MK. 3
Mtu Mwenye Mkono Uliopooza
1 tAkaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza; 2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. 3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4 Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza. 5 tAkawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
6 tMara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza.Watu wengi kando ya Ziwa
7 tNaye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Uyahudi, 8 tna Yerusalemu, na Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea. 9 tAkawaambia wanafunzi wake ya kwamba chombo kidogo kikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga. 10 Maana aliponya wengi, hata wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa. 11 tNa pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.
12 tAkawakataza sana, wasimdhihirishe.Yesu Awateua wale Kumi na Wawili
13 tAkapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. 14 Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri, 15 tena wawe na amri ya kutoa pepo. 16 tAkawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro; 17 tna Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; 18 na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,
19 na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.Yesu na Belzebuli
Kisha akaingia nyumbani. 20 Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate. 21 tJamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili. 22 ttNao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo. 23 Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani? 24 Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama; 25 na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama. 26 Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo. 27 Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake. 28 Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; 29 tbali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
30 tkwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.Mfano wa Mpanzi
31 tWakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita. 32 Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. 33 Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani? 34 Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu! 35 Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.
MARK 3
A Man with a Paralyzed Hand
(Matthew 12.9-14; Luke 6.6-11)
1 The next time Jesus went into the synagogue, a man with a paralyzed hand was there.
2 The Phariseest wanted to accuse Jesus of doing something wrong, and they kept watching to see if Jesus would heal him on the Sabbath.
3 Jesus told the man to stand up where everyone could see him.
4 Then he asked, “On the Sabbath should we do good deeds or evil deeds? Should we save someone's life or destroy it?” But no one said a word.
5 Jesus was angry as he looked around at the people. Yet he felt sorry for them because they were so stubborn. Then he told the man, “Stretch out your hand.” He did, and his bad hand was healed.
6 The Pharisees left. And at once they started making plans with Herod's followerst to kill Jesus.Large Crowds Come to Jesus
7 Jesus led his disciples down to the shore of the lake. Large crowds followed him from Galilee, Judea, 8 and Jerusalem. People came from Idumea, as well as other places east of the Jordan River. They also came from the region around the towns of Tyre and Sidon. All of these crowds came because they had heard what Jesus was doing.
9 t He even had to tell his disciples to get a boat ready to keep him from being crushed by the crowds.
10 After Jesus had healed many people, the other sick people begged him to let them touch him. 11 And whenever any evil spirits saw Jesus, they would fall to the ground and shout, “You are the Son of God!”
12 But Jesus warned the spirits not to tell who he was.Jesus Chooses //His Twelve Apostles
(Matthew 10.1-4; Luke 6.12-16)
13 Jesus decided to ask some of his disciples to go up on a mountain with him, and they went. 14 Then he chose twelve of them to be his apostles, t so they could be with him. He also wanted to send them out to preach 15 and to force out demons. 16 Simon was one of the twelve, and Jesus named him Peter. 17 There were also James and John, the two sons of Zebedee. Jesus called them Boanerges, which means “Thunderbolts.” 18 Andrew, Philip, Bartholomew, Matthew, Thomas, James son of Alphaeus, and Thaddaeus were also apostles. The others were Simon, known as the Eager One, t
19 and Judas Iscariot, t who later betrayed Jesus.Jesus and the Ruler //of Demons
(Matthew 12.22-32; Luke 11.14-23; 12.10)
20 Jesus went back home, t and once again such a large crowd gathered that there was no chance even to eat.
21 When Jesus' family heard what he was doing, they thought he was crazy and went to get him under control.
22 t Some teachers of the Law of Moses came from Jerusalem and said, “This man is under the power of Beelzebul, the ruler of demons! He is even forcing out demons with the help of Beelzebul.”
23 Jesus told the people to gather around him. Then he spoke to them in riddles and said:
How can Satan force himself out? 24 A nation whose people fight each other won't last very long. 25 And a family that fights won't last long either.
26 So if Satan fights against himself, that will be the end of him.
27 How can anyone break into the house of a strong man and steal his things, unless he first ties up the strong man? Then he can take everything.
28 I promise you that any of the sinful things you say or do can be forgiven, no matter how terrible those things are.
29 t But if you speak against the Holy Spirit, you can never be forgiven. That sin will be held against you forever.
30 Jesus said this because the people were saying that he had an evil spirit in him.Jesus' Mother and Brothers
(Matthew 12.46-50; Luke 8.19-21)
31 Jesus' mother and brothers came and stood outside. Then they sent someone with a message for him to come out to them.
32 The crowd sitting around Jesus told him, “Your mother and your brothers and sisterst are outside and want to see you.”
33 Jesus asked, “Who is my mother and who are my brothers?” 34 Then he looked at the people sitting around him and said, “Here are my mother and my brothers. 35 Anyone who obeys God is my brother or sister or mother.”