MT. 28
Kufufuka kwa Yesu
1 tHata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. 2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. 3 tNa sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. 4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. 5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. 6 tHayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. 7 tNanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia. 8 Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. 9 Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
10 tKisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.Ripoti ya Walinzi
11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka. 12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13 twakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.Kutumwa kwa Wanafunzi
16 tNa wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. 17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. 18 tYesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 tBasi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 tna kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
MATTHEW 28
Jesus Is Alive
(Mark 16.1-8; Luke 24.1-12; John 20.1-10)
1 The Sabbath was over, and it was almost daybreak on Sunday when Mary Magdalene and the other Mary went to see the tomb. 2 Suddenly a strong earthquake struck, and the Lord's angel came down from heaven. He rolled away the stone and sat on it. 3 The angel looked as bright as lightning, and his clothes were white as snow.
4 The guards shook from fear and fell down, as though they were dead.
5 The angel said to the women, “Don't be afraid! I know you are looking for Jesus, who was nailed to a cross. 6 He isn't here! God has raised him to life, just as Jesus said he would. Come, see the place where his body was lying.
7 Now hurry! Tell his disciples he has been raised to life and is on his way to Galilee. Go there, and you will see him. This is what I came to tell you.”
8 The women were frightened and yet very happy, as they hurried from the tomb and ran to tell his disciples. 9 Suddenly Jesus met them and greeted them. They went near him, held on to his feet, and worshiped him.
10 Then Jesus said, “Don't be afraid! Tell my followers to go to Galilee. They will see me there.”Report of the Guard
11 While the women were on their way, some soldiers who had been guarding the tomb went into the city. They told the chief priests everything that had happened. 12 So the chief priests met with the leaders and decided to bribe the soldiers with a lot of money. 13 They said to the soldiers, “Tell everyone that Jesus' disciples came during the night and stole his body while you were asleep. 14 If the governort hears about this, we will talk to him. You won't have anything to worry about.”
15 The soldiers took the money and did what they were told. The people of Judea still tell each other this story.What Jesus' Followers //Must Do
(Mark 16.14-18; Luke 24.36-49; John 20.19-23; Acts 1.6-8)
16 t Jesus' eleven disciples went to a mountain in Galilee, where Jesus had told them to meet him.
17 They saw him and worshiped him, but some of them doubted.
18 Jesus came to them and said:
I have been given all authority in heaven and on earth! 19 t Go to the people of all nations and make them my disciples. Baptize them in the name of the Father, the Son, and the Holy Spirit, 20 and teach them to do everything I have told you. I will be with you always, even until the end of the world.