previous next

MK. 2

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

1  tAkaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. 2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. 3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. 4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, 7 tMbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? 8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? 9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? 10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), 11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.

12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.

Yesu Amwita Lawi


13  tAkatoka tena, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha. 14 tHata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata. 15 Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata. 16 Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Swali kuhusu Kufunga


18  tNao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? 19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga. 20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile. 21 Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi.

22 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya.

Amri Kuhusu Sabato


23  t tIkawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke. 24 Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato? 25 tAkawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa ana haja, na kuona njaa, yeye na wenziwe? 26 tJinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiathari, akaila mikate ile ya Wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe? 27 tAkawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. 28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

MARK 2

Jesus Heals a Man //Who Could Not Walk

(Matthew 9.1-8; Luke 5.17-26)

1 Jesus went back to Capernaum, and a few days later people heard that he was at home.t

2 Then so many of them came to the house that there wasn't even standing room left in front of the door.
Jesus was still teaching
3 when four people came up, carrying a man on a mat because he could not walk.

4 But because of the crowd, they could not get him to Jesus. So they made a hole in the rooft above him and let the man down in front of everyone.

5 When Jesus saw how much faith they had, he said to the man, “My friend, your sins are forgiven.”
6 Some of the teachers of the Law of Moses were sitting there. They started wondering,

7 “Why would he say such a thing? He must think he is God! Only God can forgive sins.”
8 At once, Jesus knew what they were thinking, and he said, “Why are you thinking such things? 9 Is it easier for me to tell this man his sins are forgiven or to tell him to get up and pick up his mat and go on home? 10 I will show you that the Son of Man has the right to forgive sins here on earth.” So Jesus said to the man,

11 “Get up! Pick up your mat and go on home.”

12 The man got right up. He picked up his mat and went out while everyone watched in amazement. They praised God and said, “We have never seen anything like this!”

Jesus Chooses Levi

(Matthew 9.9-13; Luke 5.27-32)


13 Once again, Jesus went to the shore of Lake Galilee. A large crowd gathered around him, and he taught them.

14 As he walked along, he saw Levi, the son of Alphaeus. Levi was sitting at the place for paying taxes, and Jesus said to him, “Follow me!” So he got up and went with Jesus.

15 Later, Jesus and his disciples were having dinner at Levi's house.t Many tax collectorst and other sinners had become followers of Jesus, and they were also guests at the dinner.

16 Some of the teachers of the Law of Moses were Pharisees, and they saw Jesus eating with sinners and tax collectors. So they asked his disciples, “Why does he eat with tax collectors and sinners?”

17 Jesus heard them and answered, “Healthy people don't need a doctor, but sick people do. I didn't come to invite good people to be my followers. I came to invite sinners.”

People Ask about Going //without Eating

(Matthew 9.14-17; Luke 5.33-39)


18 The followers of John the Baptist and the Pharisees often went without eating.t Some people came and asked Jesus, “Why do the followers of John and those of the Pharisees often go without eating, while your disciples never do?”

19 Jesus answered:
The friends of a bridegroom don't go without eating while he is still with them.

20 But the time will come when he will be taken from them. Then they will go without eating.

21 No one patches old clothes by sewing on a piece of new cloth. The new piece would shrink and tear a bigger hole.

22 No one pours new wine into old wineskins. The wine would swell and burst the old skins.t Then the wine would be lost, and the skins would be ruined. New wine must be put into new wineskins.

A Question about //the Sabbath

(Matthew 12.1-8; Luke 6.1-5)


23  t One Sabbath Jesus and his disciples were walking through some wheat fields. His disciples were picking grains of wheat as they went along.t

24 Some Pharisees asked Jesus, “Why are your disciples picking grain on the Sabbath? They are not supposed to do that!”
25  t Jesus answered, “Haven't you read what David did when he and his followers were hungry and in need?

26 t It was during the time of Abiathar the high priest. David went into the house of God and ate the sacred loaves of bread that only priests are allowed to eat. He also gave some to his followers.”
27 Jesus finished by saying, “People were not made for the good of the Sabbath. The Sabbath was made for the good of people. 28 So the Son of Man is Lord over the Sabbath.”