previous next

MT. 24

Kuharibiwa kwa Hekalu Kwatabiriwa

1  tYesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu.

2 tNaye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.

Ishara za Mwisho wa Nyakati


3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 tKwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6 tNanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7 tKwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.

8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.

Mateso Yatabiriwa


9  tWakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 tNdipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. 11 tNa manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12 tNa kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13 tLakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

14 tTena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Chukizo la Uharibifu


15  tBasi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 17 tnaye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 tOmbeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21 tKwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 tKwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 tBasi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

28 tKwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

Kuja kwa Mwana wa Adamu


29  tLakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 tndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

31 tNaye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

Funzo kutoka kwa Mtini


32 Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; 33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. 34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.

35 tMbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Haja ya kuwa Waangalifu


36  tWalakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 tKwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 tKwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 twasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40 tWakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42  tKesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. 43 tLakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.

44 tKwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.

Mtumwa Mwaminifu au asiye Mwaminifu


45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47 tAmin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48 tLakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51 tatamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

MATTHEW 24

The Temple Will Be Destroyed

(Mark 13.1,2; Luke 21.5,6)

1 After Jesus left the temple, his disciples came over and said, “Look at all these buildings!”

2 Jesus replied, “Do you see these buildings? They will certainly be torn down! Not one stone will be left in place.”

Warning about Trouble

(Mark 13.3-13; Luke 21.7-19)


3  t Later, as Jesus was sitting on the Mount of Olives, his disciples came to him in private and asked, “When will this happen? What will be the sign of your coming and of the end of the world?”

4 Jesus answered:
Don't let anyone fool you.

5 Many will come and claim to be me. They will say they are the Messiah, and they will fool many people.
6 You will soon hear about wars and threats of wars, but don't be afraid. These things will have to happen first, but that isn't the end. 7 t Nations and kingdoms will go to war against each other. People will starve to death, and in some places there will be earthquakes.

8 But this is just the beginning of troubles.
9  t You will be arrested, punished, and even killed. Because of me, you will be hated by people of all nations. 10 Many will give up and will betray and hate each other. 11 Many false prophets will come and fool a lot of people. 12 Evil will spread and cause many people to stop loving others. 13 t But if you keep on being faithful right to the end, you will be saved.

14 When the good news about the kingdom has been preached all over the world and told to all nations, the end will come.

The Horrible Thing

(Mark 13.14-23; Luke 21.20-24)


15  t Someday you will see that “Horrible Thing” in the holy place, just as the prophet Daniel said. Everyone who reads this must try to understand! 16 If you are living in Judea at that time, run to the mountains. 17 t If you are on the rooft of your house, don't go inside to get anything. 18 If you are out in the field, don't go back for your coat. 19 It will be a terrible time for women who are expecting babies or nursing young children. 20 And pray that you won't have to escape in winter or on a Sabbath.t 21 t This will be the worst time of suffering since the beginning of the world, and nothing this terrible will ever happen again.

22 If God doesn't make the time shorter, no one will be left alive. But because of God's chosen ones, he will make the time shorter.
23 Someone may say, “Here is the Messiah!” or “There he is!” But don't believe it. 24 False messiahs and false prophets will come and work great miracles and signs. They will even try to fool God's chosen ones. 25 But I have warned you ahead of time. 26 t If you are told the Messiah is out in the desert, don't go there! And if you are told he is in some secret place, don't believe it! 27 The coming of the Son of Man will be like lightning that can be seen from east to west.

28 t Where there is a corpse, there will always be vultures.t

When the Son of Man //Appears

(Mark 13.24-27; Luke 21.25-28)


29  t Right after those days of suffering,
“The sun will become dark,
and the moon
will no longer shine.
The stars will fall,
and the powers in the skyt
will be shaken.”
30  t Then a sign will appear in the sky. And there will be the Son of Man.t All nations on earth will weep when they see the Son of Man coming on the clouds of heaven with power and great glory.

31 At the sound of a loud trumpet, he will send his angels to bring his chosen ones together from all over the earth.

A Lesson from a Fig Tree

(Mark 13.28-31; Luke 21.29-33)


32 Learn a lesson from a fig tree. When its branches sprout and start putting out leaves, you know summer is near. 33 So when you see all these things happening, you will know the time has almost come.t 34 I can promise you that some of the people of this generation will still be alive when all this happens.

35 The sky and the earth won't last forever, but my words will.

No One Knows the Day //or Time

(Mark 13.32-37; Luke 17.26-30,34-36)


36 No one knows the day or hour. The angels in heaven don't know, and the Son himself doesn't know.t Only the Father knows. 37 t When the Son of Man appears, things will be just as they were when Noah lived. 38 People were eating, drinking, and getting married right up to the day the flood came and Noah went into the big boat.

39 t They didn't know anything was happening until the flood came and swept them all away. This is how it will be when the Son of Man appears.
40 Two men will be in the same field, but only one will be taken. The other will be left. 41 Two women will be together grinding grain, but only one will be taken. The other will be left. 42 So be on your guard! You don't know when your Lord will come. 43 t Homeowners never know when a thief is coming, and they are always on guard to keep one from breaking in.

44 Always be ready! You don't know when the Son of Man will come.

Faithful and Unfaithful Servants

(Luke 12.35-48)


45 Who are faithful and wise servants? Who are the ones the master will put in charge of giving the other servants their food supplies at the proper time? 46 Servants are fortunate if their master comes and finds them doing their job. 47 You may be sure a servant who is always faithful will be put in charge of everything the master owns. 48 But suppose one of the servants thinks the master won't return until late. 49 Suppose this evil servant starts beating the other servants and eats and drinks with people who are drunk. 50 If that happens, the master will surely come on a day and at a time when the servant least expects him. 51 This servant will then be punished and thrown out with the ones who only pretended to serve their master. There they will cry and grit their teeth in pain.