-9; Mark 4.1-9)


4 When a large crowd from several towns had gathered around Jesus, he told them this story:
5 A farmer went out to scatter seed in a field. While the farmer was doing this, some of the seeds fell along the road and were stepped on or eaten by birds. 6 Other seeds fell on rocky ground and started growing. But the plants did not have enough water and soon dried up. 7 Some other seeds fell where thornbushes grew up and choked the plants.

8 The rest of the seeds fell on good ground where they grew and produced a hundred times as many seeds.
When Jesus had finished speaking, he said, “If you have ears, pay attention!”

Why Jesus Used Stories

(Matthew 13.10-17; Mark 4.10-12)


9 Jesus' disciples asked him what the story meant.

10 t So he answered:
I have explained the secrets about God's kingdom to you. But for others I use stories, so they will look, but not see, and they will hear, but not understand.

Jesus Explains the Story //about a Farmer

(Matthew 13.18-23; Mark 4.13-20)


11 This is what the story means: The seed is God's message, 12 and the seeds that fell along the road are the people who hear the message. But the devil comes and snatches the message out of their hearts, so they will not believe and be saved.

13 The seeds that fell on rocky ground are the people who gladly hear the message and accept it. But they don't have deep roots, and they believe only for a little while. As soon as life gets hard, they give up.
14 The seeds that fell among the thornbushes are also people who hear the message. But they are so eager for riches and pleasures that they never produce anything.

15 Those seeds that fell on good ground are the people who listen to the message and keep it in good and honest hearts. They last and produce a harvest.

Light

(Mark 4.21-25)


16  t No one lights a lamp and puts it under a bowl or under a bed. A lamp is always put on a lampstand, so people who come into a house will see the light. 17 t There is nothing hidden that will not be found. There is no secret that will not be well known.

18 t Pay attention to how you listen! Everyone who has something will be given more, but people who have nothing will lose what little they think they have.

Jesus' Mother and Brothers

(Matthew 12.46-50; Mark 3.31-35)


19 Jesus' mother and brothers went to see him, but because of the crowd they could not get near him.

20 Someone told Jesus, “Your mother and brothers are standing outside and want to see you.”

21 Jesus answered, “My mother and my brothers are those people who hear and obey God's message.”

A Storm

(Matthew 8.23-27; Mark 4.35-41)


22 One day, Jesus and his disciples got into a boat, and he said, “Let's cross the lake.”t They started out,

23 and while they were sailing across, he went to sleep.
Suddenly a storm struck the lake, and the boat started sinking. They were in danger.

24 So they went to Jesus and woke him up, “Master, Master! We are about to drown!”
Jesus got up and ordered the wind and waves to stop. They obeyed, and everything was calm.

25 Then Jesus asked the disciples, “Don't you have any faith?”
But they were frightened and amazed. They said to each other, “Who is this? He can give orders to the wind and the waves, and they obey him!”

A Man with Demons in Him

(Matthew 8.28-34; Mark 5.1-20)


26 Jesus and his disciples sailed across Lake Galilee and came to shore near the town of Gerasa.t

27 As Jesus was getting out of the boat, he was met by a man from this town. The man had demons in him. He had gone naked for a long time and no longer lived in a house, but in the graveyard.t
28 The man saw Jesus and screamed. He knelt down in front of him and shouted, “Jesus, Son of God Most High, what do you want with me? I beg you not to torture me!”

29 He said this because Jesus had already told the evil spirit to go out of him.
The man had often been attacked by the demon. And even though he had been bound with chains and leg irons and kept under guard, he smashed whatever bound him. Then the demon would force him out into lonely places.

30 Jesus asked the man, “What is your name?”
He answered, “My name is Lots.” He said this because there were “lots” of demons in him.

31 They begged Jesus not to send them to the deep pit, t where they would be punished.
32 A large herd of pigs was feeding there on the hillside. So the demons begged Jesus to let them go into the pigs, and Jesus let them go.

33 Then the demons left the man and went into the pigs. The whole herd rushed down the steep bank into the lake and drowned.
34 When the men taking care of the pigs saw this, they ran to spread the news in the town and on the farms.

35 The people went out to see what had happened, and when they came to Jesus, they also found the man. The demons had gone out of him, and he was sitting there at the feet of Jesus. He had clothes on and was in his right mind. But the people were terrified.
36 Then all who had seen the man healed told about it.

37 Everyone from around Gerasat begged Jesus to leave, because they were so frightened.
When Jesus got into the boat to start back,
38 the man who had been healed begged to go with him. But Jesus sent him off and said,

39 “Go back home and tell everyone how much God has done for you.” The man then went all over town, telling everything that Jesus had done for him.

A Dying Girl and a Sick Woman

(Matthew 9.18-26; Mark 5.21-43)


40 Everyone had been waiting for Jesus, and when he came back, a crowd was there to welcome him. 41 Just then the man in charge of the synagogue came and knelt down in front of Jesus. His name was Jairus, and he begged Jesus to come to his home

42 because his twelve-year-old child was dying. She was his only daughter.
While Jesus was on his way, people were crowding all around him.

43 In the crowd was a woman who had been bleeding for twelve years. She had spent everything she had on doctors, t but none of them could make her well.

44 As soon as she came up behind Jesus and barely touched his clothes, her bleeding stopped.

45 “Who touched me?” Jesus asked.
While everyone was denying it, Peter said, “Master, people are crowding all around and pushing you from every side.”t
46 But Jesus answered, “Someone touched me, because I felt power going out from me.”

47 The woman knew that she could not hide, so she came trembling and knelt down in front of Jesus. She told everyone why she had touched him and that she had been healed at once.

48 Jesus said to the woman, “You are now well because of your faith. May God give you peace!”

49 While Jesus was speaking, someone came from Jairus' home and said, “Your daughter has died! Why bother the teacher anymore?”

50 When Jesus heard this, he told Jairus, “Don't worry! Have faith, and your daughter will get well.”
51 Jesus went into the house, but he did not let anyone else go with him, except Peter, John, James, and the girl's father and mother. 52 Everyone was crying and weeping for the girl. But Jesus said, “The child isn't dead. She is just asleep.”

53 The people laughed at him because they knew she was dead.
54 Jesus took hold of the girl's hand and said, “Child, get up!” 55 She came back to life and got right up. Jesus told them to give her something to eat. 56 Her parents were surprised, but Jesus ordered them not to tell anyone what had happened.