Marko 3
Yesu anamponya mwenye mkono uliopooza
(Mat 12:9-14; Luka 6:6-11)
1 Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza. 2 Humo, baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya Sabato ili wapate kumshtaki. 3 Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, “Njoo hapa katikati.” 4 Kisha, akawauliza, “Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao hawakusema neno. 5 Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena. 6 Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu.
Umati wa watu kando ya ziwa
7 Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea, 8 Idumea, ngambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda. 9 Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga. 10 Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa. 11 Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaza sauti, “Wewe ni Mwana wa Mungu!” 12 Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.
Yesu anawateua mitume kumi na wawili
(Mat 10:1-4; Luka 6:12-16)
13 Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea, 14 naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume,t wakae naye, awatume kuhubiri 15 na wawe na uwezo wa kuwafukuza pepo. 16 Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro), 17 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake “Wanangurumo”), 18 Andrea na Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanaani na 19 Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
Yesu na Beelzebuli
(Mat 12:22-32; Luka 11:14-23; 12:10)
20 Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula. 21 Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba ana wazimu.
22 Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.” 23 Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano, “Shetani anawezaje kumfukuza Shetani? 24 Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopingana, utawala huo hauwezi kudumu. 25 Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia. 26 Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa.
27 “Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyanganya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyanganya mali yake.
28 “Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote; 29 lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele.” ( 30 Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”)
Mama na ndugu za Yesu
(Mat 12:46-50; Luka 8:19-21)
31 Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kumwita. 32 Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, watu wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona.” 33 Yesu akawaambia, “Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?” 34 Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, “Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. 35 Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu.”
Mark 3
1 And he entered again into the synagogue; and there was a man there who had his hand withered.2 And they watched him, whether he would heal him on the sabbath day; that they might accuse him.3 And he saith unto the man that had his hand withered, Stand forth.4 And he saith unto them, Is it lawful on the sabbath day to do good, or to do harm? to save a life, or to kill? But they held their peace.5 And when he had looked round about on them with anger, being grieved at the hardening of their heart, he saith unto the man, Stretch forth thy hand. And he stretched it forth; and his hand was restored.6 And the Pharisees went out, and straightway with the Herodians took counsel against him, how they might destroy him.7 And Jesus with his disciples withdrew to the sea: and a great multitude from Galilee followed; and from Judaea,8 and from Jerusalem, and from Idumaea, and beyond the Jordan, and about Tyre and Sidon, a great multitude, hearing what great things he did, came unto him.9 And he spake to his disciples, that a little boat should wait on him because of the crowd, lest they should throng him:10 for he had healed many; insomuch that as many as had plagues pressed upon him that they might touch him.11 And the unclean spirits, whensoever they beheld him, fell down before him, and cried, saying, Thou art the Son of God.12 And he charged them much that they should not make him known.13 And he goeth up into the mountain, and calleth unto him whom he himself would; and they went unto him.14 And he appointed twelve, that they might be with him, and that he might send them forth to preach,15 and to have authority to cast out demons:16 and Simon he surnamed Peter;17 and James the son of Zebedee, and John the brother of James; and them he surnamed Boanerges, which is, Sons of thunder:18 and Andrew, and Philip, and Bartholomew, and Matthew, and Thomas, and James the son of Alphaeus, and Thaddaeus, and Simon the Cananaean,19 and Judas Iscariot, who also betrayed him. And he cometh into a house.20 And the multitude cometh together again, so that they could not so much as eat bread.21 And when his friends heard it, they went out to lay hold on him: for they said, He is beside himself.22 And the scribes that came down from Jerusalem said, He hath Beelzebub, and, By the prince of the demons casteth he out the demons.23 And he called them unto him, and said unto them in parables, How can Satan cast out Satan?24 And if a kingdom be divided against itself, that kingdom cannot stand.25 And if a house be divided against itself, that house will not be able to stand.26 And if Satan hath risen up against himself, and is divided, he cannot stand, but hath an end.27 But no one can enter into the house of the strong man, and spoil his goods, except he first bind the strong man; and then he will spoil his house.28 Verily I say unto you, All their sins shall be forgiven unto the sons of men, and their blasphemies wherewith soever they shall blaspheme:29 but whosoever shall blaspheme against the Holy Spirit hath never forgiveness, but is guilty of an eternal sin:30 because they said, He hath an unclean spirit.31 And there come his mother and his brethren; and, standing without, they sent unto him, calling him.32 And a multitude was sitting about him; and they say unto him, Behold, thy mother and thy brethren without seek for thee.33 And he answereth them, and saith, Who is my mother and my brethren?34 And looking round on them that sat round about him, he saith, Behold, my mother and my brethren!35 For whosoever shall do the will of God, the same is my brother, and sister, and mother.