MK. 12
Mfano wa Wapangaji Waovu
1 t tAkaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. 2 Hata kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu. 3 Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu. 4 Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha za kichwa, wakamfanyia jeuri. 5 Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua. 6 Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu. 7 Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. 8 tWakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu. 9 basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.
10 tHata andiko hili hamjalisoma,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
11 Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu?
12 Nao wakatafuta kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao.Swali juu ya Kulipa Kodi
13 t tWakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno. 14 Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo? 15 Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione. 16 Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.
17 tYesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.Swali juu ya Kufufuka
18 tKisha Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza na kusema, 19 tMwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao. 20 Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao. 21 Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika; 22 hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 23 Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye. 24 Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? 25 Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. 26 tNa kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?
27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.Amri ya Kwanza
28 t tNa mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? 29 tYesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; 30 tnawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. 31 tNa ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. 32 tYule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye; 33 tna kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.
34 tNaye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo.Swali juu ya Mwana wa Daudi
35 tHata Yesu alipokuwa akifundisha katika hekalu, alijibu, akasema, Husemaje waandishi ya kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi?
36 tDaudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu,
Bwana alimwambia Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,
Hata niwawekapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.
37 Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.Yesu Awashutumu Waandishi
38 tAkawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, 39 na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele katika karamu;
40 ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa.Sadaka ya Mjane
41 t tNaye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. 42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. 43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; 44 tmaana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
MARK 12
Renters of a Vineyard
(Matthew 21.33-46; Luke 20.9-19)
1 t Jesus then told them this story:
A farmer once planted a vineyard. He built a wall around it and dug a pit to crush the grapes in. He also built a lookout tower. Then he rented out his vineyard and left the country.
2 When it was harvest time, he sent a servant to get his share of the grapes.
3 The renters grabbed the servant, beat him up, and sent him away without a thing.
4 The owner sent another servant, but the renters beat him on the head and insulted him terribly.
5 Then the man sent another servant, and they killed him. He kept sending servant after servant. They beat some of them and killed some.
6 The owner had a son he loved very much. Finally, he sent his son to the renters because he thought they would respect him. 7 But they said to themselves, “Someday he will own this vineyard. Let's kill him! That way we can have it all for ourselves.”
8 So they grabbed the owner's son, killed him, and threw his body out of the vineyard.
9 Jesus asked, “What do you think the owner of the vineyard will do? He will come and kill those renters and let someone else have his vineyard.
10 t You surely know that the Scriptures say,
‘The stone the builders
tossed aside
is now the most important
stone of all.
11 This is something
the Lord has done,
and it is amazing to us.’ ”
12 The leaders knew that Jesus was really talking about them, and they wanted to arrest him. But because they were afraid of the crowd, they let him alone and left.Paying Taxes
(Matthew 22.15-22; Luke 20.20-26)
13 The Pharisees got together with Herod's followers.t Then they sent some men to trick Jesus into saying something wrong.
14 They went to him and said, “Teacher, we know that you are honest. You treat everyone with the same respect, no matter who they are. And you teach the truth about what God wants people to do. Tell us, should we pay taxes to the Emperor or not?”
15 Jesus knew what they were up to, and he said, “Why are you trying to test me? Show me a coin!”
16 They brought him a silver coin, and he asked, “Whose picture and name are on it?”
“The Emperor's,” they answered.
17 Then Jesus told them, “Give the Emperor what belongs to him and give God what belongs to God.” The men were amazed at Jesus.Life in the Future World
(Matthew 22.23-33; Luke 20.27-40)
18 t The Sadducees did not believe that people would rise to life after death. So some of them came to Jesus and said:
19 t Teacher, Moses wrote that if a married man dies and has no children, his brother should marry the widow. Their first son would then be thought of as the son of the dead brother. 20 There were once seven brothers. The first one married, but died without having any children. 21 The second brother married his brother's widow, and he also died without having children. The same thing happened to the third brother, 22 and finally to all seven brothers. At last the woman died.
23 When God raises people from death, whose wife will this woman be? After all, she had been married to all seven brothers.
24 Jesus answered:
You are completely wrong! You don't know what the Scriptures teach. And you don't know anything about the power of God. 25 When God raises people to life, they won't marry. They will be like the angels in heaven. 26 t You surely know about people being raised to life. You know that in the story about Moses and the burning bush, God said, “I am the God worshiped by Abraham, Isaac, and Jacob.”t
27 He isn't the God of the dead, but of the living. You Sadducees are all wrong.The Most Important //Commandment
(Matthew 22.34-40; Luke 10.25-28)
28 t One of the teachers of the Law of Moses came up while Jesus and the Sadducees were arguing. When he heard Jesus give a good answer, he asked him, “What is the most important commandment?”
29 t Jesus answered, “The most important one says: ‘People of Israel, you have only one Lord and God. 30 You must love him with all your heart, soul, mind, and strength.’
31 t The second most important commandment says: ‘Love others as much as you love yourself.’ No other commandment is more important than these.”
32 t The man replied, “Teacher, you are certainly right to say there is only one God.
33 t It is also true that we must love God with all our heart, mind, and strength, and that we must love others as much as we love ourselves. These commandments are more important than all the sacrifices and offerings that we could possibly make.”
34 When Jesus saw that the man had given a sensible answer, he told him, “You are not far from God's kingdom.” After this, no one dared ask Jesus any more questions.About David's Son
(Matthew 22.41-46; Luke 20.41-44)
35 As Jesus was teaching in the temple, he said, “How can the teachers of the Law of Moses say the Messiah will come from the family of King David?
36 t The Holy Spirit led David to say,
‘The Lord said to my Lord:
Sit at my right sidet
until I make your enemies
into a footstool for you.’
37 If David called the Messiah his Lord, how can the Messiah be his son?”t
The large crowd enjoyed listening to Jesus teach.Jesus Condemns the Pharisees //and the Teachers of the Law of Moses
(Matthew 23.1-36; Luke 20.45-47)
38 As Jesus was teaching, he said:
Guard against the teachers of the Law of Moses! They love to walk around in long robes and be greeted in the market. 39 They like the front seats in the synagogues and the best seats at banquets.
40 But they cheat widows out of their homes and pray long prayers just to show off. They will be punished most of all.A Widow's Offering
(Luke 21.1-4)
41 Jesus was sitting in the temple near the offering box and watching people put in their gifts. He noticed that many rich people were giving a lot of money. 42 Finally, a poor widow came up and put in two coins worth only a few pennies.
43 Jesus told his disciples to gather around him. Then he said:
I tell you that this poor widow has put in more than all the others. 44 Everyone else gave what they didn't need. But she is very poor and gave everything she had. Now she doesn't have a cent to live on.