previous next

Marko 12

Mfano wa shamba la mizabibu na wakulima

(Mat 21:33-46; Luka 20:9-19)

1 Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali. 2 Wakati wa mavuno, alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akamletee sehemu ya mazao ya shamba lake. 3 Wale wakulima wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu. 4 Akamtuma tena mtumishi mwingine; huyu pia wakamwumiza kichwa na kumtendea vibaya. 5 Yule mwenye shamba akatuma mtumishi mwingine tena ambaye hao wakulima walimuua. Wengine wengi waliotumwa, baadhi yao walipigwa, na wengi wakauawa. 6 Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpenzi. Mwishowe akamtuma huyo akisema, ‘Watamjali mwanangu.’ 7 Lakini hao wakulima wakaambiana, ‘Huyu ndiye mrithi, basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu!’ 8 Kwa hiyo wakamkamata, wakamuua na kumtupa nje ya lile shamba la mizabibu.

9 “Basi, mwenye shamba atafanya nini? Atakuja kuwaangamiza hao wakulima na kulikodisha hilo shamba la mizabibu kwa watu wengine. 10 t Je, hamjasoma Maandiko haya? ‘Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.

11 Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu.’”

12 Makuhani wakuu, waalimu wa sheria na wazee walifahamu ya kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu. Kwa hiyo walijaribu kumtia nguvuni, lakini waliogopa umati wa watu. Basi, wakamwacha, wakaenda zao.

Kulipa kodi kwa Kaisari

(Mat 22:15-22; Luka 20:20-26)

13 Basi, baadhi ya Mafarisayo na wafuasi wa kikundi cha Herode walitumwa ili wamtege Yesu kwa maneno yake. 14 Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?” 15 Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.” 16 Wakamwonesha. Naye akawauliza, “Sura na chapa hii ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 17 Basi, Yesu akawaambia, “Ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.” Wakashangazwa sana naye.

Suala juu ya ufufuo

(Mat 22:23-33; Luka 20:27-40)

18 Masadukayo ambao husema kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu, wakamwuliza, 19 “Mwalimu, Mose alituagiza hivi: ‘Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.’ 20 Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto. 21 Ndugu wa pili akamwoa huyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na ndugu watatu hali kadhalika. 22 Wote saba walikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa. 23 Basi, siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wa nani? Wote saba walikuwa wamemwoa.” 24 Yesu akawaambia, “Nyinyi mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu. 25 Maana wafu watakapofufuka hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni. 26 Lakini kuhusu kufufuliwa kwa wafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katika sehemu inayohusu kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto? Mungu alimwambia Mose, ‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.’ 27 Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Nyinyi mmekosea sana.”

Amri kuu

(Mat 22:34-40; Luka 10:25-28)

28 Mmojawapo wa waalimu wa sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza, akamwuliza, “Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?” 29 Yesu akamjibu, “Ya kwanza ndiyo hii: ‘Sikiliza Israeli! Bwana Mungu wetu, ndiye peke yake Bwana. 30 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.’ 31 Na ya pili ndiyo hii: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ Hakuna amri nyingine iliyo kubwa zaidi kuliko hizi.”

32 Basi, yule mwalimu wa sheria akamwambia, “Vyema Mwalimu! Umesema ukweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe. Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko tambiko na sadaka zote za kuteketezwa.” 34 Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwa ujasiri, akamwambia, “Wewe huko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hayo, hakuna mtu aliyethubutu tena kumwuliza kitu.

Suala juu ya Kristo

(Mat 22:41-46; Luka 20:41-44)

35 Wakati Yesu alipokuwa akifundisha hekaluni, aliuliza, “Mbona waalimu wa sheria wanasema ya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? 36 t Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.’

37 “Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?”

Yesu anawaonya watu kuhusu waalimu wa sheria

(Mat 23:1-36; Luka 20:45-47)

Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.

38 Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi, 39 na kuchukua nafasi za heshima katika karamu. 40 Huwadhulumu wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu! Siku ya hukumu watapata adhabu kali.”

Sadaka ya mama mjane

(Luka 21:1-4)

41 Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina ya hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi. 42 Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha. 43 Hapo Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Kweli nawaambieni, mama huyu mjane maskini ametia katika sanduku la hazina kiasi kikubwa kuliko walichotia wengine wote. 44 Maana wengine wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”

Mark 12

1 And he began to speak unto them in parables. A man planted a vineyard, and set a hedge about it, and digged a pit for the winepress, and built a tower, and let it out to husbandmen, and went into another country.2 And at the season he sent to the husbandmen a servant, that he might receive from the husbandmen of the fruits of the vineyard.3 And they took him, and beat him, and sent him away empty.4 And again he sent unto them another servant; and him they wounded in the head, and handled shamefully.5 And he sent another; and him they killed: and many others; beating some, and killing some.6 He had yet one, a beloved son: he sent him last unto them, saying, They will reverence my son.7 But those husbandmen said among themselves, This is the heir; come, let us kill him, and the inheritance shall be ours.8 And they took him, and killed him, and cast him forth out of the vineyard.9 What therefore will the lord of the vineyard do? he will come and destroy the husbandmen, and will give the vineyard unto others.10 Have ye not read even this scripture: The stone which the builders rejected, The same was made the head of the corner;

11 This was from the Lord, And it is marvellous in our eyes?

12 And they sought to lay hold on him; and they feared the multitude; for they perceived that he spake the parable against them: and they left him, and went away.13 And they send unto him certain of the Pharisees and of the Herodians, that they might catch him in talk.14 And when they were come, they say unto him, Teacher, we know that thou art true, and carest not for any one; for thou regardest not the person of men, but of a truth teachest the way of God: Is it lawful to give tribute unto Caesar, or not?15 Shall we give, or shall we not give? But he, knowing their hypocrisy, said unto them, Why make ye trial of me? bring me a denarius, that I may see it.16 And they brought it. And he saith unto them, Whose is this image and superscription? And they said unto him, Caesar’s.17 And Jesus said unto them, Render unto Caesar the things that are Caesar’s, and unto God the things that are God’s. And they marvelled greatly at him.18 And there come unto him Sadducees, who say that there is no resurrection; and they asked him, saying,19 Teacher, Moses wrote unto us, If a man’s brother die, and leave a wife behind him, and leave no child, that his brother should take his wife, and raise up seed unto his brother.20 There were seven brethren: and the first took a wife, and dying left no seed;21 and the second took her, and died, leaving no seed behind him; and the third likewise:22 and the seven left no seed. Last of all the woman also died.23 In the resurrection whose wife shall she be of them? for the seven had her to wife.24 Jesus said unto them, Is it not for this cause that ye err, that ye know not the scriptures, nor the power of God?25 For when they shall rise from the dead, they neither marry, nor are given in marriage; but are as angels in heaven.26 But as touching the dead, that they are raised; have ye not read in the book of Moses, in the place concerning the Bush, how God spake unto him, saying, I am the God of Abraham, and the God of Isaac, and the God of Jacob?27 He is not the God of the dead, but of the living: ye do greatly err.28 And one of the scribes came, and heard them questioning together, and knowing that he had answered them well, asked him, What commandment is the first of all?29 Jesus answered, The first is, Hear, O Israel; The Lord our God, the Lord is one:30 and thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind, and with all thy strength.31 The second is this, Thou shalt love thy neighbor as thyself. There is none other commandment greater than these.32 And the scribe said unto him, Of a truth, Teacher, thou hast well said that he is one; and there is none other but he:33 and to love him with all the heart, and with all the understanding, and with all the strength, and to love his neighbor as himself, is much more than all whole burnt-offerings and sacrifices.34 And when Jesus saw that he answered discreetly, he said unto him, Thou art not far from the kingdom of God. And no man after that durst ask him any question.35 And Jesus answered and said, as he taught in the temple, How say the scribes that the Christ is the son of David?36 David himself said in the Holy Spirit, The Lord said unto my Lord, Sit thou on my right hand, Till I make thine enemies the footstool of thy feet.

37 David himself calleth him Lord; and whence is he his son? And the common people heard him gladly.38 And in his teaching he said, Beware of the scribes, who desire to walk in long robes, and to have salutations in the marketplaces,39 and chief seats in the synagogues, and chief places at feasts:40 they that devour widows’ houses, and for a pretence make long prayers; these shall receive greater condemnation.41 And he sat down over against the treasury, and beheld how the multitude cast money into the treasury: and many that were rich cast in much.42 And there came a poor widow, and she cast in two mites, which make a farthing.43 And he called unto him his disciples, and said unto them, Verily I say unto you, This poor widow cast in more than all they that are casting into the treasury:44 for they all did cast in of their superfluity; but she of her want did cast in all that she had, even all her living.