previous next

MK. 16

Kufufuka kwa Yesu

1  tHata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. 2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza; 3 wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?

4 Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno.
5 Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. 6 Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka. 7 tLakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia.

8 Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.

Yesu Amtokea Mariamu Magdalene


[ 9 tNaye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. 10 Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia.

11 Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili


12  tBaada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.

13 Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki.

Yesu Awatuma Wanafunzi


14  tBaadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. 15 tAkawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 tAaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 17 tNa ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

18 twatashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Kupaa kwa Yesu


19  tBasi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20 tNao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]

MARK 16

Jesus Is Alive

(Matthew 28.1-8; Luke 24.1-12; John 20.1-10)

1 After the Sabbath, Mary Magdalene, Salome, and Mary the mother of James bought some spices to put on Jesus' body. 2 Very early on Sunday morning, just as the sun was coming up, they went to the tomb. 3 On their way, they were asking one another, “Who will roll the stone away from the entrance for us?”

4 But when they looked, they saw that the stone had already been rolled away. And it was a huge stone!

5 The women went into the tomb, and on the right side they saw a young man in a white robe sitting there. They were alarmed.
6 The man said, “Don't be alarmed! You are looking for Jesus from Nazareth, who was nailed to a cross. God has raised him to life, and he isn't here. You can see the place where they put his body.

7 t Now go and tell his disciples, and especially Peter, that he will go ahead of you to Galilee. You will see him there, just as he told you.”

8 When the women ran from the tomb, they were confused and shaking all over. They were too afraid to tell anyone what had happened.

ONE OLD ENDING TO MARK'S GOSPEL

Jesus Appears to Mary Magdalene

(Matthew 28.9,10; John 20.11-18)


9 Very early on the first day of the week, after Jesus had risen to life, he appeared to Mary Magdalene. Earlier he had forced seven demons out of her. 10 She left and told his friends, who were crying and mourning.

11 Even though they heard that Jesus was alive and that Mary had seen him, they still would not believe it.

Jesus Appears to Two Disciples

(Luke 24.13-35)


12 Later, Jesus appeared in another form to two disciples, as they were on their way out of the city.

13 But when these disciples told what had happened, the others would not believe either.

What Jesus' Followers Must Do

(Matthew 28.16-20; Luke 24.36-49; John 20.19-23; Acts 1.6-8)


14 Afterwards, Jesus appeared to his eleven disciples as they were eating. He scolded them because they were too stubborn to believe the ones who had seen him after he had been raised to life.

15 t Then he told them:
Go and preach the good news to everyone in the world.
16 Anyone who believes me and is baptized will be saved. But anyone who refuses to believe me will be condemned. 17 Everyone who believes me will be able to do wonderful things. By using my name they will force out demons, and they will speak new languages.

18 They will handle snakes and will drink poison and not be hurt. They will also heal sick people by placing their hands on them.

Jesus Returns to Heaven

(Luke 24.50-53; Acts 1.9-11)


19  t After the Lord Jesus had said these things to the disciples, he was taken back up to heaven where he sat down at the right sidet of God.

20 Then the disciples left and preached everywhere. The Lord was with them, and the miracles they worked proved that their message was true.

ANOTHER OLD ENDING TO MARK'S GOSPEL


9-10 The women quickly told Peter and his friends what had happened. Later, Jesus sent the disciples to the east and to the west with his sacred and everlasting message of how people can be saved forever.